TATIZO LA MENO KUOZA NA KUTOBOKA


Utangulizi
Mashino kwenye jino husababishwa na kutoboka kwa sehemu ngumu ya jino, mashimo hayo yanaweza kusababishwa na  mkusanyiko wa mambo mablimbali. Meno kuoza na kutoboka hutegemeana, yaani meno yakioza hupelekea kuwa rahisi kutoboka. Tatizo la meno kuwa na mashimo au kuoza husababishwa na kushambuliwa na bakteria waliopo ndani ya kinywa, kula vyakula vyenye sukari kwa wingi, na kutosafisha meno yako vema
Tatizo la meno kutoboka linajulikana duniani kote na hutokea sana kwa watoto, vijana wadogo na wazee. Hata hivyo ifahamike kwamba kila mtu anaweza kuoza meno na kutoboka ikiwa ni kichanga au mtu mzima.
Endapo tatizo la meno kuoza na kutoboka halijatibiwa  mapema, matobo hayo huweza kwenda chini mpaka kufika kwenye mzizi wa jino na kuanza kuleta Matatizo ya meno kuuma na jino kulegea na kutoka.
Dalili za meno kuoza
  • Kupata maumivu ya jino bila kuwa na sababu ya msingi
  • Jino kuwa na hisia sana, mfano kuuma dhidi ya kula vitu aina kadhaa
  • Kupata maumivu makali unapokula kitu cha baridi, moto au chenye sukari
  • Meno kubadilika rangi, rangi ya ugoro, kuwa na michirizi mweupe
  • Kupata maumivu wakati wa kung’ata meno
Visababishi
Meno kuoza husababisha matobo kwenye meno, tukio hili si la ghafla bali hutumia muda kutokea, baadhi ya maelezo ya namna ya Matatizo ya meno kuoza yanavyotokea yameelezewa hapa chini;
Kula vyakula vyenye sukari  na wanga kwa wingi
Vyakula hivi husababisha kufanyika kwa kuta nje ya jino ambayo kuta hii huliwa na bakteria, jinsi bakteria wanavyovamia kuta hii na kuila hupelekea kutengenezwa kwa kuta ingine ngumu ambayo haiwezekani kutolewa na bakteria

Kuta iliyotengenezwa kuvamiwa
Kuta ngumu iliyotengenezwa hapo juu huwa na asili ya u tindikali(asid) hivyo huvamia mfupa wa jino nan a kuuozesha na kusababisha vitobo. Vitobo vinapofanyika, asidi hupita na kuingia kwenye vitobo hivyo na kusababisha vitobo viendelee chini zaidi kwenye mzizi wa jino ambako kuna mishipa ya fahamu na damu. Mtu kwa hatua hii huwa anapat amaumivumakali ya jino.

Uvamizi kuendelea
Endapo mtu asipopata matibabu mapambano dhidi ya bakteria na kuta zilizofanyika huendelea, asidi huendelea kuharibu mzizi wa jino na kuleta maumivu zaidi, matokeo yake huweza kusambaa hadi kwenye mfupa unaoshikilia jino na kufanya uharibifu huko

Vihatarishi
Kila mtu mwenye meno ana hatari ya kuoza na kutoboka kwa meno, vitu vifuatavyo huongeza hatari ya meno kutoboka

Sehemu jina lilipo
Meno ya nyuma ya kinywa huwa hatarini sana kutoboka, meno haya huwa na mabonde, mashimo na milima mingi sana ambayo huweza kukusanya mabaki ya chakula. Kuwepo nyuma na sifa zilizotaja hufanya meno haya kuwa hatarini kutosafishwa vema na hivyo kuoza kirahisi

Vyakula aina fulani na vinywaji
Vyakula vinavyokaa mda mrefu kwenye kinywa kama maziwa, ice cream, asali, soda, matunda ya kukaushwa, keki, pipi vyakula vya mbegu na chipsi husababisha sana meno kuoza kuliko vyakula vingine ambavyo havinati kwenye meno.

