Migraine ni tatizo ambalo halielezeki mpaka leo nini ni kisababishi, tatizo hili linapotokea mgonjwa hupata maumivu ya kichwa ya upande mmoja. Mara nyingi sana, maumivu haya ya kichwa huambatana na dalili kwenye macho au masikio zikijulikana kama viashilia au kitaalamu Aura ambazo hutokea maranyingi kabla ya kichwa kuanza kuuma na wakati mwingine wakati wa kichwa kuuma au baada ya kichwa kuuma.
Kipanda uso kinatokea sana kwa wanawake na linahusianishwa sana na urithisaji- pia tatizo hili linaelezewa kitaalamu kwamba kuna mabadiliko katika vina saba ambayo hutokea na hivyo huweza kutokea kwenye familia fulani.
Nini husababisha maumivu haya ya migraine?
Zamani ilijulikana kwamba kipanda uso kinasababishwa na mabadiliko yanayotokea katika mishipa ya damu ya kichwa, inaeleza kuwa kuna wakati mishipa ya damu husinyaa kwa muda na baadae hufuatiwa na kipindi cha kutanuka kwa mishipa hiyo hivo kuleta maumivu wakati wa kitendo hiki kinapotokea. Kwa sasa kuna maelezo yajulikanayo kama neurovascular theory ambapo yanasema kwamba kipanda uso husababishwa na matatizo/mabadiliko yanayotokea katika mfumo wa fahamu na matatizo hayo yanatokana na kubadilika kwa mpitisho wa virutubisho kutoka katika mishipa ya damu kwenda kwenye chembe hai za ubongo na hivo kusababsisha michomo kwenye mishipa ya fahamu kutokana na kukosa virutubisho hivyo.
Kuhusianishwa kwa vinasaba kunaonyesha kwamba asilimia 70 ya watu wenye kipanda uso wana ndugu wa tumbo moja wenye tatizo hili na pia mambo mengi ya kimazingira husababisha kupata kipanda uso kwa mtu aliye na vihatarishi vya ugonjwa huu.
Mgonjwa wa kipanda uso anapata dalili zipi?
Dalili za kipanda uso zinapotokea au kabla hazijatokea huwa na dalili za awali au viashiria kwamba ugonjwa unatokea, viashiria hivyo vimewekwa katika makundi manne kitaalamu prodrome, aura, headache na postdrome
Prodrome
Dalili hii hutokea siku moja au mbili kabla mtu hajashikwa na kipanda uso na huwa na dalili kati ya zifuatazo
Choo kikumu au kukosa choo
Msongo wa mawazo (depression)
Njaa kali
Kutotulia kimawazo au matendo
Mtoto kulia sana anaposhikwa
Kukakamaa kwa shingo
Kupata miayo mingi isiyozuilika
Aura
Kipindi hiki kinaweza kutokea kabla au baada ya kipanda uso kutokea. Aura hutokea kutokana na maabiliko kwenye mfumo wa fahamu na huja na dalili zinazodhuru mfumo wa hisia kama vile mtu anaweza kuona mwanga mkali unammulika wakati hakuna mwanga, kuhisi mguso mwilini. Mabadiliko mengine ni kwenye mgonjeo wa mwili na mfumo wa maongezi. Watu wengi wanapata kipanda uso pasipo kupata dalili hizi au aura na dalili hizi hutokea polepole na kuongezeka na hukaa kwa dakika 20 hai 60. Mifano ya aura ni
Matatizo ya kuona kama kuona maumbo, mwanga mkali au miali ya mwanga inamulika machoni
Kupoteza uwezo wa kuona
Kuhisi michomo ya pini au sindano
Ugumu katika maongezi kama vile kushindwa kueleweka unachoongea au kutamka maneno
Kwa mara chache sana aura inaweza kutokea na ganzi miguuni au kupoeza fahamu kwa miguu
Kushikwa na maumivu ya kichwa ya kipanda uso
Kama maumivu haya yasipotibiwa hukaa kwa masaa ma 4 hadi 72, lakini namna maumivu yanavyojirudiarudia kutokea hutofauiana kati ya mtu na mtu. Mtu mwingine anaweza kupata kipanda uso mara nyingi katika mwezi au mara chache. Mtu akiwa anapata kipanda uso anaweza kupata mambo kati ya yafuatayo
Maumivu upande mmoja au pande zote za kichwa
Maumivu ya kupwita,
Kupata shida anapokuwa kwenye mwanga
Kichefuchefu na kutapika
Kuona kwa mfifio vitu vinavyokuzunguka
Kizunguzungu na wakati mwingine hufuatiwa na kuzimia
Postdrome
Hiki ni Kipindi cha mwisho, hutokea baada ya kupata kipanda uso/maumivu ya kichwa-migraine, kipindi hichi mwathilika wa kipanda uso anaweza kuhisi ameisha au mtupu ingawa watu wengine wanaweza kuhisi wanafuraha ya uongo
Nini huchochea tatizo la kipanda uso?
