Kujaa Maji kwa Mirija ya Uzazi (hydrosalpinx)

Nini maana ya hydrosalpinx au kujaa maji kwa mirija ya uzazi

Hydrosalpinx ni kitendo cha kuziba kwa mirija ya uzazi (fallopian tubes) kutokana na kuwepo kwa majimaji katika mirija hii na hivo kuzuia yai kusafiri kutoka kwenye mifuko ya mayai (oavri) mpaka kwenye mfuko wa mimba (uterus).

Hydrosalpinx (kujaa maji kwa mirija ya uzazi) husababishwa na nini?

Kwa kiasi kikubwa wataalamu wanasema tatizo hil linatokea endapo mgonjwa aliwahi kuugua magonjwa yoyote  katika njia ya uzazi au magonjwa ya ngono, uvimbe kwenye kizazi kutokana na kukua kwa tishu laini za mfuko wa mimba, pia kama mgonjwa aliwahi kufanyiwa upasuajikwenye kizazi kwa kipindi cha nyumba na hivo kuacha majeraha kwenye mirija ya uzazi basi hupelekea kupata tatizo hili la Hydrosalpinx. Endelea kusoma zaidi Makala yetu kupata ufahamu wa tatizo hili ambalo linaweza kuzuia mwanamke kupata ujauzito na hatimaye ugumba.

Jinsi gani hydrosalpinx inavosababisha ugumba

Tunafahamu kwamba ili mwanamke apate mimba basi ni lazima yai ambalo lipo tayari yaani limeshavevuka litoke kwenye ovari kisha lisafiri hadi kwenye  mirija ya uzazi ndipo lipate kurutubishwa na mbegu ya kiume, ovari ndicho kiwanda cha mwanamke cha kutengeneza mayai. Kitendo hichi cha urutubishaji hutokea siku ya 14 kwenye mzunguko wa hedhi. Kwahivo kama mrija umeziba manake yai halitaweza kusafiri na urutubishaji hautafanyika hivo mimba haitaweza kutungwa.

Swali: vipi kama mrija mmoja umeziba na mwingine uko vizuri je kuna uwezekano wa mimba kutungwa?

Kuna mrija miwli ya uzazi, mrija mmoja kutoka kwenye kila mfuko wa mayai(ovari) hivo kila mwezi mfuko mmoja wa mayai hutoa yai moja ili liweze kurutubishwa na mbegu ya kiume, na mara chache hutokea mifuko yote kutoa yai moja ndani ya mwezi mmoja. Hivo ni wazi kwamba kama mrija mmoja umeziba na mwingine upo vizuri basi yai litasafiri vizuri, urutubishaji utafanyika na  mimba itatungwa. Lakini athari zingine zaa mrija wa kwanza kuziba itaendelea kuwepo, wanasayansi wamebaini kwamba kuziba kwa mrija mmoja kunaweza kusababishakutiririsha maji kuelekea kwenye mfuko wa mimba na hivo kuathiri kiumbe kipya.

Matibabu yanayopatikana kwa kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kuna aina nyingi za matibabu yanayotolewa kwa kuziba kwa mrija ya uzazi katika mahospitali. Dactari wako anatakiwa akupe maelezo ya kina ni tiba gani inafaa zaidi kutokana na tatizo lako. Tiba hizi ni kama inavoelezwa hapa chini
  1. Tiba kwa upasuaji kuondoa mrija ulioathirika
Madi wanaweza kupendekeza kufanya upasuaji na hivo kuondoa mrija ulioziba ama kujaa maji, kitaalamu tiba hii huitwa laparoscopic salpingectomy. Njia hii huweza kuhatarisha ufanyaji kazi wa ovari kwa kukosa damu kutokana na kwamba mrija wote hukatwa na kuondolewa kabisa.
  1. Sclerotherapy (kunyonya maji yaliyoziba kwenye mrija wa uzazi:
Tiba hii hufanyika kwa ultrasound na yaweza kuwa tiba salama  zaidi kuliko kukata mrija wa uzazi, katika tiba hii tube nyembamba huingizwa kwenye mrija ulioathirika na hivo kunyonya maji yaliyopo.
  1. Tiba ya upasuaji mdogo kwenye eneo lilloziba kwenye mrija wa uzazi:
Upasuaji huu hulenga eneo husika kwenye mrija wa uzazi. Hivo eneo hili hupasuliwa na maji kusafishwa na kisha kushonwa tena ili kuzuia maji maji kuvia kwenye mfuko wa mimba ama uterus.

No comments