Preeclampsia
Au Shinikizo La Damu linaloelekea kusababisha kifafa cha mimba ni
tatizo linaloletwa na ujauzito na lina ambatana na shinikizo la juu la
damu na dalili za kudhulika kwa vioungo ndani ya mwili, mara nyingi huwa
figo.
Preeclampsia huanza kuonekana kuanzia wiki ya ishirini ya ujauzito kwa mwanamke ambaye shinikizo lake la damu lilikuwa kawaida.
Kuongezeka
kidogo kwa shinikizo la damu huwa ni dalili mojawapo ya shinikizo la
damu linaloelekea kusababisha kifafa cha mimba, pasipo matibabu pre
eclampsia huweza kuleta madhara makubwa kwa mama hata kuondoa uhai wa
mama au mtoto.
Kama ukipata pre eclampsia dawa ya kutibu kabisa tatizo hilo ni kujifungua.
Kama
ukigundulika mapema zaidi katika kipindi cha ujauzito una tatizo hili
la preeclampsia, wewe na dakitari mtapata utata kuhusu kitu cha kufanya
kwa sababu mtoto huwa hajakomaa na kuwa tayari kuishi nje ya tumbo la
mama na hivyo huhitaji mda ili kuweza kukomaa , lakini wewe huhitaji
kujiweka hatarini kwenye usalama wa maisha yako na mtoto.
Dalili za preeclampsia
Mara
nyingine ugonjwa huu unaweza usionekane kwa dalili . Shinikizo la damu
la juu linaweza likaongezeka polepole, lakini mara nyingi huanza ghafla
kwa watu wenye tatizo hili la preeclampsia. Kupima shinikizo la damu na
kudhibiti ongezeko huwa sehemu ya matibabu ya kuzuia matokeo mabaya ya
tatizo hili kwa sababu dalili ya kwanza mara nyingi huwa ni ongezeka la
shinikizo la damu.
Shinikizo
la damu la 140/90 mmHg au zaidi, lililopimwa kwa vipimo viwili wakati
tofauti kwa wastani wa masaa 4 kupita kila baada ya kipimo, huwa ni
shinikizo la juu.
Dalili zingine za shinikizo la damu linaloelekea kuwa kifafa cha mimba ni
-
Kiwango kikubwa cha protini kwenye mkojo au dalili za uhalibifu wa figo kama kupungua kwa mkojo ama mkojo kuwa na rangi tofauti
-
Maumivu makali ya kichwa
-
Kubadilika kwa hali ya kuona kama kutoona kabisa au kuona ukungu au kuumizwa na mwanga
-
Maumivu ya juu ya kitovu, mara nyingi upande wa kulia kwenye mbavu
-
Maumivu ya chembe ya moyo
-
Kichefuchefu na kutapika
-
Kupungua kwa kiwango cha mkojo
-
Kupungua kiwango cha chembe mgandisho za damu(chembechembe zinazogandisha damu)
-
Kushindwa kufanya kazi kwa ini
-
Kuishiwa pumzi, kunasababishwa na maji kujaa kwenye mapafu
Kuongezeka
uzito ghafla na kuvimba sana kwenye maeneo ya uso na mikono maranyingi
huambatana na preeclampsia lakini dalili hii huonekana kwenye magonjwa
mengi na wakati mwingi huwa kawaida kwenye ujauzito hivo huwa sio
dalili ya kutegemea sana kwa mgonjwa ili kusema ana preeclampsia
Nini husababisha preeclampsia
Sababu
halisi inayopelekea kusababisha tatizo hili bado haijulikani. Wataalamu
wa afya wanaamini kwamba tatizo hili huanzia kwenye kondo la nyuma
ambalo hutumika kumlisha mtoto kipindi chote cha ujauzito.
