Watu
wengi hudhani kama mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa
ni upande wa mwanamke, lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna
uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana
na ugumba upande wa mwanaume.
Mwanaume
kuzalisha mbegu chache kuliko kawaida ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa
wanaume.
MBEGU
CHACHE NI KIASI GANI?
Shahawa
kawaida ni mchanganyiko wa maji maji (ute) unaotengenezwa na tezi dume na mbegu
za kiume (manii). Mtu anakua na tatizo la mbegu chache pale katika kila
Millilita moja ya shahawa zake kunakua na mbegu (manii) chini ya millioni 15.
Kwa kawaida mwanaume anazalisha zaidi ya manii millioni 20 katika kila
millilita moja ya shahawa anazomwaga.
Kitaalamu
tatizo hili linaitwa OLIGOSPERMIA (ol-ih-go-spur-me-uh), na kutokuwa na mbegu
za kiume kabisa kwenye shahawa inajulikana kama AZOOSPERMIA
DALILI
Dalili
kuu ya tatizo hili ni kushindwa kutungisha mimba/kupata mtoto.Zinaweza kuwepo
dalili nyingine kulingana na chanzo cha tatizo hili mfano mirija ya manii
kuziba,matatizo kwenye korodani na matatizo kwenye mfumo wa hormone.
Dalili
nyingine ni kama
Matatizo
kwenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa mfano kukosa hamu ya kufanya tendo la
ndoa,uume kushindwa kusima au kuwa mlegevu unaposimama.
Maumivu
na uvimbe kwenye korodani
Kupungua
au kutokuwa na ndevu na nywele za sehemu nyingine za mwili ,hii ni dalili ya
uhaba au upungufu wa hormone ya testosterone.
VISABABISHI
VYA TATIZO HILI
Kutengenezwa
kwa mbegu inahusisha korodani na tezi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana kama
hypothalmus ambayo hii inahusika na kuzalisha hormone zinazochochea uzalishwaji
wa mbegu za kiume. Matatizo katika viungo hivi huweza kupelekea tatizo hili.
Pia
kuna weza kuwepo na matatizo katika maumbo ya mbegu za kiume nayo kupelekea
tatizo hili.
Visabibishi
vya tatizo hili ni kama ifatavyo:
SABABU ZA
KIAFYA
1.Kuvimba
kwa mishipa ya damu ya korodani-Varicocele ,hali hii inaathiri kiwango cha joto
kwenye korodani hivyo kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.
2.Maambukizi,
Baadhi ya maambukizi yanaweza kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume na jinsi
mbegu hizi zinavyotelewa nje.Magonjwa ya zinaa,magonjwa ya korordani yanaweza
kupelekea kuziba kwa mirija ya manii na kuharibu seli zinazohusika na
kutengeneza manii kwenye korodani.
3.Matatizo
katika kutoa mbegu nje mfano tatizo la misuli ya shingo ya kibofu kutobana
vizuri hivyo kupelekea shahawa kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya
kutolewa nje.
4.Kinga
ya mwili kuziharibu mbegu.Kuna tatizo la kinga ya mwili kuzisoma mbegu za kiume
kama wadudu wanaoleta magonjwa hivyo kuziharibu (sperm ant bodies)
5.Saratani,
kuna baadhi ya saratani kama saratani ya tezi ya pituitari,saratani ya korodani
zinaathiri pia utengenezwaji wa mbegu za kiume
6.USAWA
WA HOMONI USIO SAWA (Hormone Imbalance):
Tatizo la
homoni kutokuwa sawa si jambo linalowapata wanawake peke yao, ni jambo
linalojitokeza pia kwa wanaume ingawa wengi wao huwa hawana muda wa kufikiri
kuwa nalo. Homoni zina umhimu mkubwa katika kazi ya uzalishaji wa mbegu na
katika afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla.
Moja ya
homoni kuu inayohusika na uzazi kwa mwanaume ni homoni ya testosterone.
Kutokana na maisha yetu ya kisasa na baadhi ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu
upande wa uwingi wa mbegu, wanaume wengi wanajikuta katika hali hii ya kuwa na
tatizo la homoni zao kutokuwa katika usawa unaohitajika kwa afya bora ya uzazi.
Vipo vitu
vinavyoweza kuharibu homoni ya testerone na huanza kwa kuigiza au kijifanya
vyenyewe ni estrogens (xenohormones). Estrogen ikizidi katika mwili wa mwanaume
hupelekea uhanithi (uume kushindwa kusimama), kukosa hamu ya tendo la ndoa,
kupungua kwa mbegu na kupungua kwa maji maji ya mbegu kwa ujumla.
Visababishi
hasa vya kuharibika kwa testeroni ni pamoja na
• Vyakula
vyenye soya
• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani
• Homoni zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama
• Vifaa au vyombo vya plastiki aina ya HDPE.
• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani
• Homoni zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama
• Vifaa au vyombo vya plastiki aina ya HDPE.
7.Mishipa
ya manii kuziba
8.Madawa,
Baadhi ya madawa mfano dawa za kutibu saratani,dawa za fangasi,na baadhi ya ant
biotic zikitumika kwa muda mrefu zinaweza kusababisha tatizo hili.
9.
Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa
katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Stress
inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya
stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.
Vile vile
kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.
Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na
tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.
Kuwa na
amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.
SABABU ZA
KIMAZINGIRA
- kemikali za viwandani kama benzene,toluene,xylene,dawa za kuua wadudu,rangi za nyumba, zinaweza kupelekea tatizo hili
- Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume. Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta. Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.
- Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa
vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na
ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake
hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa
hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.
Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia. Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.
• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.
Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation). Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.
•
Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika
mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la
homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.
Kwenye
bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya
estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako. Vyote hivi vina madhara katika
afya ya mwanaume.
• Vyakula
vyenye soya –
Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya
soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume. Vinasemwa moja
kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya
uzazi wa mwanaume
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.
•
Matumizi ya vifaa vya plastiki – kuna baadhi ya vifaa vya plastiki vinapowekewa
chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza
kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa
uzazi wa mwanaume.
• Joto
kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo
ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya. Inasemekana kuwa hii
ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya
mwili wake.
Joto
linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka
mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya
uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.
•
Mfadhaiko (Stress) –
Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea
kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Stress
inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya
stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.
Vile vile
kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.
Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na
tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.
Kuwa na
amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.
• Aina ya
chakula unachokula – Chanzo
kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula
sahihi na cha kutosha kila siku. Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume
anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E,
folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu
mwilini (antioxidants).
- Uzito kupita kiasi
JINSI YA
KUJIKINGA
Njia
kubwa ya kujikinga na tatizo la mbegu chache ni kula vyakula vyenye
virutubisho vinavyosaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa mbegu za kiume.
Njia
nyingine ni pamoja na:
kuacha
kuvuta sigara
kutokunywa
pombe kupindukia
kutotumia
dawa za kulevya
kuepuka
msongo wa mawazo
kutovaa
nguo zinazobana sana korodani
kupunguza
uzito uliozidi
Epuka
kula vyakula vyenye Soya mfano mbegu za soya,maziwa ya soya
Wasiliana
na daktari wako kuhusu matumizi ya dawa zinazoathiri uzalishwaji wa mbegu hizi.


No comments