Kupinda Kwa Nyeti Ya Mwanamme (Peyronie’s Disease)

Peyronie's Disease ni ugonjwa unaotokana na kutengenezwa kwa uvimbe mgumu(Plaque) ulio kama kovu kwenye misuli ya uume,hali hii husababisha uume kupinda kuelekea sehemu iliyoathirika.

Hili ni tatizo la kupinda uume au kuwa kuwa mwembamba , mara nyingine hambatana na maumivu. Kuharibika kwa umbo la uume hutokea baada ya kuumia na hasa upande wa juu wa kiungo hiki. Baada ya kuumia , hutokea maumivu wakati uume ukisimama kwa kipindi kama cha miaka miwili hivi. Baadaye maumivu hupotea, lakini uume hubaki ukiwa umepinda.

Zifuatazo ni sababu za uume kupinda kama zilivyoorodheshwa hapo chini:
  • Kuharibika kwa umbo la uume hutokea baada ya kuumia na hasa upande wa juu wa kiungo hiki.
  • Baada ya kuumia, hutokea maumivu wakati uume ukisimama kwa kipindi cha miaka miwili hivi.
  • Baadaye maumivu hupotea, lakini uume hubaki ukiwa umepinda.
  • Uume kupinda pia huweza kutokea kiasili yani bila sababu yoyote.
  • Uume kupinda pia huweza kutokea bila maumivu yoyote hivyo ikawa si ugonjwa.
  • Kuvaa chupi zinazobana haswa kipindi cha balehe huchangia uume kupinda.
Image result for peyronies 


DALILI ZA TATIZO HILI 
 Katika hatua za mwanzo mtu hupata maumivu kwenye uume, Pia maumivu wakati uume unaposimama na matitizo ya uume kushindwa kusimama au kutosimama vizuri(Weak erections),Maumivu haya yanaweza kuwa kidogo au yanaweza kuwa makali sana kiasi cha mtu kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku.Na maumivu ya uume huwa makali sana hasa wakati wa usiku

Baadae maumivu ya uume huisha ila uume unabaki umepinda hali inayopelekea kupata shida wakati wa tendo la ndoa.

MATIBABU
Matibabu ya tatizo hili yamegawanjika katika aina mbili,kwa njia ya upasuaji na kwa njia ya madawa.

Upasuaji
Upasuaji hufanyika kwa kuondoa Uvimbe au kovu linalopelekea uume kupinda,
Kama tatizo hili limepelekea mtu kupata matatizo ya uume kusimama basi anawekewa kifaa maalumu cha kusaidia uume kusimama(Penis implant)
Image result for peyronies disease treatment

Madawa
Mbali na upasuaji,njia nyingine ya kutibu tatizo hili ni kwa kuchoma dawa zinazosaidia kuyeyusha kovu/uvimbe unaosababisha uume kupinda.Dawa hizi zinachomwa katika sehemu iliyoathirika.

Hivyo basi unapopata dalili za tatizo hili wahi hospitali kupata msaada wa kitabibu.

 




No comments