Wazazi wengi
wanaweza kuandaa lishe ya watoto, lakini changamoto iliyopo ni kwamba
hawajui wanatakiwa wawe na vitu gani vya msingi na kwa kiasi gani
mchanganyiko unaotakiwa uwe.
Endapo wazazi/walezi wanaweza kuandaa lishe ya mtoto vema basi mtoto atakuwa vema kiakili na kimwili
Kwanini uwe na mchanganyiko mzuri wa chakula?
Kwanza
kabisa na ijulikane kwamba mtoto hukua haraka zaidi kuliko mtu mzima,
hivyo anahitaji aina fulani ya vyakula ili apate kukua vema, mtoto mdogo
anahitaji ale mara kwa mara ili akue haraka. Mtoto mchanga anapozaliwa
anatakiwa kunyonya maziwa ya mama tu katika kipindi chote cha miezi
sita. Usimpe mtoto vyakula vingine ikiwa pamoja na maji.
Ni kwanini ufanye hivyo?
-
Maziwa ya mama huwa yanatosha kabisa kwa mtoto,
-
Yana kinga za mwili kutoka kwa mama hivyo hujenga kinga ya mwili ya mtoto dhidi ya maradhikama kuharisha n.k
-
Maziwa ya mama pia yapo safi na tayari kutumika mda wowote ule
-
Maziwa ya mama yana vitamini, na viinirishi vingi vinavyomtosha mtoto na kumsaidia akue vema
Mtoto
aliye chini ya miezi sita atatakiwa kunywa maziwa ya mama kwa afya
bora na kuepuka magonjwa ya kuharisha na mengine ya mfumo wa tumbo
Ni makundi gani ya vyakula yanayotakiwa?
Yapo makundi mbalimbali ya vyakula vinavyohitajika katika kuandaa lishe ya mtoto, makundi hayo ni
-
Protini
-
Wanga
-
Mafuta
Pia mtoto anatakiwa kupata maji, vitamini na madini.
Nafaka/Vyakula venye wanga kwa wizi ni kama hivi vifuatavyo;
-
Mahindi
-
Mchele
-
Mtama
-
Uwele
Vyakula/nafaka zenye protini kwa wingi ni kama vile;
-
Maharagwe ya soya
-
Maharagwe
-
Dagaa
-
Samaki
-
Choroko
-
Mbaazi
Vyakula/nafaka zenye mafuta kwa wingi ni kama vile;
-
Karanga
-
blue band
-
Siagi
Jinsi gani ya kuchanganya lishe ya mtoto?
Jambo la msingi linalotakiwa kufanyika kwa ajili ya kuandaa lishe ya mtoto ni;
-
Mtoto anatakiwa apate protini kwa wingi maana huhitajika kujenga mwili yaani misuli mifupa, chembe hai za mwili, kinga ya mwili, nywele ubongo, mishipa ya fahamu n.k
-
Kiasi cha wanga kinahitajika lakini ni kwa kiasi kidogo, wanga huu hutoa (nishati) nguvu katika mwili (wanga hubadilishwa kwenda kuwa glucose ambayo hutumiwa na chembe hai za mwili kuzalisha nguvu), mtoto anapolia, anapokula, anapocheza na anapoongea hutumiwa nguvu hivyo ni lazima apate mchanganyiko wa wanga katika chakula anachopata
-
Mafuata huhitajika pia kwa kiasi, kazi ya mafuta ni kutunza joto mwilini
Kiasi
cha wanga cha kuweka kwenyemchanganyiko wa mtotokutokana na umri
hakijaandikwa katika makala haya, kama utakuwa na maswali basi tutafute
kwenye namba zetu hapo chini)
Umri wa miezi 0 hadi miezi 6
-
Kiasi cha maji ni lita 0.7 kwa kila siku
-
Kiasi cha wanga ni gramu 60 kwa kila siku
-
iasi cha mafuta ni gramu 31 kwa siku
-
Kiasi cha protini ni gramu 9.1 kwa kila siku
Kumbuka mtoto wa miezi 0 hadi miezi 6 ananyonya maziwa ya mama tu na huwa na kiasi cha kutosha kama kilivyoainishwa hapo juu
Mtoto mwenye umri wa miezi 7 hadi mwaka 1 anahitaji chakula kiasi hiki kwa siku
-
Maji lita 0.8 kwa siku
-
Wanga gramu 95 kwa siku ( asilimia 70 ya chakula)
-
Mafuta gramu 30 kwa siku ( asilimia 22 ya chakula)
-
Protini gramu 11 kwa siku ( asilimia 8 ya chakula )
Yaani
kwa maana nyingine ukiwa unaandaa chakula/lishe bora ya mtoto mdogo
hakikisha asilimia 70 ya mchanganyiko inakuwa wanga, 22 inakuwa mafuta
na asilimia 8 inakuwa chakula cha protini. Maji yatahitajika kwa kiasi
kilekile unachotumia kuandaa chakula cha mtoto.
Kumbuka
-
Watoto wanatakiwa kula mara kwa mara, mtoto mchanga anyonye mara nane kwa siku(jumla ya usiku na mchana) na mtoto mwingine ale milo isiyopungua milo nane kwa siku(mchana na usiku)
-
mfano mtoto wa miezi saba anaweza kunyonya mara 4 kwa siku na kunywa uji mara nne kwa sku kwa kiasi kinachomtosha
-
-
Mtoto anatakiw akunyonyachuchu moja kwa muda usiopungua dakika 20 kabla ya kuhamishiwa chuchu nyingine
No comments