Ulimi wa jiografia au urimi ramani kwa lugha ya kiingereza "geographic tongue" hutokana na ni michomo ya kinga za mwili ambayo huathiri sakafu ya juu au kwenye pembe za kushoto na kulia ya ulimi. Tatizo hili halina madhara yoyote kwa binadamu. Tafiti nyingi zimeonesha ulimi jiografia huambatana na matatizo ya pumu ya Ngozi, licheni planas na soriasisi
Tatizo hili husababisha ulimi uonekane kuwa umefunikwa na mabaka madogo meupe au ya kuchanganyika na rangi ya pinki pamoja na na vipele vidogo ambavyo ni tezi za radha za papilla.
Hata hivyo mabaka hayo mara nyingi huwa hayana tezi za papilla na huonekana kama kisiwa chenye eneo laini jekundu na kingo zake huwa na mwinuko mdogo , unaofanya ulimu kuwa na mwonekano wa ramani.
Dalili
Mwonekano wa ulimi huwa kama kwenye picha iliyo kwenye utangulizi hapo juu pamoja na;
- Kubadilika kwa maeneo ambayo ramani hizi zinatokea, kubadilika kwa umbo la ramani
- Maumivu, kuhisi vibaya kwenye ulimi
- Ulimi kuwaka moto inayoambatana na kula vyakula vyenye viungo na tindikali
- Kutokuwa na dalili kabisa
Kumbuka kama una mabadiliko kwenye ulimi ambayo yamedumu zaidi ya siku 10 onana na daktari wako kwa vipimo na uchunguzi
Visababishi
Hakuna kisababishi kinachosemekana kusababisha tatizo hili,
Kinga
Hakuna kinga ya tatizo hili
Vihatarishi
Tafiti zinaonyesha kuwa vihatarishi yaliyoorodheshwa hapa chini huambatana na kihatarishi cha kupatwa na ulimi wa ramani.
- Kuwa na mtu kwenye familia mwenye tatizo hili
- Ulimi uliopasuka na kuwa na mifereji kwenye sakafu ya ulimi
Madhara
Hakuna madahra ya tatizo hili, mgonjwa hapaswi kuwa na hofu endapo ana tatizo hili kwa sababu haitaaleta tatizo lolote mwilini.
Hata hivyo watu wanaopata tatizo hili huonekana kupatwa na tatizo la wasiwasi kuingana na ulimi wao kubadilika
Matibabu
Endapo umepata na tatizo hili unaweza kuwasilianana daktari wako kwa ushauri na vipimo zaidi
Wasiliana na daktari wa Ngozi kwa ushauri na matibabu sasa kwa kubonyeza link hii:
Karibu tukuhudumie. Bofya link hii https://wa.me/255657282717

No comments
Post a Comment