Kula mara kwa mara
Kama unakula vyakula vyenye sukari aua vinywaji mara kwa mara, unawapa bakteria muda mwingi wa kuozesha sukari na wanga kuwa tindikali na hivyo kula mifupa ya jino. Kunywa soda na vyakula vingine vyenye tindikali huendelea kuharibu meno kwa njia hii.
Kuwalisha watoto wakati wa kula

Kutopiga mswaki vya kutosha
Kutopiga mswaki kwa dawa haswa wakati umemaliza kula ni kihatarishi kikubwa cha kuoza na kutoboka kwa meno

Kiungulia
Watu wenye ugonjwa wa kiungulia huwa hatarini kwa meno kuoza na kutoboka kwani asidi kutoka tumboni hucheuliwa kwenye meno. Asidi hii huunguza kuta za meno na kuzifanya ziwe dhaifu na kutoboka
Kutokuwepo kwa madini ya fluoride kwenye dawa za meno
Madini ya fluoride huwa asilia kwenye maji na huwa na kazi ya kuzuia meno kutoboka na kuyafanya yawe imara. Hata hivyo fluoride ikizidi kwenye maji huweza kusababisha meno kubadilika rangi na kuoza kirahisi

Matatizo ya kula
Kutapika, kula sana, husababisha meno kutoboka, kula sana husababisha Matatizo ya kutozaliwa kwa mate pia. Kutapika sana husababisha tindikaliya tumboni kuunguza meno.
Umri mdogo na umri mkubwa zaidi
Meno kuoza na kutoboka hutokea sana kwa watoto wadogo na wazee. Watoto wadogo hupata kutokana na vyakula wanavyokula na kutofanyia usafi wa meno, kwa wazee wengi ambao wanatumia dawa ambazo zinazuia kuzalishwa kwa mate huwa na kihatarishi cha kuoza na kutooboka kwa meno

Mdomo kukauka
Midomo kukauka husabaishwa na kutokuwepo kwa mate kinywani, mate hukinga meno kuoza na kutoboka, mate huwa na kemikali asilia ambazo huyeyusha tindikali kwenye kinywa inayofanya na bakteria. Madwa yanayosababishwa kinywa kukauka humweka mtu hatarini kuoza meno na kutoboka

Kuziba meno
Kuziba meno kwa watu wenye Matatizo ya meno kutoboka husababisha Matatizo zaidi, sehemu meno yalipozibwa huwa na sakafu ambayo huwani rahisi kufanyika kwa kuta ambazo huvutia bakteria kuzila na kutengeneza asidi kwa wingi hatimaye kutoboa jino zaidi.
Madhara
Madhara mengi yanayoweza kujitokeza ni kama vile
  • Maumivu ya meno
  • Usaha kwenye meno
  • Kuvimba kwa fizi
  • Kuvunjika na kuharibika kwa meno
  • Matatizo ya kushindwa kutafuna
  • Kucheza kwa meno na kung’oka
Kama mashimo yakiendelea kwa muda mrefu Matatizo yanayoweza kutokea ni pamoja na
  • Maumivu makali yanayoharibu ubora wa maisha ya mtu
  • Kupoteza uzito kutokana na kushindwa kula
  • Kung’oka kwa meno
  • Kufanyika kwa usaha kwenye mzizi wa meno

Kujikinga

  • Osha meno yako na dawa ya meno yenye madini ya fluoride, angalau mara mbili kwa siku, au kila baad aya kula chakula
  • Suuza mdomo wako kwa maji yenye fluoride(yanawezaekana yakawa maji maalumu)
  • Mwone daktari mara kwa mara kwa uchunguzi endapo una Matatizo ya meno
  • Ziba meno yaliyo mazima kujikinga na meno kutoboka haswa kwa watoto walio kwenye umri wa kwenda shule
  • Kunywa maji ya bomba- maji haya huwa na fluoride ambayo hulinda meno
  • Usile mara kwa mara vyakula vyenye sukari kwa wingi na vinywaji vyenye sukari
  • Pata matibabu ya mara kwa mara ya madini ya fluoride kutoka kwa daktari wako ili kujikinga na kmeno kutoboka
  • Tumia dawa za kuua bakteria endapo una maambukizi kwenye meno
  • Tumia dawa asilia ambazo zinasemekana kuponya meno na kuzuia yasitoboke. Kumbuka unabidi utumia dawa zilizothibitishwa na kuwa hazina madhara.

No comments