FAHAMU ZAIDI KUHUSU MINYOO INAYOENEZWA KWA KULA NYAMA YA NGURUWE







TEGU NI NINI?
Tegu ni ugonjwa wa minyoo ambao ushambulia wanyama na binadamu na haswa unasababishwa na kula nyama iliyo beba minyoo wa tegu au kula chakula chenye mayai yake.
Miongoni mwa minyoo ambayo inasababisha tegu  ni minyoo ya nyama ya ng’ombe (Taenia_sagina), minyoo ya nyama ya nguruwe (Taenia solium), minyoo ya mbwa (Ochinococcus_granulosis).
Leo tutajikita kuongelea ugonjwa wa TEGU utokanao na nguruwe inayoitwa Taenia solium ambayo ina urefu wa takribani mita 2 mpaka mita 50  ambayo husabisha Tegu kwa binadamu kutoka kwa nguruwe, pia siyo tu kusabisha magonjwa kwa binadamu lakini pia ikiwemo kushusha uchumi kwa vile nyama ya nguruwe mwenye ugonjwa hutupwa yote.

Ugonjwa huu upo sehemu mbalimbali za Tanzania kama maeneo ya Iringa, Mbulu, Morogoro, Mbeya, sehemu nyingine nyingi na karibu maeneo yote duniani.
Husababisha ugonjwa unaojulikana kitaamu kama Cysticercosis na hii inatokana na kuwepo kwa viuvimbe vingi ndani ya viungo vya mwili vilivyojaa majimaji.


UGONJWA    WA     TEGU UNAENEZWAJE?
Ugonjwa husabishwa na lava wa tegu au mayai yake.
  • Kwa nguruwe
Nguruwe hupata endapo wakila chakula au maji machafu ambayo yamechanganyikana na kinyesi cha binadamu chenye mayai ya tegu.


Kwa binadamu
  • Binadamu anaupata ugonjwa huu kwa kula nyama ya nguruwe ambayo ina ugonjwa huu (adult Taenia solium) na hakikupikwa vizuri, bila kupikwa kabisa au bila kuiva vizuri. Kwa kitaalamu ugonjwa huu huitwa Taeniosis
  • Binadamu anaupata ugonjwa huu pia kupitia chakula, maji au mboga za majani amabazo zina mayai ya tegu kutoka katika kinyesi cha biandamu au nguruwe. Kwa kitaalamu ugonjwa huu huitwa  cysticercosis

JE NI NJIA/ TABIA ZIPI UHATARISHA NA KUONGEZA BINADAMU KUPATA UGONJWA HUU?
  • Kutokuwa na choo au kuwa na matumizi hafifu ya choo (usafi wa choo na mikono)
  • Kutozingatia usafi binafsi na wamazingira (kujisaidia porini)
  • Kuwaachia nguruwe na kuzagaa au kuzurura mtaani kujitafutia chakula
  • Kunywa maji amboyo siyo safi na salama
  • Kula nyama ya nguruwe ambayo haija pikwa au kuiza vizuri.
DALILI AU ISHARA
kwa Binadamu
  • Uvimbe chini ya ulimi unao uma ukibonyezwa.
  • Tumbo kuuma na kukosa hamu ya kula
  • kuharisha na mara nyingine kufunga choo na kupungua uzito
  • kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kuchanganyika, kuyumbayumba,kifafa na kasha kifo kwasababu lava huenda kwenye mfumo wa fahamu wa binadamu na hasa maeneo ya ubongo
  • kupatwa na vijiuvimbe ambavyo havionyeshi dalili zozote kwenye misuli katika maeneo mbalimbali ya mwili.
  • kuchoka magoti na viungo vingine wakati wa kupanda mlima na mwili kukosa nguvu
  • Mda mwingine husababisha kidole tumbo na kupatwa na vijiuvimbe kwenye macho.
 
Kwa nguruwe
  • Kudhoofika kwa afya na kushindwa kula kwa ajili ya maumivu ya chini ya ulimi.
  • Kuwepo kwa malengelenge kwenye sehemu ya haja, mashavuni, mabegani na ulimi, na pia hutoa maji yenye rangi ya kawawia na lava huonekana kama nukta nyeupe akishwa chinjwa.
  • Pia uvimbe huonekana kwenye ini, bandama, ubongo na tezi akisha chinjwa.

