Nimesukumwa kuandika Makala hii na hali iliyopo sasa mama zetu
wanameza dawa hizi kutokana na ushauri wanaopewa ili kuongeza na damu na
kuwakinga wasizae watoto wenye ulemavu mfano mdomo sungura,mgongo
wazi nk.
Katika hali ya kusikitisha mama zetu wamekua wakimeza dawa hizi katika njia isiyo sahihi.Nitakuelezea kwa nini.
JE NI KATIKA UMRI GANI WA MIMBA UNAPASWA KUANZA KUMEZA FOLIC ACID.
Kikawaida viungo vya mwili wa mtoto huwa vinatengenezwa ndani ya miezi
mitatu ya mwanzo, Ubongo na uti wa mgongo na mapafu hivi hutengenezwa
kati ya siku ya 20 hadi 25. Matatizo katika utengenezwaji wa ubongo na
viungo vingine hutokea ndani ya siku 28 za ujauzito.Na kipindi hiki
mjamzito anakua bado hajafahamu kama ni mjamzito wengi wao uanza
kujigundua baada ya mwezi mmoja.Mama wengi huanza clinic wakiwa na umri
wa mimba wakiwa na miez mitatu kuendelea na hapo ndipo wanaanza kupewa
folic acid.Kwa hiyo kipindi hiki tayari kama kuna matatizo yamesatokea
na folic acid hazimsaidii tena labda kwenye swala la kuongeza damu.
USHAURI.
Kutokana na matatizo haya kutokea kabla ata mtu hajajigundua ni
mjamzito ni muhimu wamama wanaotafuta watoto kuanza kutumia folic acid
au kupata folic acid miezi mitatu kabla ya ujauzito.Yaani pale unapoamu
kuwa upo tayari kubeba mimba unaanza folic acid au kula vyakula vyenye
folic acid kwa wingi.
Kutokana na mimba nyingine kuja bila kupangwa
basi mwanmke yyote alio kwenye umri wa kupata mimba anapaswa kupata au
kula vyakula vyenye folic acid ya kutosha.
FOLIC ACID NI NINI?
Folic acid ni mkusanyiko wa vitamins(B12,B9,C,folate n.k)unaotoka
kwenye matunda na vyakula unaotengenezwa mfumo wa supplement(vidonge)
vinavyosaidia mwili kuzalisha damu ya kutosha na kumpa kinga mama
mjamzito ili aweze kuzaa mtoto asie na ulemavu.Folic acid inaweza
kutumiwa hata na mtu wa kawaida kutibu mapungufu ya damu na kuepusha
maradhi mengineo kama cancer ,matatizo ya moyo na ugonjwa wa kupooza.
Kiasi gani mama anatakiwa kutumia folic acid
Mama mwenye mimba anatakiwa atumie kiwango
cha 400micrograms
Mama anaetafuta mimba anatumia kiasi cha 400micrograms miezi 3 kabla
5Mg kwa mama alieshawahi kuzaa mtoto mwenye matatizo hayo,ni vizuri
ukawahi kutumia mapema kuna uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye hayo
matatizo tena vizuri kunywa mapema ili umwepushe
Mama mwenye uzito mkubwa au diabetes nae ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye mapungufu, vizuri wakatumia 50mg za folic acid
Madhara ya upungufu ya folic acid kwa mama mjazito
Mama na mtoto kukosa ya damu ( anaemia)
Kuadhiriwa kwa ubongo na uti wa mgongo wa mtoto
Mtoto kuzaliwa mgongo wazi / kuzaliwa na uvimbe mkubwa mgongoni
Mtoto kutozaliwa na kichwa kikubwa kuzidi umri wake na kumwelemea,
Mtoto kuzaliwa mdomo juu ya lips (panakuwa hapafungi)
Mtoto kuzaliwa na kichwa chenye mapungufu kinakuwa na umbo kama la chura
Mimba kuharibika(Miscarriage)
Mtoto kuzaliwa njiti
Kuleta ulemavu wa miguu
Vyakula vyenye vyanzo vya folic acid
Mama anaweza kaputa folic acid kupitia vyakula na matunda kama
Machungwa au ndimu
Parachichi
Papai
Nyanya
Bamia
Viazi vitamu
Dagaa
Maharagwe meusi/ njegere
Mayai ya kuchemsha
Brown rice n brown bread
Pasta / tambi ndefu
Broccoli
Spinach
Maharage mabichi
Beetroot


No comments