TATIZO LA KUTOJIMUDU KWA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL INCOMPETENCE)



Ni kufunguka kwa shingo ya kizazi kabla ya uchungu kuanza.
Nini tofauti kati ya Shingo ya uzazi kutojimudu na kufunguka kabla ya wakati?
Kutojimudu kwa shingo ya uzazi hutokea kufunguka mapema kwa njia ya uzazi katika kipindi cha miezi mitatu ya pili ya ujauzito kunakosababisha kutoka kwa mimba. Ili kuitwa kwamba shingo ya uzazi haijiwezi unatakiwa kuwa na vipindi viwili vinavyofuatana. Kwa hivyo shingo ya uzazi isiyojimudu humaanisha kujirudia kufunguka kwa shingo ya uzazi kabla ya uchungu.

Athari ya tatizo ikoje?
Athari halisi ya tatizo bado haijulikani lakini imelipotiwa kwamba athari za kujirudia kutokea kufunguka kwa shingo ya kizazi huwa ni asilimia 1 kati ya ujauzito zinazotokea. Kujirudia kutojimudu kwa shingo ya uzazi hutokea kwa asilimia 20- 30mwanamke aliye na shingo ya kizazi isiyojimudu na alipoteza  ujauzito zinazofuatana katika kipindi cha kati cha ujauzito kusikoambatana na maumivu huwa na uwezo wa asilimia 70-75 ya kuendelea na ujauzito mpaka mwisho bila matibabu yoyote
Nini husabaisha kufunguka kwa shingo ya kizazi kabla ya wakati?

Mfuko wa uzazi umetengenezwa kwa misuli laini tishu unganishi na mishipa ya damu. Mgawanyiko wa tishu hizi kwenye shingo ya uzazi huwa sio sawia kulinganisha na sehemu nyingine ya kizazi. Kuna misuli mingi kwenye mlango wa ndani na tishu unganishi nyingi sehemu ya nje. Utofauti wa muundo wa tishu kwenye mfuko shingo ya kizazi unaelezewa kuwa ni sababu inayosababisha kutojimudu kwa shingo ya kizazi na kupelekea kufunguka kabla ya kufika mwisho wa ujauzito.
Jinsi gani tatizo hutambuliwa?

Kwa miaka mingi, kutumia vidole kujua urefu wa shingo ya kizazi ni njia iliyokuwa ikitumika. Lakini kwa sasa matumizi ya ultrasound yamekuwa yakingezeka na kuwa njia muhimu katika utambuzi wa tatizo hili. Kuna utofauti mdogo kati ya mpimaji mmoja na mwingine kuhusu urefu wa shingo ya kizazi ukilinganisha na njia ya kidole. Ultrasound inauwezo wa kupima urefu wote wa shingo ya uzazi ukilinganisha na njia ya vidole ambayo hupima urefu wa shingo ya kizazi sehemu ya nje kwenye uke tu. Tafiti zinaonyesha kuwa na shingo ya kizazi fupi (chini ya sentimita 2.5) au kufunguka kwa shingo ya ndani ya uzazi kwenye wiki ya 24 kwa kutumia ultrasound hutabili kujifungua kabla ya wakati.

Kipimo gani cha kutegemewa kujua tatizo la shingo ya kizazi isiyojimudu?

Hufanyika awali kwa kuuliza historia, lakini kuna vipimo kadhaa vinavyoweza kufanyika. Uwezo w akupitisha mpira wa foley namba 16 au kitanua shingo ya kizazi namba 8 huweza maanisha kuna tatizo la shingo ya kizazi kutojimudu. Kuna kipimo cha ultrasound inayopimwa kupitia ukeni kuingia kwenye kizazi pia kwa ajiri ya kuangalia tabia na umbo la uzazi.

Kipimo gani cha kutegemewa kujua tatizo la shingo ya kizazi isiyojimudu?

