Katika
miaka ya hivi karibuni kutokana kuongezeka kwa watu wenye nyama uzembe
au kitumbo na kutafuta tiba dhidi ya uzito uliopita kiasi na nyama
uzembe, kupoteza uzito kwa njia ya kutakasa mwili kumewafanya watu wengi
kuweka macho kwenye njia hii kuwa ndo njia nzuri na njia moja maarufu
zaidi ya kupunguza uzito haraka.
Makala hii inakuambia namnaya kupunguza uzito kwa njia ya kutakasa na faida na madhara yake
Nini maana ya kupunguza uzito kwa njia ya kutakasa mwili?
Neno
kutakasa kama lilivyo na maana kwamba ni kusafisha, katika kupunguza
uzito humaanisha kusafisha mwili dhidi ya sumu mbalimbali zilizo ndani
ya mwili. Hakuna maana nzuri ya nini maana ya kutakasa mwili na nini
haswa vinapaswa kuwepo wakati wa kutakasa mwili.
Kwa
ujumla kutakasa mwili huhusisha njia ya kujizuia kula aina fulani ya
vyakula au kubadili maisha au kutumia dawa aina fulani za miti
shamba(dawa asilia)
Njia
hizi wengne hutumia ili kuondoa sumumwilini, na wengine hutumia kama
njia ya kupunguza uzito, ikiwa pamoja na kupunguza mafuta sehemu fulani
tu ya mwili mfano tumbo n.k
Baadhi
ya njia huhusisha kutumia dawa asilia au mazoezi, nyingine huhusisha
kutumia chakula aina fulani ambacho unakula kila siku.
Kuna utofauti kati ya kutakasa mwili na kutumia dawa za kuondoa sumu mwilini?
Ni
ngumu kutofautisha kati ya kutakasa mwili na kuondoa sumu mwilini kwa
kwa sababu njia zote hazina utofauti kati ya miongozo na nini haswa
kiwepo au kifanyike wakati wa kutakasa au kuondoa sumu mwilini. Hivyo
maneno haya siku zote yanatumika yakiwa na maana moja.
Kila aina ya njia ina malengo ya kutoa tiba yam da mfupi yaani chini ya mwezi mmoja au siku 30
Chakula cha kuondoa sumu
Vyakula
vya kuondoa sumu mwilini hufanya kazi kwa kanuni kwamba mwili huhitaji
msaada wa kuondoa sumu na kemikali hatari mwilini ambazo huzuia wewe
kufikia kiwango cha juu cha afya njema.
Sumu
hizi zinatuzunguka katika maisha ya kila siku na hupatikana kutokana na
maisha ya binadamu na shughuli wanazofanya; zikihusisha
-
Uchafuzi wahali ya hewa
-
Madini
-
Kemikali za viwandani
-
Dawa za kuua wadudu kwenye mimea au vyakula
-
Viasha mizio( allegen)
Chakula
cha kuondoa sumu kinaweza kuhusisha, kukuzuia kula aina fulani ya
vyakula na kufunga, dawa za asilia, dawa za kuamsha kuharisha, dawa za
kulegeza haja kubwa na kuacha kula vyakula aina fulani. Baadhi ya njia
huweza kuondoa sumu kwenye kiungo fulani tu cha mwili mfano figo, ini,
kibofu cha mkojo au utumbo
Kupungua uzito kunaweza kuwa moja ya malengo ambayo unaweza kuyafikia ili kuondoa uchafu na sumu kama vile
-
Viamsha mizio(allergen)
-
Maumivu ya kichwa na kipanda uso
-
Matatizo ya mmengenyo wa chakula
-
Kuchoka
-
Kichefuchefu
-
Chunusi
-
Harara kwenye ngozi
-
Kurekebisha homoni mwilini
Ingawa dawa za kuondoa sumu zimekuwa maarufu sana, hakuna ushahidi kuwa njia hizii zinafanaya kazi kwa ufanisi gani.
Kutakasa mwili siku zote kunasisitiza chakula
Baadhi
ya milo ya kutakasa mwili hufanya kazi kama dawa za kuondoa sumu
mwilini, huhusisha kukataza kula baadhi ya vyakula na kupata viinirishe
muhimu.
