Leo katika makala hii tutaangalia ni jinsi gani Caffeine inaweza kuathiri uwezo wa mwanamke kushika mimba na kwa mwanaume inaweza kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.
Tafiti zinaonesha kuwa kunywa Caffeine zaidi ya Milli gram 300 (sawa na kikombe kimoja cha kahawa) inaweza kupelekea matatizo kwenye uzazi.
Kwa wanawake caffeine inaathirir jinsi misuli laini ya mirija ya uzazi inavyotanuka na kusinyaa ili yai lijongee hivyo kuathiri jinsi gani yai linasafiri baada ya kuachiliwa kutoka kwenye mfuko wa mayai.Pia inaathiri kujongea kwa mbegu za kiume ili zilifike yai.
Kwa wanaume tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya caffeine zaidi ya milli gramu 300 kwa siku inaweza kupelekea tatizo la mbegu chache (low sperm count) kwani caffeine inaathiri uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Ni muhimu kwa wanandoa wanaotafuta watoto kuepuka matumizi ya bidhaa zenye kahawa ili kuepuka kuathiri uwezo wao wa kupata watoto.
KIASI CHA CAFFEINE KILICHOMO KWENYE VINYWAJI
Tumeona kwa kikombe kimoja cha kahawa kinakua na Caffeine katika kiwango cha Milligramu 300. Je vipi kuhusu soda na vinywaji vingine?
Hivi ni vinywaji vyeme caffeine na kiwango chake
CHAI:
- Chai ya kawaida (kikombe kimoja) = 14 to 70 mg
- Instant tea (kikombe kimoja) = 11 to 47 mg
Vinywaji baridi:
- Coke (chupa moja) = 35 to 47 mg na bidhaa nyingine zenye cola vina kiwango hiki.
- Pepsi (chupa moja) = 36 to 38 mg
- Mountain Dew, regular (chupa moja) = 54 mg
- sprite (chupa moja)= 38mg
- Mountain Dew MDX (chupa moja) = 71 mg
- cola (12 oz.) = 72 mg
- Pepsi diet =34.4mg
- cocacola diet=34.4mg
energy drinks:
- Azam energy drink(chupa moja.) = 215 mg
- Switch(chupa moja) = 160 mg
- Red Bull (chupa moja.) = 80 mg
- shark (chupa moja) = 300 mg
cocoa, chocolate, na ice creams:
- Cocoa kijiko kimoja = 2 to 13 mg
- Milk chocolate (1.55 oz.) = 9 mg
- Dark Chocolate (1.45 oz.) = 31 mg
- Coffee Ice Cream (8 oz.) = 68 to 84 mg
- chocolate Ice Cream (8 oz.) = 68 to 84 mg


No comments