Maziwa ya kopo (baby formula) ni maziwa ya ngo’mbe wana ya process
na kuweka kwenye mfumo wa powder,na kuongezea virutubisho vingine.Maziwa
ya kopo yana utofauti sana na maziwa ya mama sababu maziwa ya mama
yanavirutubisho vingi ni asilia vinavyo mpa mtoto kinga mwilini na
kumwongezea uzito mtoto kwa haraka ,wakati maziwa ya kopo yanachukua mda
kumkuza mtoto na kumpa kinga ndogo mwilini na kumfunga choo.
sababu zitakazo pelekea mtoto kupewa maziwa ya kopo?
Mama kutokuwa na maziwa ya kutosha
Mtoto kutokushiba maziwa ya mama(hayamtoshi)
Mama kupatwa dharura (kupata safari ya mda mrefu,kuumwa au kifo n.k)
Wazazi wengi wanakosea kuwapa watoto maziwa ya kopo kusipo sababu
maalum,mtoto anatakiwa apewe maziwa ya kobo iwapo kuna sababu malum na
ushauriane na daktari, lasivyo ni vizuri mtoto anyonyeshwe maziwa ya
mama ili apate virutubisho na kinga mwilini vitakavyo mwepusha na
maradhi.
Aina za maziwa ya kopo
Kuna aina nyingi za maziwa ya kopo ya watoto ,kuna mengine
yalishawahi pigwa marufuku nchini Tanzania kama (lactogen n.k)ila kuna baadhi
yanatumika na ni mazuri kama
:Nan,
:Sma kopo la gold
:S26 kopo la gold
:Baby infant
:Cow gates
MADHARA YA MAZIWA YA KOPO
Maziwa ya kopo ni hatari sana kwa watoto sababu uaminifu ni mdogo
,kwa mfano Tanzania wafanya biashara wengi sio waaminifu wanauza maziwa
fake kwa kujali maslai yao na selikali inatoa onyo mara kwa mara,mzazi
unatakiwa kuwa makini sana maziwa fake huadhiri ini,figo
,kuhara,kutapika,kupata rashes,maumivu ya tumbo au kupata cancer .
USHAURI TOKA AFYA BORA KWA MTOTO
1:Maziwa ya kobo ukifungua kutumia unatakiwa utumie kwa siku 30 zaidi hapo hayafai tena kutumika mwaga.
2:Chemsha maji ya kutengenezea maziwa kabla hujachanganya na maziwa.
3:Hifadhi maziwa kwenye chombo cha plastic chenye mfuniko hakikisha
hewa haipiti,kopo la maziwa yenye material ya steel(bati) ni sumu mbaya
huchochea kupata cancer kwa urahisi.
4:Unachotakiwa nunua maziwa yalio pakiwa kwenye makopo ya plastic
au box dogo hayo ni mazuri zaidi kama cow gate,sma haya yatatoka Uk.
5:Soma expiry date(siku ya mwisho maziwa kutumika) ni hatari sana,usimpe mtoto bila kusoma tarehe.
6:Yakague maziwa kwa kuweka kwenye chombo cha plastic mara nyingine yanakuja na uchafu ndani mende,pini n.k
7:Maziwa mengine huwa yanakataa watoto wanapata maumivu ya tumbo wengine hutapika hivyo unaweza mbadilishia.
8:Nawa mikono yako kwa maji safi kabla hujamtengenezea maziwa mtoto
9:Maziwa ya mama ni muhimu kuliko ya kopo au ng’ombe mtoto anakuwa na kinga kubwa mwilini yako ni salama zaidi kwa afya yake.
No comments