Kwa
ujumla hulenga kuondoa vyakula visivyo na umuhimu kiafya na vile vyenye
kuamshamizio na mdalala wake kutumia vyakula vyenye afya njema, vyakula
asilia na visivyo sindikwa
Kupoteza
uzito huwa nilengo mojawapo la kutaka samwili, lakini pia kutakasa
mwili hulenga kuondoa Matatizo mengi ya kula mfano kuondoa hamu ya kula
sana n.k
Vyakula ambavyo vinaondolewa kwenye ili kuutakasa mwili ni
-
Sukari
-
Vyakula vya kusindikwa
-
Pombe
-
Maziwa
-
Soya
-
Ngano
-
Mahindi
-
Vyakula vyenye gluten
Mifano ya njia mbalimbali za kutakasa mwili ni kama zilivyoorodheshwa hapo chini;
Utakaso wa kuacha baadhi ya vyakula
Siku
30 za kuacha kula vyakula kadhaa vya sukari, maziwa, mazao jamii ya
kunde, vyakula vitokanavyo na mbegu na pombe. Kipindi hiki utatumia
matunda kwa wingi, mboga za majani na nyama nyeupe.
Utakaso wa kutumia juisi
Huduma
kwa siku 3 hadi 7, utaacha kula vyakula aina zote, na kubakisha juisi
tu na maji. Kuna orodha maalumu ya juisi na mboga za majani unazotakiwa
kula kwa kipindi hicho
Utakaso wa limao
Utakaso wa limao huhusisha kutumia mchanganyiko wa limao na maji pilipili na Mchanganyiko maalumu wa uji w matunda.
Utakaso
wa siku 21 wa kutumia viinirishi mbadala na dawa za kulegeza utumbo na
matumbo. Huhusisha kusitisha kula vyakula vya maziwa na maziwa, nyama,
sukari na vyakula vya kusindikwa.
Je njia hizi zinafanya kazi kweli?
Hakuna
tafiti ya kisayansi iliyofanyika dhidi ya ubora wa aina fulani ya dawa
au tiba ya utakaso ambayo inafanya kazi, hivyo ubora na ufanisi wa aina
hii ya tiba bado hazifahamiki.
Hata
hivyo njia hizi humfanya mtu kutumia nishati kidogo mwilini na hivyo
humsababisha kupoteza uzito kwa kuwa anatumia vyakula vyenye nishati
kidogo sana.
Baadhi
ya tafiti zilizofanyika zinaonyesha kwamba kutumia vyakula vyenye
nishati kidogo sana kwa siku huwa na mchango mkubwa wa kupoteza uzito.
Je kuna madhara yoyote ya kiafya mtu anaweza kupata kutokana na tiba utakaso?
Ndio kuna madhara mtu anaweza kupata ikitegemea aina ya njia na hali ya afya ya mtu
Matatizo
mengi hutokea kwa watu endapo watapungua uzito haraka mfano, kupata
mawe kwenyekifuko cha nyongo, kuishiwa maji mwilini, kupungukiwa
viinirishimuhimu mwilini. Upungufu wa vitamin n.k
Kwa
watu wenye Matatizo ya figo baadhi ya tiba utakaso mfano ile ya kutumia
juisi ya mboga za majani kwa wingi inaweza kupelekea kuharibika kwa
figo zaidi kwa watu walio na tatizo la figo iliyoferi kwa mda mrefu.
Mambo ya msingi kufahamu
-
Njia hii ni nzuri kwa kupoteza uzito kwa mda mfupi
-
Ni njia ambayo haina utafiti mwingi wa kisayansi uliofanyika kuhusu kila aina ya njia ya utakaso
-
Ni muhimu kuwa na mtaalamu wa afya mwenye ujuzi na njia hizi akusimamie ili aweze kukukinga na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa kukupa ushauri nini cha kufanya
UNAHITAJI KUPUNGUA UZITO?
JIPATIE KITABU CHA MUONGOZO WA KUPUNGUA UZITO KWA GHARAMA NAFUU.
WASILIANA NASI KUPITIA NAMBA 0762167811.
UNAWEZA KUANGALIA SAMPLE YA KITABU CHETU NA KUONA KIMESHEHENI MAMBO GANI KWA KUBOFYA LINK HII.
No comments