Matege ni hali ya mifupa kuwa laini na dhaifu, hali
hii husababishwa na kuwepo kwa upungufu endelevu wa madini ya vitamini D
kwa watoto.
Vitamini D huongeza ufyonzaji wa madini ya kalisium na
phosphorua kutoka kwenye mfumo wa chakula-utumbo na kuingia kwenye
damu. Upungufu wa vitamini D husababisha uwiano wa madini ya kalisium na
phosphorus kuharibika na hivyo mifupa kuwa dhaifu na kupata tatizo la
matege-rickets.
Kama upungufu wa vitamini D ama kalisiumu utasababisha
matege, kwa kuongeza vitamin D ama Madini ya kalisium kwenye chakula
huweza kunaweza kurekebisha tatioz la matege kwa mwanao. Matege kutokana
na tatizo la kijeni-kuzaliwa nalo huwa vigumu kutibika na huhitaji
matibabu ya ziada. Baadhi ya matatizo ya mifupa huweza kurekebishwa kwa
njia ya upasuaji.
Dalili
Dalili za tatizo la rickets huwa pamoja ni
-
Kuchelewa kukua
-
Maumivu ya utu wa mgongo, kiuno na miguu
-
Misuli kuwa dhaifu
Kwa sababu tatizo la rickets huathiri chembe za ukuaji wa mifupa, mwisho wake husababisha matatizo ya mifupa kama
-
Kupinda kwa miguu kama upinde wa mvua
-
Viganja na magoti kuwa nene
-
Mifupa ya kwenye chuchu kutangulia mbele zaidi
-
Wasiliana na daktari wako endapo mwanao anaonekana kupinda miguu
Visababishi
Mwili wako unahitaji vitamin D ili kufyonza madini ya
kalisiumu na phosphorus kwenye chakula kinachoingia tumboni. Tatizo la
rickets huweza kutokea endapo mwanao anakosa kiwango cha kutosha cha
vitamini D au mwili wake unashindwa kutumia vema vitamin hii kutokana na
matatizo katika chembe hai.
Upungufu wa vitamini D Unaweza kupata vitamin D kutokana na
Mwanga wa jua-
ngozi huwa na uwezo wa kuzalisha vitamin D endapo itaanikwa kwenye jua
haswa lile la asubuhi. Watoto walio kwenye nchi zilizoendelea hukaa kwa
kiwango kidongo kwenye mwanga wa jua, na pia hukaa kwenye nyumba zenye
vioo ambavyo haviruhusu kupitishwa kwa mwanga wa jua na hivyo kutopigwa
na mwanga wa jua na kukosa vitamin D.
Chakula
Mafuta ya samaki, kiini cha mayai. Baadhi ya vyakula
siku hizi vimeongezewa madini ya vitamini D kama vile maziwa, vyakula
vya nafaka na vinywaji vya matunda. Watoto ambao hawapati vyakula hivi
hupata tatizo la rickets
Tatizo la ufyonzaji
Baadhi ya watoto wamezaliwa na tatizo la kiafya linalozuia ufyonzaji wa vitamini D kama vile
-
Ugonjwa wa celiac
-
Ugonjwa wa Michomo kwenye mfumo wa chakula IBD
-
Ugonjwa wa cystic fibrosis
-
Matatizo ya figoVihatarishi
-
Umri miezi 3 hadi 36 huwa hatarini kupata tatizo la rickets kwa sababu mifupa yao hukua haraka sana
-
Ngozi nyeusi- ngozi nyeusi huwa haipokei mwanga wa jua vema kuliko ngozi nyeusi hivyo huzalisha vitamin D kwa kiwango kidogo.
-
Mazingira- watu wanaoishi mazingira ya kaskazini mwa dunia hupata mwanga wa jua kwa kaisi kidogo na hivyo hutengeneza kiwango kidogo cha vitamini D.
-
Kuzaliwa kabla ya umri-njiti
-
Madawa ya kutibu kifafa- huwa na mwingilino katika utumiaji wa vitamini D kwenye chembe za mwili.
-
Kunyonya maziwa tu-maziwa ya mama huwa hayana kiwango cha kutosha kuweza kuimarisha mifupa. Watoto wanaonyonya maziwa ya mama tu wanatakiwa kupata matone ya vitamini DMadhara
-
Kushindwa kukua
-
Uti wa mgongo kupinda
-
Matatizo ya mifupa kufanyika vibaya
-
Matatizo ya meno
-
Kifafa
Vipimo na utambuzi
Daktari atamchunguza mwanao kwa kubonyehsa kwa kiasi
kwenye mifupa ya mwanao kuangalia udhaifu na atatia umakini kwenye
mifupa ya;
Kichwa- mtoto anaweza kuchelewa kufunga kwa utosi
Miguu-watoto wagodo huonekana na miguu upinde kiasi, ila watoto wenye upungufu wa vitamini D huwa na upindi unaoonekana sana.
Kifua- huchomoza mbeleviganja
Magoti na viganja- huwa kubwa kuliko kiasi
Kipimo cha xray pia huweza kuonyesha udhaifu katika mifupa ya watoto
Matibabu
Matibabu ya dawa kama vitamini D na Madini ya kalisium. Fuata ushauri wa daktari wako kuhusu matumizi ya dawa hizo
Matibabu ya upasuaji-
kama miguu imepinda kama upinde wa mvua, daktari anaweza kukushauri
kutumia viatu ama vazi maalimu linaliweza kunyoosha miguu. Matatizo
makubwa ya kupinda miguu huweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji.
Kijikinga na upungufu wa vitamini D
Watoto wengi na vijana wanapata kiasi cha kutosha cha
vitamini D kutoka kwenye jua. Vichanga na watoto wadogo kabisa huweza
kukosa kiasi cha vitamini D kinachohitajika kwa sababu hawakai kwenye
mwanga wa jua
Kama ndo hivyo basi hakikisha mwanao anapata kiasi cha
kutosha cha vyakula vyenye vitamini D kama mafuta ya samaki, kiini cha
yai au vyakula vya kusindikwa kama
-
Maziwa ya kopo
-
Nafaka
-
Maziwa
-
Juisi ya machungwa
No comments