Tatizo la kutumia vijiuasumu(Antibiotics) bila ya
kupata vipimo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya limekua kubwa ambalo
linasababisha madhara ya kiuchumi na uhai kutokana na kuzidiwa na vimelea vya
ugonjwa ambavyo vinakua sugu kutokana na
matumizi mabaya ya dawa hapa nchini
Dawa za Antibiotiki ni dawa ambazo zipo kwenye kundi kubwalinalojulikana kama antimicrobials. Antimicrobials ni dawa ambazohutumika kuua au kuzuia ukuaji wa vimelea vinavyosababishamagonjwa ya kuambukiza kwa binadamu na wanyama
Tafiti za Kimataifa zinaonesha kuwa kuna
ongezeko kubwa duniani lamatumizi ya dawa za
antibiotikis’. Kwa mwaka 2000-2010 matumizi yadawa za antibiotiki
yaliongezeka kwa asilimia thelathini
(30%). Pia,tafiti hizo zinaonesha kuwa kwa mwaka 2010 jumla ya tani 63,200
zaantibiotiki zilitumika kwa mifugo peke yake.
Dawa hizo zinatumika vibaya, ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 20-50 ya antibiotiki zinatumika isivyo sahihi duniani.
Hapa nchini Tanzania, Utafiti uliofanywa na Wizara mwaka 2014 katikamikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza ilioneshamatumizi makubwa ya dawa za antibiotiki hadi kufikia asilimia 67.7.Pia,
tafiti zimebainisha kuongezeka kwa kiwango cha usugu waantibiotikisi. Mfano, utafiti wa kitaifa uliofanyika juu ya usugu wa dawaza kifua kikuu (MDR-TB) ilionesha usugu wa dawa kwa wagonjwawapya kuwa ni asilimia 1.1; na kwa wagonjwa wanaorudia dawa zaTB baada ya kupona kuwa na usugu wa asilimia 3.9. Pia, katika kutibuugonjwa wa malaria, usugu wa dawa za Chloroquine naSulfadoxine/Pyrimethamine, au “SP” ulijitokeza na kupelekea kutumikakwa dawa ya sasa iitwayo Artemether/Lumefantrine, au “ALU”.
Katika tafiti ya kutibu maambukizi ya njia ya mkojo (Urinary TractInfection, au “UTI”) kwa kutumia dawa ya sindano ya gentamycinuliofanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilionesha kuongezekakwa usugu wa dawa hiyo kutoka asilimia 6.9 mwaka 2003 hadi asilimia44 mwaka 2011. Aidha, katika kutibu ugonjwa huo, tafiti nyingine1
ilifanyika
katika hospitali ya
Rufaa ya Kanda
ya Bugando, ambapoimeripotiwa kuongezeka
kwa usugu wa
dawa ya sindano
yaceftriaxone kutoka asilimia 14 mwaka 2009 hadi asilimia 29.4
mwaka2011.
SABABU ZINAZOCHANGIA TATIZO HILI.
Zipo
sababu nyingi zinazochangia uwepo
wa usugu wa
dawa zaantimicrobials. Mojawapo
ni maduka mengi
ya dawa kuuza
kwawananchi dawa za antimicrobials bila cheti cha daktari au kutotoa
dozikamili. Ikumbukwe kuwa dawa za antimicrobials hutolewa
kwa cheticha daktari tu
Wakati
mwingine dawa za
binadamu hutumika kutibia
wanyamakinyume na sheria za matumizi ya dawa. Pia wapo
wafanyabiasharawanaoandaa vyakula vya
wanyama ambao wamekuwa
na tabia yakuongeza
antimicrobials kwenye vyakula
hivyo kwa kufikiria
kuwazinasaidia mnyama husika kukua haraka na kutopata magonjwa.

Madhara yanayoweza kutokea kutokana na usugu wa dawa zaantimicrobials ni pamoja na magonjwa kushindikana kutibiwa nadawa hizo na hata kuweza kusababisha vifo.
Matibabu mbadala baada ya dawa za kawaida kuwa sugu yanakuwana gharama kubwa na ya muda mrefu. Mfano, matibabu ya mgonjwampya wa Kifua Kifuu kwa dawa za kawaida yanafanyika kwa kipindicha miezi sita na yanagharimu takribani shilingi laki nne (400,000/=).

Madhara yanayoweza kutokea kutokana na usugu wa dawa zaantimicrobials ni pamoja na magonjwa kushindikana kutibiwa nadawa hizo na hata kuweza kusababisha vifo.
Matibabu mbadala baada ya dawa za kawaida kuwa sugu yanakuwana gharama kubwa na ya muda mrefu. Mfano, matibabu ya mgonjwampya wa Kifua Kifuu kwa dawa za kawaida yanafanyika kwa kipindicha miezi sita na yanagharimu takribani shilingi laki nne (400,000/=).
Ikitokea mgonjwa huyo akapata kifua kikuu sugu matibabu hayoyanatibiwa kwa miezi 20 hadi 22 na gharama zake ni takribani shilingimilioni kumi na saba. Kama mgonjwa huyo atapata kifuu kikuu SuguZaidi matibabu yake yanakuwa ya muda mrefu zaidi na gharamakubwa takriban shilingi milioni 64.
Watanzania wanashauriwa kuacha mazoea ya kununua dawa ovyobila kupata cheti cha Daktari na ushauri wa wataalamu wa afya.Ndugu wananchi, vile vile nasisitiza ni muhimu sana kumaliza dozi zadawa.
Kila mmoja wetu ana mchango mkubwa katika kuzuia uwezekano wavimelea kujenga usugu dhidi ya dawa za antimicrobials. Mapambanodhidi ya usugu wa dawa za antimicrobials yatafanikiwa tu pale ambapomimi na wewe kwa ujumla tutashiriki katika vita hii.
“Fuata ushauri wa wataalam wa afyakabla ya
kutumia antibiotiki”
No comments