Kwanza kabisa tuangalie udhibiti wa hormone katika mzunguko wa hedhi, yaani hormone zipi zinahusika na mzunguko wa hedhi na zinafanya vipi kazi.Kama inavyoonekana katika mchoro huu.
Katika ubongo kuna tezi ya hipothalmas inayozalisha hormone ya Gonadotropini hii hormone inachochea tezi ya pituitari ambayo nayo ipo kwenye ubongo kuzalisha hormone zifatazo
1.hormone chochezi ya mayai (FSH) ambayo huchochea kukua na kupevuka kwa mayai na kuchochea mfuko wa mayai (ovari) kuzalisha hormone za uzazi estrogen na progesterone.
2.Hormone ya lutea ambayo huchochea kuachiliwa kwa yai kutoka kwenye mfuko wa mayai (Ovulation).
Baadae estrogen na progesterone ambazo zinakazi kubwa katika mzunguko zinapokuwa zimezalishwa kwa kiasi cha kutosha zinafanya sasa tezi ya hipothalmus isizalishe tena Hormone ya gonadotropin na kuzuia mzunguko mzima.
Pindi unapokaribia hedhi estrogen na progesterone zinashuka kiwango ili kuruhusu Hipothalmus izalishe tena gonadotropin ili mzunguko uanze tena
JE DAWA ZA UZAZI WA MPANGO KAMA MAJIRA ,P2 NA NYINGINEZO ZINAATHIRI VIPI MZUNGUKO?
Kwanza kabisa ile dhana kwamba zinaacha sumu si kweli,
Unapomeza mfano vidonge ndani ya masaa 24 hadi 36 zinakuwa zimeshatolewa kabisa mwilini kupitia ini.
Sasa kwa nini mtu anaweza kukosa hedhi baada ya kuacha kutumia hizi dawa.
Dawa hizi zinakuwa na kemikali ambazo zinafanana na hormone ya progesterone na nyingine zina dawa inayofanana na estrogen.
Zinapoingia mwilini zinafanya kazi kama hormone hizo na kuziba vijishikizo (receptors) za hormone hizo, mwili huhisi kuwa kuna kiwango kikubwa cha hormone ya estrogen na progesterone matokeo yake hipothalmus inakuwa inactive na kuacha kuzalisha hormone ya gonadotropin na kuathiri uzalishwaji wa mayai na hedhi. Hadi mtu hapati ujauzito. Kwa hiyo znafanya kazi kwa kuvuruga huo mpangilio wa hormone.
Unapoacha kutumia tezi ya hipothalmus kurudia hali yake ya kawaida kuanza kuzalisha gonadotropin inatofautiana kati ya mtu na mtu wengine muda mfupi na wengine muda mrefu kwani mwili umekua tegemezi kwa hizo hormone zilizomo kwenye dawa kuliko zile unazozalisha wenyewe.
HIVO BASI DAWA HIZI HAZIACHI SUMU BALI ZINAVURUGA JINSI MFUMO WA HORMONE UNAVORATIBU MZUNGUKO WA HEDHI
No comments