Utangulizi
Mama
anapoenda hosptali kwa mara ya kwanza kabisa anapokuwa mjamzito hupata
fursa ya kupima vipimo mbalimbali kama wingi wa damu, kundi la damu(
A,B, AB au O) na hali ya rhesus yaani rhesus ((positive ama Negative)
chanya ama hasi))
Hali
ya Rhesus hurithiwa katika vinasaba, vinasaba hivi hutengeneza protini
inayoitwa D antigen. Ukiwa ni rhesus chanya maana yake ni kwamba unayo
protini hiyo katika chembe zako nyekundu za damu na ukiwa negative
maanake hauna protin hiyo na utaitwa rhesus hasi
Watu wengi duniani huwa ni rhesus chanya
Ni vip hali yako ya rhesus inamdhuru mtoto?
Mambo
ya madhara kwa mtoto yanatokea endapo mama ni rhesus hasi tu na anabeba
mtoto ambaye ni rhesus chanya, mtoto huyu hurithi rhesus chanya kutoka
kwa baba yake.
Kama
damu ya mtoto itagusana na ya mama wakati wa kujifungua, kinga yako ya
mwili(mama) itaamsha chembe hai za ulizi dhidi ya damu hiyo ya rhesus
chanya kutoka kwa mtoto, chembe hizi huzaliwa chemikali ambazo hukaa
mwilini kwa mda mrefu sana na hutunza kumbukumbu. Kwa mimba ya kwanza
mama atajifungua vema tu
Mama
atakapopata ujauzito mwingine basi chembe hizi na chemikali hizo hupita
katika kondo la mama na kuingia kwa mtoto na kumuua. Mambo haya hutokea
kwa sababu mtoto anaonekana kama kitu kigeni katika mwili wa mama
Hivo wamama wengi wenye tatizo hili huwa na historia ya kuwa na mtoto mmoja na mimba zinazofuata zote mtoto hufia tumboni
Je sindano hii ya ant-D hufanya kazi gani?
Dawa
hii huzuia kutengenezwa kwa kemikali zinazoleta madhara kwa mtoto pia
huharibu chembe chembe za mtoto katika mfumo wa damu wa mama na hivo
husababisha kuzuia kutengenezwa kwa kemikali hizo. Ni jambo la msingi
kuzuia kutengenezwa kwa kemikali hizi kwa sababu endapo zitatengenezwa
hudumu katika mwili wako milele
Dakitari wako atakuchoma sindano hii kwenye bega
Sindano
hii itachomwa kwenye wiki 28 na 34 za ujauzito baadhi ya klinic hutoa
kwenye wiki ya 28 na 30 kiwango kikubwa cha dozi ya dawa hii
Dawa
hii unatakiwa kupewa pia ndani ya masaa 72 kwenye tukio ambapo damu ya
mtoto itagusana na damu ya mama(wakati wa kujifungua, kupigwa tumboni,
kutokwa na damu baada ya wiki 20 za ujauzito,kutolewa maji kwenye kifuko
cha mimba,kufuzungushwa kwa mtoto ili kichwa kitangulie kutoka kwa
mtoto ambaye alikuwa ametanguliza makalio, ujauzito kutishia kutoka)
Vipi kama nina kemikali hizi zinazoua mtoto?
Mtaalamu
wa afya atakupima damu yako mapema kabisa katika ujauzito wako na
katika wiki ya 28 ya ujauzito kuangalia kama unakemikali hizi.wakati
mwingine kemikali hizi zinaweza kutengenezwa bila wewe kujua endapo
mimba ilitoka ama ujauzito ulitungwa nnje ya mfuko wa kizazi .Kama
umepimwa na ukakutwa unakemikali hizi basi hutachomwa sindano hii, kwa
sababu dawa hii huzuia kutengenezwa kwa kemikali hizo na ikiwa
zimeshatengenezwa basi hutapewa maana haitakuwa na msaada kwako.
Md\badala wake ni kwamba utahitaji kuonana na mtaalamu wa kinamama ili
upate uchunguzi na uangalizi wa karibu
Mtaalamu
huyu atakuwa anacheki hali ya mtoto endapo anaishiwa damu atapewa damu
hata kabla ya kuzaliwa. Matibabu haya huwa na matokeo mazuri na mtoto
huweza kuzaliwa, ingawa hushauriwa mtoto kuzaliwa kabla ya wakati kwa
kuanzisha uchungu ama kufanyiwa upasuaji. Mtoto anapozaliwa hulazwa wodi
maalumu ya vichanga kwa unagalizi zaidi, endapo atapata manjano atapewa
matibabu ya mwanga ili kusaidia ini lake kusafisha kemikali manjano
mwilini mwake
Nini hufanyika mtoto anapozaliwa?
Mtoto anapozaliwa damu kwenye kitofi chake huchukuliwa na kupimwa kundi lake na hali yake ya rhesus
Endapo
mtoto ni rhesus chanya, mama utchomwa sindano nyingine ya ant-D nah ii
hutolewa ndani ya masaa 72 ya kujifungua ili kwamba kinga zako za mwili
zisiamke na kutengeneza kemikali zinazoua mtoto
Endapo mtoto wako ni rhesus hasi na wewe ni hasi basi hutachomwa dawa hii.
Kwa mawasiliano na elimu zaidi na matibau tutafute kupitia namba zetu hapo chini ya website karibu sana
No comments