MBINU ZA KUMFANYA MTOTO ALE CHAKULA

Heshimu hamu ya kula ya mwanao- Kama mwanao hana njaa, usimlazimishe kula chakula au kitu chochote kile cha kutafuna. Vivyo hivyo usimlazimishe mwanao kufasisha sahani yaani kumaliza chakula chote ulichomuwekea. ukifanya hivyo jambo hili huweza kusababisha mtoto kujilazimsha kula. Kwa kuongezea Mtoto anaweza kupata wasiwasi na kukataa au kuwa na hisia kidogo ya njaa na hivo tumbo lake huwa kama limejaa.

Mwekee au mpe chakula kiasi-Kufanya hivi unaweza kuzuia mtoto kuona balaa la chakula,pa  utampa uwanja aombe zaidi kama bado hajashiba.

Fuata utaratibu wako-Kula au mpe chakula mtoto muda na wakali ule ule kila siku. Unaweza kumpa maziwa ama juisi ya matunda na chakula. Katikati ya mlo mmoja na mwingine mpe mwanao maji na vitafunwa vingine. Ukiacha mwanao anywe maji tu na juisi na vitafunwa siku nzima huweza kupunguza hamu ya kula chakula.

Uwe mvumilifu na chakula kigeni-Watoto wadogo mara kwa mara hushika na kunusa chakula kigeni, na huweza kuweka kiwango kidogo mdomoni na kisha kutema. Mwanao anaweza kuhitaji kuonyeshwa chakula hicho mara kwa mara kabla hajaanza kula chakula hicho.

Mtie moyo mwanao kwa kuzungumzia rangi ya chakula, umbo na harufu na kama kina radha nzuri. Weka chakula kipya kila unapokuwa unampa chakula anachokipenda ili akizoee na hicho pia.

Mshawishi-Weka chakula kwenye sahani nzuri ama kisosi anachokipenda. Unaweza kukata chakula chako kwenye maumbo mbalimbali kwa kutumia kisu ili kumvutia. Mpe vyakula anavyokula asubuhi kama kifungua kinywa wakati wa usiku. Mpe chakula chenye rangi nzuri ya kuvutia.

Mwache mwanao akusaidie kufanya manunuzi-Ukiwa umeenda kununua vitu vya kula, mpe nafasi ya kuchagua matunda, mboga za majani na vyakula vingine vyenye afya. Usinunue chochote tu ambacho hutaki mwanao ale. Ukiwa nyumbani, mshawishi mwanao akusaidie kuosha mboga, atwange karanga ama aandae meza.

Kuwa mfano-Kama ukila vyakula vyenye afya njema mwanao pia atafuata jambo hilo

Kuwa mbunifu-Weka vipande vidogo vya matunda kwenye sahani ya chakula cha nafaka, au weka karoti kwenye supu nk. Fanya ubunifu mbalimbali kiasi kwamba mtoto akipende chakula.

Punguza uharibifu wa mawazo ya mtoto-Zima TV yako na vifaa vingine vya umeme ili kumsaidia mtoto awaze kula tu. Kumbuka pia matangazo ya TV kuhusu chakula huweza kumfanya mtoto apende kula vitu vyenye sukari ama kutokula vyakula vyenye afya.

Usimpe kitindamlo kama zawadi-Kusimamisha kumpa kitindamlo mwanao kuna mpa ujumbe kwamba kitindamlo ni chakula kizuri, ambapo kinaweza kumfanya mwanao apende vitu vitamu tu. unaweza kuchagua siku moja au mbili kwa wiki wakati wa usiku kama usiku wa kutumia vitindamlo na usimpe siku zingine za wiki au mzoeshe mwanao kwamba vitindamlo ni matunda, maziwa au vyakula vingine vyenye afya ili awe anavipenda na kula kila siku au mara kwa mara.


Fahamu pia

Kuandaa chakula kingine mara baada ya mtoto kukataa kile ulichoandaa huweza kusababisha mtoto kuwa mchaguzi wa chakula Fulani tu. Mtie moyo mwanao akae mezani kwa mda wote mnapokuwa manakula hata kama hali hicho chakula. Endelea kumpatia chakula chenye afya mwanao mpaka pale atakapotambua na kuvifahamu vyakula na pendeleo lake.

Kama una wasiwasi kuhusu mwanao kuchagua chakula kwamba kunamdhuru afya na maendeleo yake ya ukuaji, onana na daktari wa mwanao. Daktari atachora chati ya uzito na maendeleo ya ukuaji wa mtoto. Kwa nyongeza weka rekodi ya aina na kiasi cha chakula anachokula kwa siku tatu zilizopita. Daktari atapata picha na atakusaidia kukutoa wasiwasi. Rekodi ya chakula alichokula siku za nyuma huweza kumsaidia daktari kutambua tatizo lolote lile.

Kwa sasa kumbuka, tabia ya ulaji wa mtoto haiwezi kubadilika ghafla uamkapo asubuhi- lakini hatua ndogo ndogo zinazochukuliwa kila siku huweza kusaidia ulaji wa chakula bora kwa maisha yake yote.

No comments