Utunzaji
wa meno ya watoto unahitaji uangalizi mkubwa kama ilivyo kwa watu
wazima, na upuuzaji wa suala hilo unaweza kuwa na madhara ya muda mrefu
maishani. Hii ndio maana madaktari wa meno wanashauri kuwa, ni vyema
meno ya watoto yakaanza kusafishwa tangu pale linapochomoza au kuota
jino la awali kinywani na ikiwezekana hata kabla ya hapo.
Baadhi ya
wataalamu wanashauri wazazi kutumia kitambaa na maji safi kusafishia
meno ya mtoto, huku akiwa ameketi katika hali ya utulivu. Itafahamika
kuwa bacteria au vijidudu maradhi huishi kwenye sehemu ile ya jino
iliyofunikwa na utando wa vyakula uliong'ang'ania kwenye jino.
Bacteria
hao hukutana na chakula na kusababisha asidi na hatimaye hutengeneza
tundu au mmomonyoko katika meno. Utando huo unapaswa kuondolewa kila
siku wakati unapopiga mswaki ili kuhakikisha kuwa meno na fizi zako ni
safi na salama.
Wazazi wanapaswa kuzingatia usafi wao wa kinywa pamoja
na wa watoto wao. Vijidudu hivyo maradhi vinapatikana ndani ya mate na
kwa hivyo ni rahisi kuenezwa kutoka kwa mzazi hadi kwa moto wakati wa
kubusiana au kushumiana na kupitia uchangiaji wa vyombo vya chakula.
Wazazi au walezi wanapaswa kubeba jukumu la kusimamia afya ya kinywa ya
watoto wao hadi hapo watakapofikia umri wa kati ya mia minane au tisa.
Kwani wataalamu wanasema kuwa katika kipindi hicho, watoto huwa hawana
uwezo wa kujisimamia katika kuboresha usafi wa meno unaotakikana. Mtoto
anaweza kuanza kusafisha meno yake kwa kutumia mswaki vile
inavyotakikana chini ya usimamizi wa wazazi au walezi akiwa na umri wa
miaka saba.
Usafi wa kinywa na meno unapaswa kuanzishwa hata kabla
ya mtoto hajaanza kuota meno. Fizi za watoto wachanga na wale wa
chekechekea zinaweza kusafishwa kwa kufutwa kwa utaratibu kwa kutumia shashi au gauze, au hata kitambaa kisafi chenye unyevunyevu. Kitendo
hicho huchangamsha pia fizi za mtoto na kusaidia kupunguza baadhi ya
maumivu ambayo huwapata watoto wakianza kuota meno. Madaktari wa meno
wanasema kuwa, mara meno ya mtoto yanapochomoza , yanapaswa kusafishwa
kwa mpangilio angalau mara mbili kwa siku, baada ya kifungua kinywa na
kabla ya kulala, yaani usiku, bila ya kusahau ulimi.
Imeelezwa kuwa
kwa watoto wadogo yaani wale wa chekechea, wazazi wanashauriwa kutumia
kiwango kidogo cha dawa ya meno yaani dawa hiyo iwekwe kwenye shashi au
gauze na wasafishe meno ya watoto wao kwa utaratibu. Na ikiwa meno yote
ya mbele ya mtoto wako yameota, unashauriwa kutumia mswaki mdogo wa
watoto. Njia nyepesi ya kumsafisha mtoto ni kuhakikisha kuwa kichwa
chake kimejiegemeza kwenye mapaja yako, ili uweze kuona vyema ndani ya
kinywa chake na kuyasafisha kama inavyotakikana, huku mtoto akiwa katika
hali ya utulivu. Na iwapo mtoto atakuwa mkubwa kuanzia miaka saba
anaweza kusimama mkabala na mzazi wake huku ukikiinua kichwa chake
ilikuweza kufikia na kuona vizuri meno yote.
Mara nyingine wazazi
wamekuwa akishuhudia watoto wao wakitokwa na damu kwenye fizi wakati
wakipigwa mswaki. Jambo hili lisiwazuia wazazi kuwasafisha meno watoto
wao. Kuvuja damu fizi ni ishara ya kuathiriwa na maradhi. Kwa hiyo
uvujaji huo wa damu hutatokomea iwapo utando unaong'ang'ania kwenye meno
na bacteria au vijidudu maradhi vitaondolewa.
Kwa kuzingatia kuzagaa
aina mbalimbali za dawa za kusafisha meno(au tooth paste) katika maduka
mbalimbali hivi sasa, wazazi wanakabiliwa na halingumu katika kuchagua
dawa ipi ni bora kwa usafi na utunzaji wa meno ya watoto.
Lililo na umuhimu hapa ni kufahamu kiasi kinachotakikana kutumia katika
mswaki wa mtoto wako na si aina ya dawa. Kiasi kidogo tu cha dawa ya
meno kinatakikana kwa mtoto wako na si kurundika lundo la dawa, hiyo
haina faada yoyote ghairi ya kumletea madhara.
Dawa ya meno haipaswi
kumezwa. Hatua ya kumeza au kulal kiasi kikubwa cha dawa ya kusafishia
meno inazidisha hatari ya kuoza meno ya muda ya watoto yaani(permanent
teeth, khususan kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Kwa
sababu hiyo wataalamu wa meno hawashauri kutumia dawa za kusukutulia
kinywa yenye kampaundi ya fluoride kwa watoto chini ya miaka sita, kwa
sababu hawawezi kujizuia kumeza na hivyo huwa na uwezekano mkubwa wa
kukumbwa na maradhi ya fluorosis.
Je mnafahamu kuwa chakula kina
athari kubwa katika afya ya kinywa na meno ya mtoto wako?Uchaguzi wa
vyakula na mipangilio ya ulaji inayoasisiwa tangu kipindi cha utotoni
unaweza kuwa na taathira kwa afya ya uhai wa maisha yako yote. Mlo
kamiliunaojumuisha vyakula vya aina tatu kwa siku(Yaani
protini,vitaminina wanga ) unapaswa kushajiishwa. Hatua ya kujumuisha
mada za protini katika milo hiyo husaidia watoto kutohisi njaa haraka,
na hivyo kumfanya mtoto kukosa hamu ya kukimbilia kula vyakula visivyo
na manufaa kama vile vyenye sukari nyingi. miendo bora ya ulaji chakula pamoja na
usafi wa kinywa unaotakikana si tu kuwa humuepusha mtoto kuoza na
kuharibika kwa meno yake, bali pia humfanya mtoto kimwili kuwa katika
afya njema.


No comments