Figo ni miongoni mwa viungo
muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. Kwa kawaida,
mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale ya
maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya
mbavu za chini.
Kazi za figo
Kazi kuu za figo ni
kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu kadhaa katika damu na hivyo kusaidia
katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini.
Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini
na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya
madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje
uchafu usiohitajika.
Kazi nyingine za
mafigo ni
·
Kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu mbalimbali katika damu pamoja na
kiasi cha maji katika mwili
·
Husaidia kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana
katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu.
·
Husaidia uzalishaji wa vitamini D
·
Husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini
(blood pressure)
Utengenezaji wa
mkojo
Kwa kawaida damu
inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa
uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika mwilini. Kitendo hiki cha
utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu zifuatazo;
·
Hatua ya kwanza ni uchujaji. Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na
kupita kwenye glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo
limeundwa na mishipa mingi midogo ya damu iliyojizungusha pamoja. Vitu mbali
mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu inayopita kwenye vimishipa hivi
na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa kwa ajili ya uchujaji
zaidi.
·
Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya vitu
vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu
kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.
·
Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo, husafiri
kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo kama ureta.
Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye mrija waurethra.
Figo kushindwa
kufanya kazi (Renal Failure/ Kidney Failure)
Kushindwa kufanya
kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au figo lote litapoteza uwezo wake
wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na kutengeneza mkojo. Kitendo hiki
husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu kadhaa katika damu ambazo ni
hatari kwa afya ya mhusika.
Aina za figo
kushindwa kufanya kazi
Figo kushindwa
kufanya kazi kumeganyika katika makundi yafuatayo
·
Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF) au
Acute Kidney Failure (AKF).
·
Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency)
·
Tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure)
Figo kushindwa
kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF)
Hii ni hali
inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku chini ya 14, na
kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika damu. Hali hii
huwapata karibu asilimia 5% ya wagonjwa waliolazwa hospitali kwa sababu ya
matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa wagonjwa mahututi na wale
wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa ICU.
Katika makala hii
tutatumia zaidi kifupisho cha ARF.
Visababishi na aina
za ARF
Visababishi (au
aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu:
·
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal
causes/failure)
·
Matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu
au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure)
·
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal
causes/failure)
Matatizo
yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal
causes/failure)
Aina hii hutokea kwa
takribani asilimia 60 mpaka 70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu
ya kutosha kwa ajili ya kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake
ipasavyo. Mambo yanayoweza kusababisha prerenal failure ni
pamoja na:
·
Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi,
kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia)
·
Kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu
ya:
o Kushuka kwa ghafla
kwa shinikizo la
damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji
mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika mfumo wa
damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha
shinikizo la damu
o Kuziba au kusinyaa
kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo
o Moyo kushindwa
kufanya kazi (heart failure) au shambulio la
moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwashinikizo la
damu
o Ini kushindwa kufanya
kazi (liver failure) kunakoweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa
homoni zinazoathiri shinikizo la damu pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye
figo.
Mwanzoni kabisa mwa
pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote inayotokea kwenye figo, na mara
nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa
na kushughulikiwa ipasavyo.
Matatizo ndani ya
figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo
(Renal causes/failure)
Mambo
yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu asilimia 25 mpaka 40 ya
vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi hili hujumuisha vile
vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na seli za figo
zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.
Visababishi hivyo ni
pamoja na:
·
Magonjwa katika mishipa ya damu
·
Kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika
figo
·
Ajali/Kuharibika kwa tishu na seli za figo
·
Magonjwa ya mzio katika glomeruli na figo kwa ujumla (glomerulonephritis).
Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi (infection) ya
bacteria jamii ya streptococci.
·
Magonjwa ya mzio katika nyama za figo (acute interstitial nepthritis).
Mambo yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa
kama vile Aspirin, Ibuprofen (Brufen), baadhi ya antibiotics, na baadhi ya dawa
za kutoa maji mwilini (antidiuretics); magonjwa kama vile saratani ya damu
(leukemia), lupus na lymphoma. Magonjwa ya mzio katika nyama za figo
husababisha madhara katika seli zinazohusika na uchujaji na ufynzaji wa chumvi
na maji.