Mwanzoni
kabisa mwa ujauzito, mishipa mipya ya damu hutengenezwa na kuingiza
damu kwenye kodo la nyuma, wanawake wenye tatizo la preeclamsia mishipa
hii huwa haitengenezwi vyema. Mishipa huwa myembamba kuliko kwaida na
huwa na tabia tofauti inapokutana na vichochezi mwili ambapo husababisha
mishipa hii kuruhusu kiwango kidogo cha damu kupita ndani yake na
kuingia kwenye mji wa mimba
Sababu zinazosabaisha kufanyika vibaya kwa mishipa hii huwa ni
-
Kiwango kidogo cha damu kinachofika katika tumbo la uzazi
-
Kuharibiwa kwa mishipa ya damu
-
Tatizo la mfumo wa kinga za mwili kupambana na mwili
-
kuwa na vinasaba vinavyoambatana na ugonjwa huu
Matatizo mengine ya shinikizo la damu
Preeclampsia huwa moja miongoni mwa magonjwa manne yanayoambatana na matatizo ya shinikizo la damu. Magonjwa mengine ni kama
Shinikizo la damu linaloanza wakati wa ujauzito
Wanawake
wenye shinikizo la damu la juu wakati wa ujauzito wanakuwa na shinikizo
hilo pasipo kuwa na protini kwenye mkojo kama wakipimwa mkojo wao, pia
huwa hawana dalili za kuharibika kwa organi mojawapo mwilini.
Baadhi ya wanawake wenye shinikizo la damu la juu wakati wa ujauzito huweza kupata preeclampsia.
Shinikizo la damu sugu
Shinikizo
la damu sugu ni lile mwanamke anakua nalo kabla ya kupata ujauzito au
linalogunduliwa kabla ya wiki ya 20 ya ujauzito na liaendelea baada ya
mama kujifungua mtoto.
Kwa
sababu shinikizo la damu huwa halina dalili wakati mwingine huwa vigumu
kutambua kwamba limeanza lini kwa mama kama asipofanya vipimo
Shinikizo la damu sugu linaloambatana kuelekea kuwa preeclampsia
Shinikizo
hili hutokea kwa wanawake wenye tatizo sugu la shinikizo la damu la juu
ambao shinikizo hilo hubadilika kuwa baya zaidi na kuonekana kwa
protini kwenye mkojo baada ya kipimo au matatizo mengine ya kiafya
wakati wa ujauzito
Vihatarishi
Preeclampsia hutokea kama matokeo/madhara ya ujauzito.
Vihatarishi ni kama;
-
Historia ya preeclampsia-kuwa na historia kwa mama au ndugu wa tumbo moja huongeza hatari ya kupata tatizo hili kwa kiasi kikubwa
-
Ujauzito wa kwanza- hatari ya kupata tatizo hili huongezeka kwenye ujauzito wa kwanza
-
Mpenzi mpya- kila ujauzito unapokuwa na baba mpya huongeza hatari ya kupata tatizo hili la preeclampsia ukilinganisha na mwanamke anayepata ujauzito kwa mwanaume yuleyule
-
Umri- hatari ya kupata tatizo hili huongezeka kwa wanawake wanaopata mimba kwenye umri wa zaidi ya miaka 40 au chini ya miaka 15
-
Kitumbo-kuwa na kitumbo au uzito kupita kiasi huonekana kuhusiana na tatizo hili
-
Mapacha-kuwa na mapacha au watoto wengi zaidi kwenye ujauzito mmoja huongeza hatari ya kupata preeclampsia
-
Muda kati ya ujauzito mmoja na mwingine- kuwa na mtoto chini ya miaka miwili au zaidi ya miaka kumi baada ya ujauzito uliopita huongeza hatari ya kupata tatizo hili la preeclampsia
-
Magonjwa mengine-kuwa na tatizo sugu la shinikizo la damu la juu kabla ya ujauzito, kipanda uso, kisukari aina ya 1 na 2, magonjwa ya figo, tatizo la damu kuganda, au ugonjwa wa lupus huongeza hatari ya kupata preeclampsia
Madhara ya preeclampsia
Tatizo
la preeclampsia linapoonyesha dalili mbaya mapema hutishia maisha
ya mtoto na mama. Mama mwenye Preeclampsia anaweza akahitaji kuanzishiwa
uchungu kwa ajiri ya kujifungua . Mama anaweza kujifungua kwa upasuaji
endapo matatizo mengine yametokea kama mtoto kutanguliza makalio, au
matatizo mengine.
Kama una preeclampsia kali au ujauzito wako unawiki chini ya 30 unawe kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mtoto
Madhara ya preeclampsia ni;
Kukosekana
damu inayoenda kwenye kondo la nyuma-pre eclampsia hudhuru mishipa
inayopeleka damu kwenye kondo la nyuma(placenta) na kama lisipopata damu
ya kutosha mtoto atapata damu kidogo na kiwango kidogo cha chakula na
hivyo hukua taratibu, kuwa na uzito kidogo au kujifungua kabla ya
wakati, mtoto kupata matatizo ya mfumo wa upumuaji.
