Nini maana ya hydrosalpinx au kujaa maji kwa mirija ya uzazi
Hydrosalpinx ni kitendo cha kuziba kwa mirija ya uzazi (fallopian
tubes) kutokana na kuwepo kwa majimaji katika mirija hii na hivo kuzuia
yai kusafiri kutoka kwenye mifuko ya mayai (oavri) mpaka kwenye mfuko wa
mimba (uterus).
Hydrosalpinx (kujaa maji kwa mirija ya uzazi) husababishwa na nini?
Kwa kiasi kikubwa wataalamu wanasema tatizo hil linatokea endapo
mgonjwa aliwahi kuugua magonjwa yoyote katika njia ya uzazi au magonjwa
ya ngono, uvimbe kwenye kizazi kutokana na kukua kwa tishu laini za
mfuko wa mimba, pia kama mgonjwa aliwahi kufanyiwa upasuajikwenye kizazi
kwa kipindi cha nyumba na hivo kuacha majeraha kwenye mirija ya uzazi
basi hupelekea kupata tatizo hili la Hydrosalpinx. Endelea kusoma zaidi
Makala yetu kupata ufahamu wa tatizo hili ambalo linaweza kuzuia
mwanamke kupata ujauzito na hatimaye ugumba.
Jinsi gani hydrosalpinx inavosababisha ugumba
Tunafahamu kwamba ili mwanamke apate mimba basi ni lazima yai ambalo
lipo tayari yaani limeshavevuka litoke kwenye ovari kisha lisafiri hadi
kwenye mirija ya uzazi ndipo lipate kurutubishwa na mbegu ya kiume,
ovari ndicho kiwanda cha mwanamke cha kutengeneza mayai. Kitendo hichi
cha urutubishaji hutokea siku ya 14 kwenye mzunguko wa hedhi. Kwahivo
kama mrija umeziba manake yai halitaweza kusafiri na urutubishaji
hautafanyika hivo mimba haitaweza kutungwa.
Swali: vipi kama mrija mmoja umeziba na mwingine uko vizuri je kuna uwezekano wa mimba kutungwa?
Kuna mrija miwli ya uzazi, mrija mmoja kutoka kwenye kila mfuko wa
mayai(ovari) hivo kila mwezi mfuko mmoja wa mayai hutoa yai moja ili
liweze kurutubishwa na mbegu ya kiume, na mara chache hutokea mifuko
yote kutoa yai moja ndani ya mwezi mmoja. Hivo ni wazi kwamba kama mrija
mmoja umeziba na mwingine upo vizuri basi yai litasafiri vizuri,
urutubishaji utafanyika na mimba itatungwa. Lakini athari zingine zaa
mrija wa kwanza kuziba itaendelea kuwepo, wanasayansi wamebaini kwamba
kuziba kwa mrija mmoja kunaweza kusababishakutiririsha maji kuelekea
kwenye mfuko wa mimba na hivo kuathiri kiumbe kipya.
Matibabu yanayopatikana kwa kuziba kwa mirija ya uzazi.
Kuna aina nyingi za matibabu yanayotolewa kwa kuziba kwa mrija ya
uzazi katika mahospitali. Dactari wako anatakiwa akupe maelezo ya kina
ni tiba gani inafaa zaidi kutokana na tatizo lako. Tiba hizi ni kama
inavoelezwa hapa chini
-
Tiba kwa upasuaji kuondoa mrija ulioathirika
Madi wanaweza kupendekeza kufanya upasuaji na hivo kuondoa mrija
ulioziba ama kujaa maji, kitaalamu tiba hii huitwa laparoscopic
salpingectomy. Njia hii huweza kuhatarisha ufanyaji kazi wa ovari kwa
kukosa damu kutokana na kwamba mrija wote hukatwa na kuondolewa kabisa.
-
Sclerotherapy (kunyonya maji yaliyoziba kwenye mrija wa uzazi:
Tiba hii hufanyika kwa ultrasound na yaweza kuwa tiba salama zaidi
kuliko kukata mrija wa uzazi, katika tiba hii tube nyembamba huingizwa
kwenye mrija ulioathirika na hivo kunyonya maji yaliyopo.
-
Tiba ya upasuaji mdogo kwenye eneo lilloziba kwenye mrija wa uzazi:
Upasuaji huu hulenga eneo husika kwenye mrija wa uzazi. Hivo eneo
hili hupasuliwa na maji kusafishwa na kisha kushonwa tena ili kuzuia
maji maji kuvia kwenye mfuko wa mimba ama uterus.
No comments
Post a Comment