·
Magonjwa ya ukosefu wa damu katika mirija ya figo (acute tubular
necrosis) ambayo hufanya seli na tishu za mirija hii kufa na hivyo mirija
kushindwa kufyonza chumvi na maji kuyarudisha mwilini. Mambo yanayosababisha
hali hii ni pamoja na shock (upungufu wa damu kuingia kwenye figo), matumizi ya
madawa kama vile baadhi ya antibiotiki, sumu, dawa zinazotumika viwandani na
kwenye x-rays na baadhi ya madawa yanayotumika kutibu saratani.
Matatizo yanayoathiri
mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/failure)
Mambo
yanayosababisha hali hii huchangia kati ya silimia 5 mpaka 10 ya vyanzo vyote
vya ARF. Postrenal failure wakati mwingine huitwa pia obstructive renal
failure kwa sababu husababishwa na mambo yanayozuia utoaji wa mkojo
nje ya figo.
Kuziba kwa ureta
moja ama zote mbili kunaweza kusababishwa na:
·
Saratani ya viungo vya njia ya mkojo au viungo vilivyo karibu na njia ya
mkojo kiasi cha kuzuia mkojo kutoka nje ya figo
·
Matumizi ya baadhi ya madawa
Kuziba kwa njia ya
mkojo katika eneo la kibofu cha mkojo kunaweza kutokana na:
·
Kuvimba kwa tezi
dume (hii ni kwa wanaume)
·
Kuwepo kwa damu iliyoganda katika kibofu
·
Matatizo ya mfumo wa fahamu yanayoathiri utendaji kazi wa kibofu cha
mkojo
Tafsiri nyingine ya
ARF
Wagonjwa wa ARF
wanaweza kupata mkojo kidogo sana au wasipate kabisa., au wanaweza kuwa na
ongezeko la creatinine kwa kasi ya kutisha au kwa kasi ndogo sana. Hali hizi
zinaweza pia kutumika kutoa tafsiri nyingine ya maana ya ARF.
Mtu anayetoa kiasi
cha mkojo chini ya 400mL kwa siku hujulikana kama ana oliguria, na huchukuliwa
kuwa ana hali mbaya ya kutoweza kupona.
Mtu anayetoa mkojo
chini ya 100mLkwa siku husemwa ana Anuria, ambayo kama imetokea ghafla,
huashiria kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mirija inayotoa mkojo kwenye figo
zote mbili, na mara niyingi hali hii ni ya hatari zaidi. Tafsiri hii husaidia
sana katika kuamua aina ya matibabu na muda wa kumpatia mgonjwa matibabu ili
kuepusha madhara zaidi yanayoweza kumpata.
Dalili za ARF
Katika hatua za
mwanzo mwanzo, baadhi ya waathirika wanaweza wasioneshe dalili zozote za tatizo
hili. Dalili ni kama
·
Kupungua kwa uzalishaji mkojo
·
Kuvimba mwili
·
Kupoteza umakini
·
kuchanganyikiwa
·
Uchovu
·
Kulegea mwili
·
Kichefuchefu na kutapika
·
Kuharisha
·
Maumivu ya tumbo
·
Kuhisi ladha ya chuma na uchachu mdomoni
·
Na katika hatua za mwisho kabisa, mgonjwa anaweza kupata degedege na
hatimaye kupoteza fahamu (coma).
Vipimo na uchunguzi
Kama ilivyoainishwa
hapo juu kuwa baadhi ya wagonjwa wanaweza wasiwe na dalili zozote za tatizo
hili. Hata wale wenye kuonesha dalili, zinaweza zisiwe mahsusi (non-specific).
Uchunguzi wa mwili unaweza usioneshe tatizo lolote lile, au kukawa na dalili
chache sana ambazo zinaweza zisimsaidie sana daktari kufikia uamuzi.
Baadhi ya vipimo
vinavyoweza kugundua uwepo wa ARF ni pamoja na
·
Kipimo cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia
kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu. Aidha
husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika damu.
·
Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood
electrolytes)
·
Uchunguzi wa damu (Full Blood Picture): Husaidia kuonesha uwepo wa
maambukizi ya bacteria na/au upungufu wa damu mwilini (anaemia)
·
Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24
·
Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha
electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.
