Friday, 22 May 2020

JE KUPUNGUZA UZITO KWA KIASI KIKUBWA NDANI YA MUDA MFUPI NI SALAMA KIAFYA?



Bila shaka wengi tumekutana na matangazo ya kibiashara mfano "PUNGUZA KILO 10 NDANI YA SIKU 7" N.k
Yawezekana kweli njia zinazotumika zinaweza kufanya hivyo kukata huo uzito kwa siku tajwa, leo katika makala hii napenda tuelezane kama kupunguza uzito kiasi kikubwa kwa muda mfupi ni salama kiafya na je madhara gani yanaweza kumpata mtu anaetekeleza program ya kupungua uzito kwa kasi sana.

Kupunguza uzito kwa kasi sana ni hatari kiafya inaweza kulelekea matatizo ya kiafya na pia inakuweka kwenye hatari ya uzito kurudia tena kuwa juu zaidi ya awali pale unapomaliza program ya kupungua uzito.

NINI MAANA YA KUPUNGUA UZITO KWA KASI.

Kitaalamu inashauliwa kupunguza  kilo 1.5 hadi 2 kwa wiki (siku 7), kupunguza kiwango hiki kwa wiki ni salama kiafya. Ila kupunguza zaidi ya kiasi hicho kwa wiki moja ndio Kupunguza uzito kwa kasi ambayo inaweza kusababisha matatizo ya kiafya.

Tafiti zinaonesha kuwa wale wanaopunguza uzito taratibu kwa kiwango kinachoshauliwa na wataalamu wa afya hawarudii hali ya uzito kuwa juu, ila wale wanaopunguza kwa kasi wengi wao baada ya muda uzito unarudia kuwa juu na saa nyingine juu zaidi ya awali.

Report ya utafiti huo hapa.https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/1615884/

Katika utafiti huo walitumia watu 103 ambao waliwekwa kwenye program ya kupunguza uzito zaidi ya kilo 2 kwa wiki na 97 waliwekwa kwenye program ya kupunguza uzito taratibu kwa kiwango kinachoshauliwa kiafya.

Matokeo: baada ya mwaka wale wote waliokuwa katika program ya kupungua kwa kasi wote walirudia uzito na unene wao wa awali.

MADHARA YA KIAFYA YA KUPUNGUZA UZITO KWA KASI.

Program za diet zinazopunguza mwili kwa kasi sana mara nyingi huwa hazina nishati lishe ya kukidhi mahitaji ya mwili na zinaukosesha mwili virutubisho muhimu.
Zifatazo ni athari za kupunguza uzito kwa kasi sana.

1.Kulegea kwa misuli.
Kupungua uzito kwa kasi kwa kutumia program ya vyakula vyenye nishati lishe
 isiyokidhi mahitaji ya mwili hupelekea upungufu wa protini mwilini hali inayopelekea misuli kulegea.
Ripoti ya utafiti hapa:  https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/1615908/

2.Athari kwenye ngozi.
Kupunguza uzito kwa kasi hupelekea kupunguza hali ya kuvutika kwa ngozi
 (elasticity) na kupelekea ngozi kungeneza makunyanzi,ngozi kutepeta na kwa wengine kupelekea kupata michirizi.kuepuka hili vyema kufata program inayokupunguza taratibu ili ngozi iwe inazoea hali mpya mwili.wakati unapungua nayo inaendana na hayo mabadiliko

3.Kuathiri mfumo wa hormone.
Kupunguza uzito kwa kasi hupelekea kuathiri uzalishwaji wa hormone zinazohusika na michakato ya mwili kuzalisha nguvu (metabolism) mfano hormone ya thyroid.

3.Upungufu wa virutubisho
Unapokula chakula chenye nishati lishe kidogo kupindukia inakuweka kwenye hatari ya kukosa virutubisho muhimu katika mwili na kupelekea matatizo kama
1.kupukutika kwa nywele
2.uchovu kupindukia
3.kinga ya mwili hafifu
4.mifupa isiyo imara.

4.Mawe kwenye mfuko wa nyongo.
Unapotumia chakula chenye nishati lishe kidogo sana hupelekea mwili kutengeneza kemikali ya Ketone ambayo ikizidi inapelekea kutengenezwa kwa mawe kwenye mfuko wa nyongo na kwenye kibofu cha mkojo.
Kujikinga na hali hii fata program inayoshauliwa kiafya na kunywa maji ya kutosha.


Mwisho, ni muhimu sana kufata programu ya kupunguza uzito ambayo haikupeleki kasi sana, fata program ambayo inalenga kupunguza uzito usiozidi kilo 2 ndani ya siku 7 ili kuepuka athari mbali mbali kama zilizotajwa hapo juu. Na kukuwezesha kuishi katika uzito wa malengo yako maisha yako yote.

No comments

Post a Comment