JE KULA NANASI NA PAPAI WAKATI WA UJAUZITO KUNA MADHARA?


Si kweli.
Kuna uvumi kwamba unapokula nanasi au juice yake inasababisha mimba kutoka au kujifungua kabla ya muda wa kujifungua kufika.

Ni uvumi tu. Ndani ya nanasi kuna Bromelain. Na vidonge vya bromelain sio salama kutumika wakati wa ujauzito kwani vinapelekea mimba kuharibika. Ila kiwango kilochomo kwenye nanasi ni kidogo sana. Ili ufikie kiwango cha kidonge kimoja cha bromelain unahitaji kula nanasi 10 kwa wakati mmoja,unaweza ona ni kiasi kidogo cha bromelain kilichopo kwenye nanasi. Hivyo kula nanasi haina tatizo kwa mjamzito ila ina faida kwani ina kiwango kikubwa cha Iron na folate ambayo ni muhimu kuongeza damu. Pia ina vitamin C, Manganesse, na vitamin B6 ambavyo.ni muhimu kwa mama mjamzito



Kuhusu papai

Papai likiwa bichi au halijaiva vzuri linakua na kitu kinaitwa latex ambacho kinaweza kusababisha mji wa mimba ( uterus) kusinyaa na kupelekea kuharibika kwa mimba.ila lililoiva halina hiki kitu na ni safe kutumia wakati wa ujauzito. Na viazi vitamu havina shida

Download Dr.Joh android app kuendelea kujifunza zaidi maswala mbali mbali ya afya.ingia playstore search DOCTOR JOH kisha install. Au bofya link hii kudownload

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.doctor.joh

No comments