Ili mtu aseme ana tatizo hili ni pale anapokosa period au
anapata mzunguko usioeleweka baada kipindi cha miezi 6 tokea aache kutumia dawa
za uzazi wa mpango.
Kwa kitaalamu hali hii inaitwa post pill amenorrhea.
Tafiti zinaonesha kuwa kati ya wanawake wanaotumia dawa za
uzazi wa mpango aslimia 2 hadi 3% wanapata hali hii.
TATIZO HILI HUTOKEAJE.
hii inatokana na kuathiriwa kwa utendaji kwazi wa tezi ya
pituitari na dawa za uzazi wa mpango.
Katika mzunguko wa kawaida tezi ya pituitari huzalisha
hormone chochezi ya mayai (follicle stimulating hormone) na hormone ya lutea
(lutenizing hormone) ambazo hizi zinachochea kupevuka kwa mayai kwenye mfuko wa
mayai (ovari).
Mayai yaliyokomaa huzalisha hormone ya estrogen. Pia hormone
ya progesterone huzalishwa baada ya yai
lililopevuka kuachiliwa kutoka kwenye ovari. Kazi ya hormone hizi ni kuandaa
mji wa mimba kulokea yai likirutubishwa na kutunza ujauzito. Kusipokuwa na
kurutubishwa kwa yai ule utando ulioandaliwa hutoka kama damu ya hedhi.
Dawa za uzazi wa mpango zinakuwa na hormone za estrogen na
progesterone.hivyo mwanamke anapotumia dawa za uzazi wa mpango zenye hormone
hizi kiwango cha hormone hizi kwenye damu kinaongezeka na kufanya mwili kuhisi
kuna kiwango cha kutosha cha hormone hizi hivyo kufanya tezi ya pituitari
kuacha kuzalisha hormone chochezi ya mayai na hormone ya lutea.
Na kama tunavyojua yai haliwezi kupevuka kusipokuwa na
hormone ya lutea na hormone chochezi ya mayai.
Mwanamke anapoacha kutumia dawa hizi inaweza kuchukua muda
kwake kuanza kupevusha mayai na kupata siku zake kama kawaida.
Saa nyingi hali inaweza kuwa mtu anapata damu kidogo sana ya
hedhi au mzunguko usioeleweka.
VIPIMO.
tatizo hili linaweza kugundulika kwa kupima kiwango cha
hormone chochezi ya mayai (FSH) na hormone ya lutea kwenye damu.
MATIBABU
kitu cha kwanza ni kumshauri mtu alipata hali hii kusubiria
kwa muda wa miezi 6,wanawake walio wengi ndani ya kipindi hiki cha miezi situ
wanakuwa wamerudia katika hali yao ya kawaida.
Endapo imezidi miezi 6 au mwanamke ana uhitaji mkubwa wa
mtoto basi kuna matibabu anapatiwa. Afike kupata ushauri wa daktari.
Endapo una tatizo hili wasiliana nasi kupata ushauri wa matibabu.
whatsapp +255762167811
email: johanestinga@gmail.com
No comments