Reye’s syndrome Tatizo linaloweza kusababishwa na matumizi ya aspirine


Reye’s syndrome ni hali inayojitokeza kwa nadra lakini ni tatizo endapo itatokea ambalo husababisha kuvimba kwa ini na ubongo. Tatizo hili mara nyingi huathiri watoto wa rika dogo ambao wanapona kutoka kwenye maambukizi ya virusi mara nyingi mafua ama tetekuwanga.

Dalili na viashiria kama kuchanganyikiwa, degedege na kupoteza fahamu huhitaji matibabu ya haraka.  Kugunduliwa mapema na kupata matibabu huweza kuokoa maisha ya mtoto.

Dawa ya aspirini imekuwa ikihusishwa na tatizo la reyes syndrome, kwa hivo chukua tahadhali unapokuwa unampa mtoto ama kijana wako dawa hii. Ingawa dawa ya aspirini inashauriwa kuanza kutumika kwa watoto walio na miaka kuanzia miwili(2), watoto wanaopona kutoka kwenye maambukizi ya mafua na tetekuwanga hawatakiwi kutumia dawa hii kabisa. Ongea na daktari wako endapo  unataka ufafanuzi zaidi

Dalili
Mtoto mwenye tatizo la reyes mara nyingi kiwango cha sukari wmilini hushuka wakati kiwango cha kemikali za ammonia na hali ya aside ya damu huongezeka, wakati huo huo ini huvimba na hukusanya kiwango kikubwa cha mafuta- hukaliwa na kiwango kikubwa cha mafuta. Uvimbe unaweza kutokea pia kwenye ubongo, na hupelekea kupata degedege na kupoteza fahamu.
Dalili za reyes syndrome hutokea mara nyingi siku ya 3 hadi 5 baada ya kupata maambukizi ya virusi wa tetekuwanga mafua ama maambukizi kwenye mfumo wa juu wa hewa kama mafua.

Daliliz a awali za reyes syndrome

  • Watoto walio chini ya umri wa miaka 2 hupata dalili za
  • Kuhara
  • Kupumua kwa haraka

Dalili za ziada
  • Hali ya ugonjwa inapozidi kuwa mbaya dalili na viashiria na viashiria vinavyojitokeza huwa mbaya zaidi kama;
  • Mtoto kulialia, kuwa mkali au tabia zisizo za kawaida
  • Kuchanganyikiwa, kutotambua mata, kuwa mkali au tabia zisizo za kawaida
  • Kuchanganyikiwa, kutotambua mazingira na kupata ndoto
  • Kuchoka au kupooza kwa miguu na mikono
  • Degedege
  • Mwili kulegea sana
  • Kupungua kwa ufahamu

Wakati gani wa kumwona daktari
Kugunduliwa mapema na kupata matibabu ya tatizo la reyes syndrome huweza kuokoa maisha ya mtoto, kama unashuku mwanao ana tatizo hili basi mwahishe mara moja hospitali

Visababishi

Visababishi halisi vya tatizo la reyes syndrome huwa havifahamiki, ingawa kuna mambo kadhaa huchangia katika usababishaji wa tatizo hili. Tatizo hili huonekana kuamshwa na matumizi ya dawa ya aspirini kutibu maambukizi ya virusi sana sana mafua na tetekuwanga kwa watoto ama vijana wadogo ambao wanatatizo la uchakataji wa mafuta kwenye ini.
Matatizo ya uchakataji wamafuta kwenye ini huwa ya aina nyingi na hurithiwa, tatizo hili huambatana na kushindwa kwa uvunjwaji wa mafuta kwa sababu vimeng’enya vinakosekana au havifanyi kazi ipasavyo. Kipimo cha ugunduzi kinahitajika kugundua kama mwanao ana tatizo la uchakatuajiw a mafuta.

Kwa baadhi ya wagonjwa, tatizo la reye’s syndrome huweza  kuwa tatizo ndani ya mwili amabalo hufunuliwa-huwekwa hadharani na maambukizi ya virusi. Sumu kama dawa za kupuliza kwa ajili ya kuuwa wadudu, madawa ya kienyeji na rangi za kupaka pia huchangia kusababisha tatizo hili

Vihatarishi

vihatarishi vifuatavyo vikitokea kwa pamoja siku zote huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo la reyes syndrome.
Matumizi ya asipirni kwa mgonjwa mwenye virusi kama mafua, tetekuwanga au maambukizi ya mfumo wa juu wa hewa.
Kuwa na tatizo kwenye ini la uchakataji hafifu wa mafuta

Madhara

Watoto wengi na vijana walio chini ya miaka 20 wakipatatatizo la reyes syndrome hupona ingawa huweza kuachwa na uhalibifu wa kudumu kwenye ubongo. Bila uchunguzi na amtibabu sahihi tatizo hili huweza kusababisha kifo siku chache baadae

Vipimo na matibabu

Hakunakipimo maalumu cha kugundua tatizo la reyes syndrome. Ingawa vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika viwili ama kimojawapo.

  • Kipimo cha kuchukua maji wkenye uti wa mgongo
  • Kipimo cha kuchukua kinyama kwenye ini
  • Kipimo cha CT
  • Kipimo cha ngozi
     
Matibabu

Matibabu ya reyes syndrome hufanyika hospitali. Mgonjwa mwenye hali mbaya zaidu hutibiwa kwenye chumba cha uangalizi makini yaani ICU. Wafamnyakazi wa hospitali watakuwa wakipima shinikizo la damu la mtoto kwa karibu sana na vipimo vingine vya uhai. Matibabu huwa pamoja na;

  • Kuwekewa maji kenye mishipa
  • Madawa ya kupunguza maji mwilini-mdawa haya hupunguza uvimbe na shinikizo kichwani kwa njia ya kukojoa.
  • Madawa ya kuzuia kutokwa damu- kutokwa damu kutokana na kuharibiwa na ini hutibiwa kw akutumia vitamini K, kuongezewa giligili ya plasma na chembe sahani.
  • Kama mtoto anapata shida ya kupumua basi atawekewa mashine ya kumsaidia kupumua





No comments