Kunyofoka
kwa kondo la nyuma- kondo la nyuma linaponyofoka kutoka kwenye ukuta wa
uzazi husababisha kuvia kwa damu ndani ya kizazi na kufa wa mtoto
tumboni. Kiwango cha damu kikipotea kwa wingi mama huwa hatarini
kuishiwa na damu na kifo .
Kupata
dalili za HELLP syndrome. Dalili hii huambatana na kuvunjwa vunjwa kwa
chembe nyekundu za damu mwilini, kuongezeka kwa kemikali Ini
zinazoashiria uharibifu kwenye Ini, kiwango kidogo cha chembe za
kugandisha damu. Dalili hizi zinapotokea huweza kusababisha majanga kwa
mama na mtoto puia- dalili zake huwa ni
-
kichefuchefu na kutapika,
-
maumivu ya kichwa,
-
na maumivu upande wa juu wa kulia ya tumbo amabapo ini limekaa.
HELLP
huwa hatari kwa sababu huonyesha uharibifu mkubwa wa organi mbalimbali
mwilini na huweza kutokea ghafla hata kabla ya kutokea kwa shinikizo la
damu la juu.
Kifafa
cha mimba- kama preeclampsia ikidhibitiwa vyema kifafa cha mimba au
eclampsia huwa hakitokei, kifafa cha mimba huambatana na dalili za
kutetemeka mwili.
-
Dalili za mama anayeelekea kupata kifafa cha mimba ni kama maumivu upande wa kulia juu ya tumbo,
-
maumivu makali ya kichwa,
-
tatizo la kuona,
-
na kubadilika kwa
Ugonjwa
wa moyo- kuwa na preeclampsia kunaongeza hatari ya kupata ugonjwa wa
moyo na mishipa ya damu, hatari ya kupata ugonjwa huu huongezeka zaidi
kama umeshawahi kupata preeclampsia mara mbili au umewahi kujifungua
mtoto kabla ya kutimiza umri. Kuzuia kupata ugonjwa huu, mara baada ya
kujifungua jaribu kuwa na uzito kiasi, kula mbogamboga za majani na
matunda fanya mazoezi kwa kufuata ratiba na pia usivute sigara.
Vipimo
Ili
Kuweza kutambua kwamba una preeclampsia, unatakiwa uwe na shinikizo la
damu la juu na moja au zaidi kati ya viashiria vifuatavyo;
-
Protini kwenye kipimo cha mkojo
-
Kiwango kidogo cha chembe vigandishi damu kwenye kipimo cha damu
-
Kushindwa kufanya kazi kwa ini
-
Dalili za tatizo kwenye figo mbali na kuwa na protini kwenye mkojo
-
Maji kwenye mapafu
-
Maumivu ya kichwa yanayoanza ghafla
-
Kupata matatizo ya kutoona
Kipindi
cha nyuma mtu aliambiwa na dakitari kwamba ana preeclampsia kama mama
alikuwa na shinikizo la damu la juu na protini kwenye mkojo tu. Ingawa
wataalamu waliobobea kutafiti tatizo hili wanafahamu kwamba mama anaweza
kuwa na preeclampsia bila kuwa na protini kwenye mkojo.
Shinikizo
la damu linalozidi 140/90 huwa sio la kawaida katika ujauzito, ingawa
kipimo kimoja cha shinikizo la damu kikiwa juu hakimaanishi kwamba una
preeclampsia. Kama dakitari akikupima na kugundua kwamba kipimo chako
hakipo kawaida na baadae akakupima baada ya masaa manne kupita na
akakuta shinikizo lako la damu bado lipo juu, dakitari anaweza kukuambia
una preeclampsia na baadae atafanya vipimo vingine kama cha damu na
mkojo.
Vipimo vinavyohitajika
Kama dakitari amekuhisi una preeclampsia, utafanya vipimo vingine kama
Kipimo
cha damu- kipimo hiki kitaonyesha jinsi gani chembe zako za damu za
mgandisho zipo kawaida au zimepungua na pia kitaonyesha ufanyaji kazi
wako wa ini na figo.