·
Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo
·
Renal biopsy.
Matibabu ya ARF
Matibabu ya ARF
hutegemea kwanza chanzo chake na pili ukubwa wa tatizo. Kujua chanzo cha tatizo
husaidia kufahamu ni aina gani ya matibabu yanayohitajika wakati kufahamu
ukubwa wa tatizo huathiri uchaguzi wa aina ya matibabu na hata hitaji la
kufanya dialysis. Hata hivyo inashauriwa sana kumpeleka mgonjwa kwa daktari
bingwa wa magonjwa ya figo (nephrologist) kwa matibabu zaidi.
Kulingana na chanzo
cha ARF, baadhi ya matibabu yanayoweza kufanyika, hutolewa yakiwa na lengo la:
·
Kurekebisha kiasi cha upotevu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa i.v
fluids pamoja kurekebisha kiasi cha madini (electrolytes) kilichopotea
·
Kupunguza au kuzuia ongezeko la maji kwa wagonjwa ambao figo zao
zimeshindwa kabisa kutoa maji nje ya mwili
·
Kuongeza uwezo wa moyo kufanya kazi vizuri au kuongeza shinikizo la
damu husaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenda kwenye
figo
·
Kurekebisha kiasi cha madini mwilini kitendo ambacho husaidia mwili
kufanya kazi zake vema
Dialysis
Iwapo pamoja na
matibabu hayo, figo za mgonjwa zinaendelea kudorora, mgonjwa hana budi
kufanyiwa dialysis. Dialysis ni kitendo cha kutoa uchafu na maji
yasiyohitajika katika damu. Kitendo hiki hufanywa kwa kupitia mishipa ya damu
iliyo chini ya ngozi (hemodialysis) au kwa kupitia tumboni (peritoneal
dialysis). Katika hemodialysis mirija hii huunganiswa kwenye mashine ambayo
hufanya kazi kama figo. Damu kutoka kwa mgonjwa huingia katika mashine kisha
huchujwa ili kuondoa sumu, uchafu pamoja na maji yasiyohitajika kabla ya
kurejeshwa tena mwilini.
Kitendo hiki
hufanyika angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki, na kwa kiasi fulani ni ghali
na si watu wote wa kipato cha chini wanaoweza kumudu gharama zake.
Katika peritoneal
dialysis, uchafu pamoja na maji kutoka katika mzunguko wa damu huingia katika
nafasi inayotenganisha tumbo na utando wake (peritoneal space), huchujwa
kwenye utando huo kisha hutolewa kupitia sindano maalum (catheter ) iliyowekwa
juu ya ngozi na kuingia ndani ya tumbo (peritoneal cavity).
Matarajio
Wagonjwa wengi wenye
ARF hupona bila hata kuhitaji dialysis mara tu chanzo cha tatizo
kinapogundulika na kushughuikiwa mapema. Hata hivyo wakati mwingine, pamoja na
matibabu, baadhi ya figo hushindwa kurudia kufanya kazi kwa ufanisi wake wa
awali. Watu kama hawa hawa wanahitaji kufuatiliwa kwa ukaribu na umakini
mkubwa.
Kinga ya ARF
Inashauriwa
1. kufanya uchunguzi wa
figo walau mara moja kila mwaka. Hii husaidia kuchunguza utendaji wa figo na
hivyo kuepuka madhara kabla hayajatokea.
1. Kunywa maji kwa wingi
ili kuyafanya mafigo yatende kazi zake kwa ufanisi.
1. Kuepuka matumizi ya
vitu ama madawa yanayoweza kuathiri nyama, seli au tishu za figo. Ni vema
kutumia dawa pale tu unaposhauriwa na daktari.
1. Watu wenye hatari ya
kupata tatizo sugu la kushindwa kufanya kazi kwa figo (Chronic Renal Failure)
wanashauriwa kufanya vipimo na cuhunguzi mara kwa mara
1. Muone mtaalamu wa
afya mara tu uonapo dalili za kuwepo kwa shida katika kukojoa au uonapo damu
katika


No comments
Post a Comment