Taenia solium under the tongue    Taenia solium in the muscles
JE NI KWA JINSI GANI UNAWEZA KUTAMBUA UGONJWA WA TEGU?
Mara zote huwa tunatumia dalili ambazo baadhi yake zimetajwa hapo juu lakin haitoshi kusema kuwa ni tegu kwa sababu kuna magonjwa mengi mengine pia huonyesha kama hizo. Kwahiyo tunajumuisha dalili tajwa hapo juu , tabia hatarishi za ugonjwa na majibu ya kitaalamu kutoka maabara.
Katika maabara uchunguzi wa kinyesi cha mwanadamu kuangalia uwepo wa mayai ya tegu kwa kutumia darubini na pia larva wakiwa kwenye ubongo wa binadamu njia za kitaalamu zaidi hutumika kama MRI au CT brain scan.
MRI ndicho kipimo chenye uhakika kwani kinauwezo wa kuonyesha hatua ya uvimbe, mahali ulipo na mabadiliko yake.
JE  UNAJUA UGONJWA HUU UNATIBIKA ?
Dawa zipo na zina uwezo wa kuua tegu wakubwa walio kwenye misuli na kwa wadogo huwa ngumu kwa kuwa huwa ndani ya viuvimbe veyenye ngozi.
  • Kwa nguruwe:
Nguruwe wenye dalili ya ugonjwa huu inashauriwa  watibiwe kwa kutumia Oxfendazole (dawa ya minyoo ) ambayo inapendekezwa kutumika kuua tegu na lava bila kusahau ushauri wa mtaalamu wa mifugo ni muhimu.
  • Kwa binadamu:
Kwa binadamu kuna changamoto ya kutibu ugonjwa huu. Ugonjwa huu ukiwa nje ya mfumo wa fahamu huwa rahisi kutibika kwa matibabu maalamu kwa dawa za minyoo.
Niclosamida (yomesan) inaweza tumika, dichlorophen(antiphen) au quinacrine(mepacrine, atebrine) kwa kufuata maagizo kwa uangalifu yatakayotolewa na mataalamu wa afya. Lakini lava wakiwa kwenye mfumo wa fahamu upasuaji ili kuondoa uvimbe hushauriwa ufanyike.
NI NJIA ZIPI ZITUMIKE ILI KUZUIA UGONJWA HUU WA HATARI?
Mwenye jukumu, uwezo na  mchango mkubwa wa kutokomeza ugonjwa huu ni binadamu. Kwahivyo elimu ya kutosha kupambana na huu ugonjwa inahitajika kwa kiasi kikubwa sana. Kulingana na gharama kubwa za vipimo na ugumu wamatibabu kwa binadamu ni bora kujikinga na ugonjwa huu.
Nguruwe:
  • Hakikisha chakula na maji wanayopewa nguruwe yawe ni masafi​ na salama
  • Nguruwe wafungiwe ndani na wasiruhusiwe kutembea nje ya banda.
  • Hakikisha nguruwe wanapata dawa za magonjwa ya minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu
  • Nguruwe wakaguliwe na wataalamu kabla na baada ya kuwachinja na wale wote watakaopatikana na ugonjwa nyama zao ziharibiwe.​
  • Hakikisha kuwa nyama ya nguruwe imeiva vizuri na pia hakuna sehemu mbichi katika nyama ya kuchoma
Mwanadamu:
  • Hakikisha matuzi ya choo nyumbani yanafanyika ipasavyo na epukuka kujisaidia sehemu isiyo na choo.​
  • Hakikisha unapima choo chako angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu ili kujua hali yako kwa magonjwa ya minyoo​
  • Tumia dawa za minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu ili kutibu magonjwa ya minyoo ambayo hayajaanza kuonyesha dalili.
MUHIMU:
Albendazole au Praziquantel  zinatakiwa kutumika kutibu ugonjwa huu na kwenye eneo lina watu wengi wenye minyoo hii utibuji wa pamoja utasaidia kuzuia mzuko wa maisha ya tegu.

No comments