Vitu/sababu zozote zinazoweza kusabaisha maumivu ya kichwa na mambo mengi yanayoweza kuamsha ugonjwa huu kama vile
Mabadiliko ya vichochezi mwili-homoni kwa mwanamke. Mabadiliko ya kichochezi mwili cha estrogen huamsha kipanda uso kama inavyoonekana kwa wanawake wengi wanaopata kipanda uso, wanawake wanaopata maumivu ya kichwa ya kipanda uso huripoti kwamba wametoka au wapo kwenye kipindi cha hedhi ambapo homoni hii ya estrogeni huwa imeshuka kwa kipindi hiki. Wanawake mengine wanapata maumivu haya wakati wa ujauzito au wanawake wanapokuwa kwenye kipindi cha kukoma kwa mzunguko wa hedhi(menopause) madawa ya homoni kama madawa ya mpango wa uzazi huamsha kipanda uso ingawa baadhi ya wanawake huweza kupata nafuu wanapopata awa hizi
Chakula. Vyakula vilivyochacha, vyenye chumvi nyingi na vyakula vya kusindikwa huweza kuamsha kipanda uso. Kifunga au kuruka mlo kunaweza kuamsha kipanda uso pia
Msongo wa mawazo
Kulala sana au kidogo
Madawa ya kutanua mishipa ya damu (vasodilators)
Kuvuta sigara
Kukaa kwenye mwanga mkali
harufu kali kama ya pafume madawa ya meno na petroli
Jeraha kichwani
Baridi kama barafu
Kutofanya mazoezi
Kunywa wine nyekundu (red wine)
Baadhi ya vyakula vinavyosemekana kuamsha kipanda uso ni;
Vinywaji vyenye cafeine
vinywaji vyenye sukari isiyo asili kama juis kola n.k
matunda aina ya citrus kama machungwa ndimu n.k
vyakula vyenye kemikali aina ya tyramine kama cheese zilizaokaa muda mrefu n.k
nyama yenye kemikali ya nitrates
Matibabu ya kipanda uso
Matibabu ya kipanda uso huwa ya aina mbili, kuondoa dalili na matibabu ya kuzuia kupata vipindi vya maumivu ya kichwa.Kwa wagonjwa ambao wanapata kipanda uso mara kwa mara wanatakiwa kujifunza kujizuia kutoka kwenye mambo au vitu vinavyowasababishia kupata dalili hizo.
Mgonjwa wa Kipanda uso anatakiwa kupimwa na kuangaliwa kama anavihatarishi vya ugonjwa wa moyo, kama anavyo matibabu ya haraka yanatakiwa kufanyika ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea na ikiwa anakuwa na vipindi vya Aura anatakiwa kupewa elimu juu ya hatari ya kupata kiharusi na wale ambao wanavuta sigara ni vema wakaambiwa madhara ya sigara katika tatizo walionalo
Matibabu ya dawa
Dawa za maumivu kama mgonjwa anapata maumivu ya kichwa
Dawa za kuzuia kipanda uso kutokea mara kwa mara
Dawa za kuondoa dalili kama kichefuchefu au kutapika
Matibabu ya kuzuia kupata kipanda uso
Mgojwa anatakiwa ajifunze vitu/tabia gani zinazosababisha kuamka kwa kipanda uso, endapo anamatumizi ya dawa zinazoamsha kipanda uso basi anatakiwa kuacha
Matibabu mengine anayoweza kupata ni yale dawa za kuzuia kupata dalili ya maumivu ya kichwa mara anapokuwa katika kipindi cha migraine na pia kuna dawa mgonjwa anaweza kupata kila baada ya muda flani kupita kwa ajili ya kuzuia kupata vipindi vingi vya kipanda uso.
Madhara yatokanayo na kipanda uso
Maumivu sugu ya kichwa au chronic migraine
Kifafa
Kiharusi
Kupata Aura endelevu dakika 30 hadi 60)
Kiharusi cha kutokana na kipanda uso ni nadra sana kutokea, lakini kinapotokea huwa na madhara makubwa yatokanayo na kipanda uso. Katika kipindi cha aura na maumivu ya kichwa ,mivilio ya damu huweza kutokea ndani ya ubongo lakini vilevile ni nadra.
Vihatarishi vya kupata kiharusi kwa mtu anayepata kipanda uso ni hivi vifuatavyo
Maumivu ya kichwa yanayofuatiwa na kipindi cha aura
Kuwa na jinsia ya kike
Uvutaji wa sigara
Matumizi ya hormoni ya estrogen kama kwa wanawake wanaotumia vidonge vya majira
No comments