JE KULA NANASI WAKATI WA UJAUZITO INA MADHARA?

Kumekua na imani na  maneno kwamba mama mjamzito hapaswi kula nanasi wala kunywa juisi ya nanasi kwani ina madhara kwa mama mjamzito.Watu wamekuwa wakiamini kwamba ulaji wa nanais wakati wa ujauzito unaweza kupelekea mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati. Je swali hili lina ukweli wowote ndani yake?

Jambo hili si kweli. Japo ndani ya nanasi kuna kiambata kinachhoitwa BROMELAIN ambacho hutumika kutengenezea dawa ya maumivu na kuvimba (ant inflammatory), dawa hii ikitumika kwa mama mjamzito husababisha mimba kuharibika na hairuhusiwi kutumika wakati wa ujuzito.ila kiwango cha kiambata hiki kilichomo kwenye Nanasi ni kidogo sana.Kipo katika kiwango kidogo mno ambacho hakiwezi kuleta madhara yoyote kwa mama mjamzito. Inahitajika ule mananasi 10 kwa wakati mmoja ndo ufikie kiwango cha Bromelain kinachoweza kuleta madhara kwa ujauzito.

Hivyo basi ulaji wa nanasi wakati wa ujauzito hauna madhara bali ni muhimu kwa nanasi lina kiwango kikubwa cha Madini chuma(iron) na folate ambayo ni muhimu katika kutengeneza damu.Pia nanasi lina vitamini Muhimu zinazohitajika na mama mjamzito.


9 comments:

  1. Asante kwa Elimu maana watu taarifa zisizo za kitaalam ni nyingi

    ReplyDelete
  2. Asante kwa Elimu maana watu taarifa zisizo za kitaalam ni nyingi

    ReplyDelete
  3. Asante kwa ushauri maana kila mtu ni mtaalamu yaan lilikuwa linanipa mawazo sana

    ReplyDelete
  4. Asante Sana niliogopa Sana sikia habari mbaya kuhusu nanasi

    ReplyDelete
  5. Asante ban ngoj niendelee kula

    ReplyDelete
  6. Asanteni sana kwa kujali afya zetu .mungu aendelee kuwapa nguvu🙏

    ReplyDelete