Virusi vya corona ni familia kubwa ya virusi inayosababisha binadamu kuugua, mtu anaweza kupata dalili za kali na kutokwa mafua au kuwa na dalili kali Zaidi za mfumo wa upumuaji na dalili kali za ghafla kwenye mfumo wa upumuaji.
Aina ya virusi vya corona kwa binadamu.
Virusi vya corona vipo duniani kote, kuna aina saba (7) ya virusi ambavyo wanasayansi wanavifahamu kuwa vina athiri binadamu na kuwafanya waugue.
Baadhi ya virusi hawa waligunduliwa zamani sana na wengine wamegunduliwa hivi karibuni. Virussi vya corona kwa wanaweza sababisha homa kiasi au homa kali sana.
Wapo Virusi wawili waliojulikana hivi karibuni kusababisha binadamu kuugua mara kwa mara ambaao ni kirusi aina ya SARS-CoV na kirusi cha MERS-CoV
Virusi aina nyingine ni pamoja na;
- 229E(alpha)
- NL63(alpha)
- OC43(beta)
- HKU1(beta)
- 2019 nCoV
Watu wengi duniani wanaathiriwa na kirusi cha 229E(alpha), NL63(alpha), OC43(beta) na HKU1(beta)
Kirusi cha corona anaweza kubadilika asili yake mara anapoingia kwa binadamu na kuwa kirusi mpya mfano wa virusi wapya ni virusi aina tatu vilivyogunduliwa hivi karibuni ni SARS-CoV, MERS-CoV na 2019 nCoV.
Kirusi cha corona pia huweza safari kati ya binadamu na Wanyama mfano popo, paka, ngamia n.k. Jamii fulani ya virusi hawa wanaonekana kuambukizwa kutoka kwa Wanyama mfano kirusi cha SARS-CoV kimeonekana kuambukizwa kati ya paka na binadamu na cha MERS-CoV kati ya ngamia na binadamu.
JINSI GANI UGONJWA HUU UNAENEA.
Ugonjwa huu unaenea kwa
1. njia ya hewa pale mtu mwenye virusi hivi anapokohoa au kupiga chafya,
2.kugusana na kugusa majimaji ya mwili hasa majimaji yanayotoka puani au kamasi kutoka kwa mtu mwenye ugonjwa huu.pia kugusa kitambaa au nguo zilizotumiwa na mtu mwenye virusi vya corona.
Dalili za ugonjwa huu ni;
- Homa
- mafua makali
- Kikohozi
- kuumwa kichwa
- vidonda vya koo
- Kuishiwa pumzi
- kubanwa mbavu na kupumua kwa shida
- mwili kuchoka sana
- maumivu ya misuli
Dalili kali huwa pamoja na dalili za nimonia, dalili za figo kufeli kufanya kazi, mkusanyiko wa dalili za kuathirika kwa mfumo wa upumuaji
Mambo ya kufanya yaliyoshauriwa na CDC pamoja na shirika la Afya Duniani WHO ili kuzuia maambukizi ni pamoja na
- Nawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji, au kutumia sanitiza
- Funika midomo na pua kwa kutumia kiwiko cha mkono unapopiga chafya au kukohoa
- Kuacha kugusa macho, pua na mdomo endapo mikono yako si safi
- Acha kutumia vyombo, miwani, kitanda vifaa vingine pamoja na mtu anayeumwa kirusi huyu au kama wewe ni mgonjwa
- Kutokaa karibu na mtu ambaye ana dalili za kuumwa kifua kama vile kukohoa na kupiga chafya
- Kusafisha maeneo unayoshika mara kwa mara kwa kutumia dawa za kuua na kuondoa vimelea vya maradhi.
- Kukaa nyumbani ukitoka kazini, acha kukaa kwenye mazingira ya watu wengi endapo wewe ni mgonjwa ili kuzuia maambukizi kwao
- Kupika vema mayai na nyama
Mambo ya kufahamu pia
- Jinsi unavyoshika vitu mbalimbali unakusanya vimelea vya kutosha kwenye mikono yako na unaweza kujiambukiza na vimelea hivyo endapo utashika pua, macho au mdomo.
- Kutumia sabuni kunawa mikono na maji kwa sekunde 20 au kutumia sanitiza huondoa vimelea kwenye mikono yako.
UNAPOONA DALILI ZA UGONJWA HUU TOA TAARIFA KUPITIA NAMBA 0800110124
Rejea
- About coronavirus 2019 (COVID-2019). U.S. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-ncov/about/index.html. Imetembelewa machi 4, 2020.
- Coronavirus disease (COVID-19) outbreak. World Health Organization. https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019. Imetembelewa Feb. 1, 2020.
- AskMayoExpert. Upper respiratory tract infection. Mayo Clinic; 2020.
No comments