Kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki kutokana na utumizi wa tumbako. Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza uraibu
huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu
hufupisha maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Sababu ni kuwa sigara ina
kemikali zaidi ya 4,000 ambazo zina uwezo wa kudhhuru afya ya binadamu.
Madhara yanayosababishwa na uvutaji sigara ni mengi na yamesambaa
mwilini kote. Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na utumiaji
wa tumbako.
Nimejaribu kukuelezea kupitia picha hii
1.Kung’oka kwa nywele
Uvutaji sigara hudhoofisha kinga ya mwili na kisha kudhuru mizizi ya nywele . hii husababisha kung’oka kwa nywele mapema.
2.Magonjwa ya macho
Wavutaji
sigara hupata magonjwa ya macho mara nyingi kuliko wasiovuta. Sehemu ya
macho inayopitisha mwangaza inaweza kufichwa kama vile wingu
linavyoficha jua(yaani kwa ikimombo) na kusababisha upofu. Ugonjwa huu
husababishwa kwa njia mbili. Kwanza moshi wa sigara huwasha macho na
pili kemikali zilizo ndani ya sigara hupita kwenye mishipa , damu na
hatimaye kudhuru macho. Sigara pia husababisha kudhoofika kwa sehemu ya
kati ya macho(
retina) na hivyo kupunguza uwezo wa macho kuona vizuri na hata kutofautisha rangi(macular degeneration).
3.Kukunjana kwa ngozi
Kemikali
zinazopatikana ndani ya sigara hupunguza uwezo wa ngozi kujirekebisha
hivi basi ngozi huzeeka haraka na kupoteza uwezo wa kulainika. Mvutaji
wa sigara huonekana mzeee zaidi kuliko umri wake haswa.
4.Magonjwa ya masikio
Uvutaji
sigara huleta magonjwa mengi ya masikio . Sababu ni kwamba uvutaji wa
sigara husababisha uchafu kuganda kwenye mishipa ya damu na hivyo
kupunguza mwendo wa damu hadi kwenye sehemu za ndani za masikio. Moshi
na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani za masikio na
majeraha hayo yanaweza kuambukiza hata ubongo(
menengitis). Yote haya yanaweza kusababisha uziwi.
5.Saratani ya ngozi
Uvutaji sigara unasababisha saratani ya ngozi. Kemikali za sigara husababisha vidonda kwenye ngozi na ambavyo haviponi kwa urahisi. Baada ya muda hugeuka kuwa saratani.
6.Magonjwa ya meno
Sigara
hutatiza mdomo na kuongeza uchafu unaoganda kwenye meno hivi
kusababisha kuoza kwa meno, harufu mbaya mdomoni na uchafu wa meno.
Sigara pia hutatiza kupona kwa vidonda hasa baada ya kung’olewa kwa
jino. Saratani ya mdomo na ulimi inapatikana zaidi kwa wavutaji sigara
na watumiaji wa tumbako za aina nyingine.
7.Magonjwa ya mapafu
Uvutaji
wa siagara ndio sababu kubwa zaidi ya saratani ya mapafu. Pia
husababisha kupasuka kwa vibofu vya hewa safi na kutoa harufu mbaya
mwilini. Wavutaji pia hupata saratani ya koromeo na kuziba njia ya hewa
na hivo basi inabidi kutobolewa kwa kishimo kwenye shingo hili kuwezesha
mwadhiriwa kupumua.
8.Mifupa
Sigara
inasababisha mifupa kuwa myepesi na kupunguza nguvu. Sababu ni kuwa
kemikali zilizoko ndani ya sigara hupunguza uwezo wa mwili kujenga
mifupa iliyo na nguvu. Mifupa kama hii huvunjika kwa urahisi na kuchukua
muda mrefu sana(asilimia 80 zaidi ya mifupa ya kawaida)kupona.
9.Ugonjwa wa moyo
Sigara
ndio sababu kubwa zaidi ya magonjwa ya moyo. Inasababisha moyo kupiga
kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza msukumo wa damu mwililni( high blood pressure).
Mwishowe husababisha mshtuko wa moyo na hata kifo.Moja kati ya kila
vifo tatu ulimwenguni hutokana na magonjwa ya moyo na huua zaidi ya watu
milioni moja kwenye nchi za Afrika.
10.Vidonda vya tumboni
Sigara
hupunguza uwezo wa mwili kujikinga dhidi ya viini vinavvyosababisha
vidonda tumboni. Pia hupunguza uwezo wa tumbo kustahimili nguvu ya asidi
baada ya kula. Vidonda vya mvutaji basi huwa ni vigumu kutibu, na mara
nyingi hutokea tena baada ya kupona.
11.Vidole
Kutu
ya sigara hukusanyika na kuganda kwenye kucha na vidole vya mvutaji.
Kisha hubadilisha rangi ya vidole na kucha kuwa za manjano au maji ya
kunde. Ngozi ya vidole pia hukauka na kuwa ngumu sababu ya joto na
kemikali za sigara.
12.Wanawake
Sigara huongeza hatari ya kupata saratani ya fuko la uzazi(
cancer of theuterus ). NI vigumu zaidi kwa mwanamke mvutaji sigara kutungwa mimba na ni rahisi sana kwake kumpoteza mtoto katika mimba.(
miscarrige). Uvutaji wa sigara pia humfanya mwanamke kumzaa mtoto aliyekufa(
stillbirth)
au aliye na uzito usiotimia wa kawaida. Watoto hawa huwa na afya duni
baadaye. Sababu ni kuwa kemikali za sigara hupunguza mwendo wa mtoto
kukua akiwa angali mimbani. Sigara pia husababisha ugumba(
menopause) kabla ya wakati wake. Sigara pia inaweza kumfanya mwanamke kuwa tasa.
13.Wanaume
Sigara
inapunguza mpigo wa damu kwenye sehemu za uume. Sigara pia huharibu
mbegu za wanaume na kwa hiyo watoto wanaowazalisha huwa na uwezekano
mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya saratani. Sigara pia huwafanya
wanaume kuwa tasa.
14.Magonjwa ya ngozi
Sigara huleta magonjwa mengi ya ngozi kama vile uvimbe, kuwashwawashwa na hudhoofisha hali ya ngozi.
15.Ugonjwa wa ‘Buerger’
Huu
ni ugonjwa wa uvimbe kwenye mishipa ya damu ya miguuni na mikononi.
Mishipa hii huzibika na kuzuia mwendo wa damu kwenye sehemu
zilizoathirika. Isipotibiwa kwa haraka,mvutaji anaweza kukatwa miguu au
mikono.
16.Saratani
Zaidi ya kemikali 40 zinazopatikana kwenye tumbako zimethibitishwa kusababisha
saratani. Ukilinganisha na asiyevuta sigara :
16(a).Mapafu
Mvutaji ana uwezekano wa mara 22 zaidi wa kupata saratani ya mapafu
16(b).Pua
Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya pua.
16(c).Ulimi
Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya ulimi.
16(d).Tumbo
Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya tumbo mara 3 zaidi.
16(e).Figo
Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya figo mara 5 zaidi.
Saratani Zinginezo
Uchunguzi
unaonyesha kuwa saratani ya mdomo ni hadi mara 27, koo(mara 12),
koromeo(mara10).Uchunguzi pia umebaini kuwa kuna uhusiano fulani kati ya
uvutaji sigara na saratani ya matiti.
No comments
Post a Comment