Maendeleo ya ukuaji wa mtoto-Mtoto wa mwaka 1 hadi 2

Ukuaji wa mtoto huhusisha ukuaji wa uwezo wa kufanya kitu fulani ipasavyo, mfano kuanza kutambaa au kutembea kwa mara ya kwanza, kupunga mkono wa bye bye, kusema maneno na kuongea, anavyocheza, tabia yake, anavyoruka na kushirikiana na wenzake.
Mwaka wa pili wa maisha, mtoto huanza kujitambua na kutembea kwenda huku na kule kwa kuwa na shauku ya kujua mambo na vitu vinavyomzunguka. Kwenye kipindi hiki mtoto anakuwa na tabia kuwa mbishi na asiyesikia mtu, kujitambua kwenye picha na kioo pia kuiga tabia za watu wengine wakubwa au watoto waliomzidi umri. Watoto wakati huu wanatakiwa pia kuweza kutambua majina ya vitu na wanafamilia anaoishi nao. Mtoto huweza kuongea sentesi fupi, kufuata maelekezo na miongozo wanayopewa. Mfano anaweza kuleta kitu kilicho ndani ya kabati mara baada ya kuambiwa niletee kitu fulani kipo ndani ya kabati

Mambo muhimu ya kukumbuka kuyafanya na yatamsaidia mtoto wako
  • Msomee mtoto vitabu vinavyoendana na mtoto
  • Mwombe akutafutie kitu, au aseme majina ya sehemu ya mwili wako, mfano muoneshe mkono na aseme huo ni nini
  • Cheza michezo ya kutumia vifaa, mfano kupanga vitu vya watoto, kujenga nyumba ya kuunganisha vidude vya kujengea nyumba vya watoto, au kuunga puzzles n.k
  • Mwache acheze na kutambua mazingira yake vizuri na kujua mambo mapya
  • Msaidie mtoto kusema vema maneno ambayo hajui mfano akisema baba na akawa anaonyeshea chupa, mwambie ndio hii inaitwa chupa.
  • Mkuze kwa kujitegemea mfano kumsaidia anapovaa aingize mguu mwenyewe na mikono kwenye shati
  • Onya makosa ya kwa mtoto na kumwambia kwanini asifanye zaidi ya kumpa adhabu.mwambie anatakiwa kufanya nini mbadala
  • Mpeleke mtoto aka talii sehemu za wanyama  au hata kutembea tu ili aweze kujua mazingira mapya na vitu vipya

Vitu vya kufanya ili kuhakikisha usalama wa mtoto
  • Usimwache mtoto karibu na majibila mtu kuwepo anayemwangalia wakati mtoto yupo kwenye maji. Hii inahusisha beseni au ndoo au bwawa la maji
  • Funga ngazi na mlango au kitu ili asipande maana anaweza Kupanda na kuanguka. Usimwache mtoto pia asiende maeneo ya matengenezo ya gari.
  • Weka vifaa vya moto mbali na mtoto, mfano pasi, hita ya maji n.k
  • Weka vitu vyenye ncha kali mbali na watoto ikiwa ni kisu, kiwembe au sindano na vitu vinavyoweza kumkata mtoto
  • Fungia dawa zote kabatini au weka sehemu ambayo mtoto hawezi kuzifikia kirahisi
  • Usimwache mwanao pekeyake kwenye gari hata kwa muda kidogo
  • Weka silaha zingine mbali nao ikiwa ni kisu, bunduki au bastola

No comments