MAAMBUKIZI KATIKA KUTA ZA NDANI ZA MOYO (INFECTIVE ENDOCARDITIS)



 leo tutazungumzia maradhi ya moyo yanayotokana na maambukizi na tutaelezea maambukizo katika kuta za moyo au  kitaalamu Infective endocarditis. Karibuni mjumuike nasi hadi mwisho wa kipindi.

Maambukizi katika kuta za ndani za moyo hutokea wakati vimelea ambavyo kwa kawaida huwa bakteria, vinapovamia kuta za ndani za moyo zikiwemo valve na kusababisha maambukizi.  Kwa kuwa katika moyo hakuna mishipa ya damu inayopeleka damu safi moja kwa moja kwenye valve za moyo, hivyo chembe chembe nyeupe za damu zinazoimarisha kinga dhidi ya maambukizi, hufika kwa shida sana kwenye valve za moyo. Pale vimelea au bakteria wanapotengeneza uoto kwenye valve za moyo, hali hii husababisha chembe chembe nyeupe kuwa butu. Kukosekana mishipa hiyo ya damu ambayo kazi yake ni kupeleka damu moja kwa moja kwenye valve za moyo, hufanya matibabu ya ugonjwa huu kuwa mgumu, kwa kuwa ni vigumu dawa kufika kwenye eneo husika.

 Maambukizi katika kuta za ndani za moyo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili kutokana na jinsi ugonjwa unavyoanza. Moja ni maambukizi ya kuta za ndani za moyo ya papo kwa hapo yanayoitwa kitaalamu acute bacteria endocarditis. Maambukizi hayo huanza kati ya siku hadi wiki kadhaa, na mgonjwa huwa na hali mbaya au mahututi. Aina ya pili ni maambukizi yasiyo ya hapo kwa hapo, katika kuta za ndani za moyo ambayo kitaalamu huitwa sub acute bacteria endocarditis. Maambukizi haya huanza kati ya wiki hadi miezi kadhaa, na dalili hutokea pole pole.
Wapenzi wasikilizaji kunavimelea vya aina mbalimbali ambavyo husababisha maambukizi katika kuta za ndani za moyo.

Image result for endocarditis
Valve za moyo zilizoathirika

WATU GANI WAKO KWENYE HATARI
 Je, ni watu gani walio kwenye hatari ya kupata mambukizi katika kuta za ndani za moyo?Watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu ni pamoja na wale mbao walishaugua ugonjwa wa kisukari huko nyuma, akina mama wajawazito, watu wenye matatizo mengine ya valve za moyoyaani (Rheumatic valvular heart disease,) kung'oa jino au meno na vilevile watu waliofanyiwa upasuaji mdogo wa kuwekewa kifaa cha kudhibiti mapigo ya moyo (pacemaker). Inafaa kutambua kuwa kutokuwa na vihatarishi hivyo tulivyovitaja havimaanishi kwamba huwezi kuugua ugonjwa huo.

DALILI ZA TATIZO HILI
Dalili za ugonjwa wa infective endocarditis ni pamoja na kuhisi homa na uchovu wa viungo, maumivu ya kichwa, kikohozi, kupumua kwa shida, maumivu ya kifua, vipele vinavyojulikana kama petechial rash ambavyo husababishwa na kuvuja damu katika mishipa ya ngozi na kusababisha madoa ya rangi nyekundu kwenye ngozi.
Image result for petechial rash

VIPIMO NA UCHUNGUZI
Vipimo vinavyotumika kutambua tatizo la maambukizi katika kuta za ndani ya moyo ni pamoja na blood culture and sensitivity, ambacho ni kipimo cha kuotesha damu ili kuangalia ni vimelea gani vilivyosababisha maambukizi hayo na pia kujua ni dawa gani inaweza kuua vimelea hivyo. Kipimo kingine ni kuangalia wingi wa damu, wingi wa chembe nyeupe ambazo ni kiashiria cha maambukizi. Pia vipimo vingine ni Echocardiogram na ultrasound ya moyo ili kuonyesha kuta za ndani ya moyo na valvu, ufanyaji    kazi wa moyo na kujua kama kuna uoto au vegetations.  Pia inapasa kufanya CT scan ya ubongo hasa kwa wale wanaoonesha dalili za matatizo ya mishipa ya fahamu ili kuangalia kama vimelea au uoto umepelekwa na damu kwenye mishipa ya ubongo,
na pia kipimo cha mkojo kwa ajili ya kuangalia kama kuna protini au chembe chembe nyekundu za damu kwenye hadubini.

MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa wa Infective endocarditis hufanyika kwa utaratibu ufuatao. Baada ya seti tatu hadi tano za damu kuchukuliwa, ni muhimu kuanza na antibaotiki ambazo ni za aina kadhaa, ndani ya saa moja hadi saa moja na nusu na kuendelea na dawa hizo baada ya kupatikana majibu ya damu. Pia inabidi kutumia dozi kubwa ya antibaotiki kwa kipindi cha wiki 6.
Halikadhalika inapaswa kumpa mgonjwa dawa ya Paracetamol au nyinginezo kama hiyo kwa ajili ya kushusha homa na kupunguza maumivu. Pia mgonjwa anapaswa kuangaliwa kwa karibu zaidi.
Sababu zinazopelekea mgonjwa afanyiwe upasuaji ni pale   moyo unaposhindwa kufanya kazi na kutotibika na dawa kirahisi. Au pale
mgonjwa anapopata maambukizi ya Fangasi (histoplasma capsulatum) katika kuta za ndani za moyo na katika valve.

