Ni
hali ya kuhisi miguu kuwa ya moto na inauma, hali hii huweza kuwa ya
maumivu madogo au makali na wakati mwingine unaweza ukakosa usingizi
kabisa wakati wa usiku kwa sababu ya maumivu. Baadhi ya visababishi vya
miguu kuwaka moto huweza kuambatana na moja kuhisi miguu inachoma kama
sindano au mwiba na mbili kupata ganzi au vyote viwili.
Ingawa
uchovu au maambukizi kwenye ngozi huweza kusababisha miguu kuwaka moto
kwa mda mfupi na kubadilika mwonekano wake wa kawaida(rangi), kuumia kwa
mishipa ya fahamu ya neva huwa ni sababu kuu ya kusababisha miguu
kuwaka moto.
Kuumia kwa neva huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama kisukari, ulevi wa pombe wa kupindukia, sumu aina fulani, upungufu wa madini na vitamin (vitamin B), au maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Vifuatavyo ni visababishi vya miguu kuwaka moto kwa undani zaidi;
Visababishi vya miguu kuwaka moto ni
-
Ulevi wa kupindukia(pombe)-( ugonjwa wa kutumia pombe)
-
Maambukizi ya fangas kwenye miguu
-
Ugonjwa wa Charcot marie tooth
-
Kutumia dawa za kutibu saratani
-
Magonjwa sugu ya figo
-
Udhaifu wa mishipa ya fahamu
-
Matumizi ya madawa
-
Ugonjwa wa mishipa ya fahamu kutokana na kisukari
-
Upungufu wa kinga mwilini(UKIMWI) au maambukizi ya VVU
-
Upungufu wa homoni (thyroid) ya tezi shingo
-
Upungufu wa vitamin mwilini(kama vile vitamin B)
Wakati gani umwone daktari?
Mwone daktari endapo
-
Maumivu ya miguu yamekuja ghafla
-
Maumivu hayo hayaishi licha ya kujipatia tiba nyumbani
-
Kama una kidonda mguuni ambacho kina dalili ya kupata maambukizi
-
Kama unapoteza fahamu kwenye miguu
-
Au endapo maumivu yanaendelea kupanda juu zaidi.
Matibabu ya miguu kuwaka moto
Matibabu
ya miguu kuwaka moto hutegemea kisababishi, kila kisababishi kina aina
yake ya matibabu. Kitu cha kwanza kabisa ni kufahamu nini
kilichosababisha maumivu hayo ili uweze kupata matibabu sahihi.
Utahitaji kuchukuliwa historia ya tatizo lako na kufanyiwa vipimo
hospitali ili kutambua kisababishi kipi haswa kinachosabaisha miguu yako
kuwaka moto.Endapo unahitaji kujua zaidi kuhusu matibabu husika basi
endelea kusoma kwenye kila kipengele cha visababishi.


No comments