Watoto wachanga wanasumbuliwa na chango(colic) wanapokuwa na umri wa
wiki 2 baada ya kuzaliwa ndipo wanapata achango. Chango ni maamivu
makali ya tumbo anayopata mtoto na kulia mara kwa mara ikiwa usiku ,
mchana au jioni ,anaweza kulia zaidi ya msaaa 3 kwa siku usiku .
Chango inachukua mda wa miezi 3-4 ndio mtoto apone,ingawa sio watoto wote wanapata na tatizo la chango.
Sababu za kuleta chango kwa mtoto?
-
Maziwa ya ngo’mbe yana protein nyingi , lactose inayopatikana kwenye
baby formulas .(hayo yote yanaweza mletea allergy na maumivu ya tumbo)
-
Mtoto atakapo nyonyeshwa sana mpaka kuvimbilwa (overfeeding)huchochea chango.
-
Hormones-zinachochea mletea maumivu ya tumbo (mtoto akiwa na stress
ya mazingira au mama anaposhindwa kumweka position nzuri wakati wa
kunyonya)
-
Gesi – mtoto ,akiwa analia au kunyonya kwa haraka anameza hewa inayokuja kuleta gesi na kumuumiza tumbo.
-
Kiungulia(heartburn)
Dalili ya chango kwa mtoto (colic)
Mtoto atalia sana kilio chake kitakuwa tofauti na kile cha kawaida
akiwa na( njaa,usingizi , au akiwa kajisaidia n.k). Analia sana
akijikunja tumbo ,kunyoosha miguu au vidole uso utabadili rangi na kuwa
mwekundu , pia anaweza kujamba mara kwa mara.
Utamsaidia vipi mtoto
-
Mama unatakiwa kuacha kula baadhi ya vyakula kwa kipindi hiko cha
miezi 3-4 ambayo inamsumbua mtoto na chango,kama (kabichi,maziwa
yango’mbe au nido, cheese ,kahawa,broccoli,maharage
-
Baada ya kumnyonyesha mweke begani na mpige pige mgongoni ili abeuwe itamsaidia
-
Mama unapo nyonyesha mtoto hakikisha mtoto anaingiza mdomo kwenye
chuchu yote na kufunika ule mstari mweusi bila kuacha nafasi akaingiza
hewa mtumboni.
-
Mfanyie massage ya tumbo- tumia mafuta ya maji weka mkononi sugua
viganja vyako vikipata joto mpake tumboni kuanzia juu kuja chini
litaletea na gesi zitatoka.
-
Weka maji vuguvugu kwenye beseni na mweke mtoto akae kwa dakika 10-15.
-
Weka maji vuguvugu kwenye chupa ya plastik funika na taulo mwekee mtoto tumboni(hakikisha -maji yasiwe yamoto sana ukamuunguza.
-
Mbebe mtembe tembe au kama kunakiti chake kile cha bembea mweke abembe atanyamaza.
-
Mtoe nje apate fresh air.
-
Mtoto akilia sana washa vacuum cleaner au radio inamfanya anyamaze.
-
Mbadilishie maziwa ya aina nyingine kama unampa ya kopo(baby formula)
-
Usimlishe sana mpaka akavimbilwa(overfeeding)
-
Kuna dawa za colic
Tiba
Kunadawa za aina tofauti ila usimpe kabla ujaonana na daktari kwani
mtoto ni mdogo sana huyo anahitaji uangalizi wa hali ya juu. Soma
vipimo vya dawa utakavyopewa kabla ujampa mtoto.
No comments