Friday, 6 September 2019

FOLIC ACID KIPINDI CHA UJAUZITO.LINI UNAPASWA KUANZA KUMEZA?

Nimesukumwa kuandika Makala hii na hali iliyopo sasa mama zetu wanameza dawa hizi kutokana na ushauri wanaopewa ili kuongeza na damu na kuwakinga wasizae watoto wenye ulemavu mfano mdomo sungura,mgongo wazi nk.
Katika hali ya kusikitisha mama zetu wamekua wakimeza dawa hizi katika njia isiyo sahihi.Nitakuelezea kwa nini.

JE NI KATIKA UMRI GANI WA MIMBA UNAPASWA KUANZA KUMEZA FOLIC ACID.
Kikawaida viungo vya mwili wa mtoto huwa vinatengenezwa ndani ya miezi mitatu ya mwanzo, Ubongo na uti wa mgongo na mapafu hivi hutengenezwa kati ya siku ya 20 hadi 25. Matatizo katika utengenezwaji wa ubongo na viungo vingine hutokea ndani ya siku 28 za ujauzito.Na kipindi hiki mjamzito anakua bado hajafahamu kama ni mjamzito wengi wao uanza kujigundua baada ya mwezi mmoja.Mama wengi huanza clinic wakiwa na umri wa mimba wakiwa na miez mitatu kuendelea na hapo ndipo wanaanza kupewa folic acid.Kwa hiyo kipindi hiki tayari kama kuna matatizo yamesatokea na folic acid hazimsaidii tena labda kwenye swala la kuongeza damu.

USHAURI.
Kutokana na matatizo haya kutokea kabla ata mtu hajajigundua ni mjamzito ni muhimu wamama wanaotafuta watoto kuanza kutumia folic acid au kupata folic acid miezi mitatu kabla ya ujauzito.Yaani pale unapoamu kuwa upo tayari kubeba mimba unaanza folic acid au kula vyakula vyenye folic acid kwa wingi.
Kutokana na mimba nyingine kuja bila kupangwa basi mwanmke yyote alio kwenye umri wa kupata mimba anapaswa kupata au kula vyakula vyenye folic acid ya kutosha.

FOLIC ACID NI NINI?
Folic acid ni mkusanyiko wa vitamins(B12,B9,C,folate n.k)unaotoka kwenye matunda na vyakula unaotengenezwa mfumo wa supplement(vidonge) vinavyosaidia mwili kuzalisha damu ya kutosha na kumpa kinga mama mjamzito ili aweze kuzaa mtoto asie na ulemavu.Folic acid inaweza kutumiwa hata na mtu wa kawaida kutibu mapungufu ya damu na kuepusha maradhi mengineo kama cancer ,matatizo ya moyo na ugonjwa wa kupooza.

Kiasi gani mama anatakiwa kutumia folic acid
Mama mwenye mimba anatakiwa atumie kiwango cha 400micrograms
Mama anaetafuta mimba anatumia kiasi cha 400micrograms miezi 3 kabla
5Mg kwa mama alieshawahi kuzaa mtoto mwenye matatizo hayo,ni vizuri ukawahi kutumia mapema kuna uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye hayo matatizo tena vizuri kunywa mapema ili umwepushe
Mama mwenye uzito mkubwa au diabetes nae ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye mapungufu, vizuri wakatumia 50mg za folic acid

Madhara ya upungufu ya folic acid kwa mama mjazito
Mama na mtoto kukosa ya damu ( anaemia)
Kuadhiriwa kwa ubongo na uti wa mgongo wa mtoto
Mtoto kuzaliwa mgongo wazi / kuzaliwa na uvimbe mkubwa mgongoni
Mtoto kutozaliwa na kichwa kikubwa kuzidi umri wake na kumwelemea,
Mtoto kuzaliwa mdomo juu ya lips (panakuwa hapafungi)
Mtoto kuzaliwa na kichwa chenye mapungufu kinakuwa na umbo kama la chura
Mimba kuharibika(Miscarriage)
Mtoto kuzaliwa njiti
Kuleta ulemavu wa miguu

Vyakula vyenye vyanzo vya folic acid
Mama anaweza kaputa folic acid kupitia vyakula na matunda kama
Machungwa au ndimu
Parachichi
Papai
Nyanya
Bamia
Viazi vitamu
Dagaa
Maharagwe meusi/ njegere
Mayai ya kuchemsha
Brown rice n brown bread
Pasta / tambi ndefu
Broccoli
Spinach
Maharage mabichi
Beetroot

No comments

Post a Comment