Kipimo
cha mkojo- kipimo hiki kinapima kiwango cha uwiano kati ya protini na
creatine kilichopo kwenye mkojo kila wakati . Mkojo hukusanywa kwa masaa
24 kutoka kwa mgonjwa kwa kuwekewa mpira wa mkojo, kipimo kikifanyika
kitaonyesha ukubwa wa tatizo la preeclampsia
Mionzi
sauti ya ujauzito-ultrasound. Dakitari atakuwa akifanya kipimo hiki
mara kwa mara ili kuangalia ukuaji wa mtoto. Kipimo hiki kinaweza kupima
uzito wa mtoto na kiwango cha maji kwenye mfuko wa uzazi
Kipimo cha kuangalia mapigo ya moyo ya mtoto yanavyobadilika kama mtoto akiwa anajicheza tumboni.
Matibabu na dawa
Tiba
pekee ya preeclampsia ni mimba kutolewa kwa maana nyingine kujifungua.
Unakuwa hatarini kupata kifafa cha mimba, kondo la nyuma kujiachisha
kutoka kuta za mfuko wa uzazi, kiharusi na kutokwa na damu kunakoweza
kusababisha kuwa na shinikizo la chini la damu endapo ujauzito utabaki.
Kama mimba ni changa sana basi itakuwa mapema kujifungua kichanga
ambacho hakijakamilika kutengenezwa na huwa si kitu kizuri.
Kama
ukigundulika una preeclampsia, dakitari wako atakufahamisha na
utatakiwa kuja mara kwa mara kitengo cha uzazi kwa ajili ya uchunguzi.
Utahitaji
pia vipimo vya damu ,mkojo na shinikizo la damu mara kwa mara unapokuja
clinic, utahitaji kipimo cha mionzi sauti na mapigo ya moyo ya mtoto
kuliko mama mwingine ambaye hana preeclampsia.
Madawa
Matibabu yanayoweza kutumika ni:
-
Dawa za kupunguza shinikizo la damu la juu .Zipo dawa aina nyingi na zingine si salama kutumia wakati wa ujauzito
-
Corticosteroids. kama mgonjwa ana HEELP syndrome dawa hii itatumika na huweza kusaidia kwa muda kazi za ini na chembe mgando za damu(chembe zinazogandisha damu). Dawa hii pia hufanya mapafu ya mtoto kufanya kazi kama ikipewa masaa ishirinina nne kabla ya kuanzisha uchungu wa uzazi kwa mama ambaye mtoto hajafikisha wiki 37 za ujauzito
-
Dawa za kifafa- kama ukiwa na preeclampsia kali daktari atakupa dawa kama magnesium sulphate ili kuzuia kutokea kwa kifafa.
Matibabu mengine ni kama
Pumzika
Kupumzika
kitandani hushauriwa sana kwa wanawake wenye kifafa cha mimb, lakini
utafiti haujaonyesha faida za tendo hili. Kupumzika kunaweza kuongeza
kuganda kwa damu na kushuka kwa kipato na kwa wanawake wengi kupumzika
kitandani hakushauriwi kwa sasa.
Kulazwa hospitali
Endapo
una preeclampsia hatari basi utalazwa hospitali na kupimwa mapigo ya
moyo na kiwango cha maji kwenye mfuko wa uzazi na kama maji ni kidogo
maana yake kiwango cha damu inayoingia kwenye kondo la nyuma na mtoto
ni kidogo
Chakula
Kama umekutwa na preeclampsia mwishoni mwa ujauzito dakitari anaweza kuamuru ujifungue mara moja
Kama
unapreeclampsia mbaya basi dakitari hataangalia kwamba mtoto anawiki
ngapi na ataamua kukuanzishia uchungu ili mtoto atoke tumboni kwa ajili
ya kuokoa maisha yako, kama haishauriwi kuachwa kwa muda basi upasuaji
utafanyika mara moja na wakti huu unaweza kupewa dawa za magnesium
sulphate kuzuia kifafa cha mimba kutokea
Baada
ya kujifungua, mategemeo ni shinikizo la damu litashuka na ndani ya
wiki 12 lakini huwa haraka sana kushuka hata kabla ya wiki hizo. Kama
unamaumivu na unahitaji dawa za maumivu baada ya kujifungua basi mulize
dakitari wako dawa gani zinafaa, dawa aina ya NSAIDs kama
ibuprofen,naproxen, huongeza shinikizo la damu. Dawa aina ya panadol
huwa salama kutumiwa.


No comments