Hufanyika awali kwa kuuliza historia, lakini kuna vipimo kadhaa vinavyoweza kufanyika. Uwezo w akupitisha mpira wa foley namba 16 au kitanua shingo ya kizazi namba 8 huweza maanisha kuna tatizo la shingo ya kizazi kutojimudu. Kuna kipimo cha ultrasound inayopimwa kupitia ukeni kuingia kwenye kizazi pia kwa ajiri ya kuangalia tabia na umbo la uzazi.
Vihatarishi

Kihatarishi kikuu ni kuwa na historia ya kupoteza ujauzito uliopita kutokana na kutojimudu kwa shingo ya kizazi. Matatizo ya kuzaliwa nayo ya kutofanyika vema kwa shingo ya kizazi na matumizi ya dawa ya DES yameripotiwa kuhusiana na tatizo hili. Vihatarishi vya kimazingira ni kama majeraha kwenye shingo ya kizazi, kukakwa kwa shingo ya kizazi, kutolewa baadhi ya sehemu ya shingo ya kizazi, kuchanika kutokana na kujifungua, na kutanuliwa kwa lazima kwa shingo ya kizazi na visababishi vingine vya majeruhi vinavyofanana pia huweza kusababisha kutojimudu kwa shingo ya kizazi.
Matibabu

Hakuna matibabu mengi yanayoweza kutibu tatizo hili ipasavyo. Matibabu huanza na kupumzika kitandani kwa mda Fulani na kufanyiwa upasujai wa kufunga shingo ya kizazi kwa mda.

Nani ni mteja wa kufungiwa shingo ya kizazi kwa mda?
Wanawake waliothibitishwa kwamba wana shingo ya kizazi isiyojimudu hufanyiwa upasuaji huu mdogo. Kitu cha msingi cha kuchagua mgonjwa wa kufungiwa shingo ya kizazi ni kutokuwa na uchungu. Kuwepo kwa uchungu kunamaanisha uchungu kabla ya wakati na matibabu haya hayafai kwa mtu huyu kwa sababu mimba huweza kutoka wakati wowote. Baadhi ya madaktari wanatoa hoja kwamba kufunguka kwa shingo ya kizazi kabla ya wakati kunaweza kusababisha kuanza kwa uchungu na kufanya zoezi la uchaguzi la nani afanyiwe upasuaji huu kuwa gumu. Hata hivyo hairuhusiwi kufanyiwa upasuaji huu mwanamke ambaye anauchungu.
 Tokeo la picha la CERVICAL INCOMPETENCE
Kipindi gani ni muafaka kwa ajiri ya kufanyiwa upasuaji huu?
Inashauriwa kwamba kufungwa kwa shingoya kizazi kwa mda kufanyike kwenye wiki  ya 13-16 za ujauzito. Kuna baadhi ya hali ambapo upasuaji huu husogezwa mbele kidogo inaweza kuwa kwa sababu mama amechelewa kuhudhuria kliniki au kutojimudu kumetokea bila kutarajiwa. Kwa watu kama hawa upasuaji unaweza kufanyika hadi wiki ya 23 za ujauzito. Mtoto anapokuwa tayari amefanyika na anaweza ishi  endapo atazaliwa upasuaji huu huwa haufanyiki mara nyingi.

Marufuku ya upasuaji huu ni nini?
Kuwepo kwa uchungu, nu marufuku ya kufanya upasuaji huu. Kupasuka kwa chupa ya uzazi, maambukizi ndani ya chupa ya uzazi, kutokuwa kwa mtoto ndani ya mfuko wa uzazi, nz matatizo mengine makubwa ya uumbaji wa mtoto huwa ni marufuku kufanyiwa upasuaji huu.
Madhara ya upasuaji huu ni yapi?

Madhara yanayohusiana na kufungwa kwa shingo ya kizazi kwa mda hugawanyika kwenye makundi mawili. Yale yanayotokana na upasujia na yale yanayotokea baadae. Madhara kutokana na upasuaji ni madhara ya dawa za usingizi,, majeraha kwenye tishu za mama, kutokwa na damu, maambukizi, kupasuka kwa chupa ya uzazi, na mimba kutoka. Madhara ya baadae ni kama kuchanika kwa shingo ya kizazi,kufanyika kwa fistula, na kuongezeka kujifungua kwa upasuaji.
Wakati gani shingo ya kizazi hufunguliwa?
Mishono ya kufunga shingo ya kizazi kwa mda hushauliwa kuondolewa kwenye wiki ya 37-38 za ujauzito kabla uchungu haujaanza ili kupunguza hatari ya uharibifu wa shingo ya kizazi na kuchanika kwa mfuko wa kizazi. Mara nyingi nyuzi huweza kutolewa kwenye ofisi na wakati mwingine inawezakuhitajika kuingia chumba maalumu cha upasuaji ili kutolewa chini ya kaputi.

No comments