Vilevile pale maambukizi yanapokuwa makali na hali ya mgonjwa kuendelea kuzorota baada ya masaa 72 ya kutumia antibaotiki.
Pia mgonjwa hufanyiwa operesheni iwapo aneurysmyasinus itapasuka au yanapotokea matatizo katika mtiririko wa mfumo wa umeme kwenye moyo unaosababishwa na kuwepo usaha katika mirija ya bawabu za moyo. Halikadhalika panapotokea maambukizi yanayotokana na kugusana kuta za valvu ya aota kwa wagonjwa wenye maradhi hayo.
Wapenzi wasikilizaji  hebu sasa tuangalie jinsi ya kuzuiamaambukizi ya kuta za ndani za moyo na valve. Kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na chama cha madaktari wa moyo cha Marekani, inapasa kuua kimelea chochote kilichopo kwenye damu kabla hakijafika kwenye valve. Ni vyema kujikinga na ugonjwa huo wa moyo kwa kutumia dawa za antibaotiki hasa kwa watu wafuatao:1) wenye valve bandia, 2) waliougua maradhi haya huko nyuma, 3) waliofanyiwa upasuaji wa kuwekewa moyo mwingine, 4) wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, 5) waliong'oa jino au meno na 6) watu waliofanyiwa upasuaji wowote katika mfumo wa upumuaji au upasuaji wowote unaohusu maambukizi katika ngozi, misuli au mifupa.
 
HISTORIA FUPI YA UPASUAJI WA MOYO
Mapinduzi na maendeleo makubwa katika tiba ya upasuaji wa moyo duniani yalianzia mwaka 1944, wakati ilipofanyika kwa mafanikio na kwa mara ya kwanza duniani operesheni ya kwanza ya upasuaji wa moyo katika Hospitali ya John Hopkins nchini Marekani. Operesheni hiyo alifanyiwa mtoto aliyekuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa nalo lililokuwa linasababisha watoto kufa kwa kukosa hewa safi ya oksijeni katika mzunguko wa damu mwilini.
Operesheni hii ilifanywa na dakta Alfred Blalock na wanafunzi wake wa upasuaji akiwemo Ddakta Denton A. Cooley profesa mwanzilishi wa Taasisi ya Moyo ya Texas ya Marekani, ikiwa ni baada ya kuombwa na daktari wa watoto, kujaribu kuokoa maisha ya watoto hao waliokuwa wanakufa bila ya kujua jinsi ya kuwasaidia. Inapaswa kujua kuwa, operesheni hii ya kwanza duniani ilifanikishwa na kijana Mmarekani mweusi Vivien Thomas aliyekuwa msaidizi wa Dakta Blalock katika majaribio ya kisayansi, aliyewezesha kufanyika kwa operesheni hii na akafikia kupewa Udaktari wa Heshima katika Tiba. Kijana huyo alifundisha madaktari wengi wa upasuaji wa moyo waliopitia katika Hospitali hiyo ya John Hopkins.  Kwa ajili hiyo operesheni hii huitwa 'Blalock-Taussing Shunt'. Lakini pia dakta Vivien Thomas  anakumbukwa katika historia ya tiba ya upasuaji wa moyo kwa mchango wake.

Operesheni hii ilikuwa ya kuunganisha baadhi ya mishipa ya damu ili kuwezesha mwili wa mtoto kupata hewa safi. Ingawa operesheni hii ilikuwa si ya kufungua moyo moja kwa moja lakini ilisaidia kutoa mwanga na kujua kwamba inawezekana kuufanyia moyo upasuaji na kurekebisha kasoro zilizomo. Hivyo madaktari na wanasayansi waliendelea na majaribio mbalimbali kwa kutumia wanyama hadi baada ya vita ya Pili ya Dunia ambapo dakta John Gibbon na mkewe Mary Gibbon katika chuo kikuu cha Minnesota mjini Minneapolis nchini Marekani, walipofanikiwa kugundua mashine ya kupitisha damu nje ya moyo iitwayo Heart-Lung machine na kujulikana kwa majina mengine kama Extracorporal Circulation machine au Cardiopulmonary Bypass machine. Hatua hiyo iliwezesha kufanywa operesheni ya kuupasua moyo na kurekebisha kasoro zilizo ndani yake na hapo ndipo mapinduzi na maendeleo makubwa katika tiba yalipoanza kutokea. Hii ilikuwa mwaka 1953.

1 comment:

  1. Dr Itua herbal medicine cure my Prostate Cancer after drinking his herbal medicine for one month and I was totally cured of cancer which all takes my whole family wonder if there could be a herbal doctor so powerful of herbs knowledge and I came to think of it how nature has blessed us with so much healing but we are so blind to see those beautiful things within us.
    Dr Itua is a herbal doctor who resides in west africa. I pay for his herbal items for preparation which he sends to me through courier service then he instructs me on how to drink the herbal medicine for one month and after the one month of treatment I'm now healthy and cured.
    Visit Dr Itua herbal center website on https://drituaherbalcenter.com or email him on drituaherbalcenter@gmail.com also dr itua has herbal medicine for all kinds of disease and infection as a human health concern.

    ReplyDelete