Sikuhizi karibu kila redio station utaskia wakitangaza juu ya clinics za tiba mbadala (HERBAL OR SANITARIUM CLINICS)na hizi utaskia mara zote wakitaja magonjwa yafuatayo kwamba wanayatibu:-
- kisukari (diabetes)
- Presha aina zote
- prostate
- kansa
- HIV
- hedhi
- nguvu za kiume
- chango
- uzazi nk
Binafsi huwa ni mfuatiliaji zaid wa mada ambazo wenye hizi clinics huzitoa ama kwa njia ya redio ama vipeperushi ama vipindi vya TV.
Jambo kubwa ambalo nimegundua ni kwamba wengi ama wote hawa naweza kusema hawana elimu ya TIBA ama utengenezaji wa dawa, ingawa wanaweza kuwa wanajua elimu ya viumbe hai. Nasema hivi kwasababu sijawah kuona popote pale duniani dawa ikatolewa bila kuonyesha active ingrediaents kwenye dawa husika na contraindications achilia mbali mambo mengine kama pharmacokinetics etc.
Ni vyema watengenezaji wa dawa hizi za sili kuonesha Active engridients zilizomo kwenye dawa pia kuonesha jinsi gan dawa zao zinavyofanya kazi mwilini yaani PHARMACOKINETICS AND PHARMACODYNAMICS, kwenye packaging zao.tujifuze kwa wenzetu mfano wachina na wahindi herbal medicines zao utakuta wameelezea kila kitu.
Pia sijawah kuona duniani dawa inatengenzwa bila kufanyiwa clinical trial, sisemei convetional medicine bali hata hizi ambazo ni za kienyeji. Mfano mzuri nchini India wanatumia sana dawa za miti shamba lkn hupita kwenye clinical trials kama zilivyo convetional medicines na hizi hukuta zina maelezo muhimu juu ya dawa husika.
Haya basi tu assume hayo yote hatuyapi vipaumbele na tukasema kwakua imemtibu gfsonwin basi na mwingine mgojwa anywe swali kwangu linabaki nani ajuaye fate yake?? je wagonjwa wanaozitumia huwa wanafanya Blood Biochemistry kujua hatma ya hizi dawa?? ama kisa imenitibu presha hata kama ikiua maini ni sawa??
hilo ni dogo manake hakunaga mtu aliyewah kufa akasifiwa marehem kaenda na viungo vyake vyote vikiwa vizima, kubwa kuliko yote unakuta mtu ana justfy kutibu magonjwa hadi 40 lkn ukichunguza mti ni huo huo ila akapaki vichupa tofauti tofauti sasa huu sio wizi?? si bora apaki kwenye kifungashio kimoja ila aonyeshe kwamba unatibu magonjwa yote haya??
Kana kwamba haitoshi watu hawa hutoa elimu za uongo juu ya afya, na inaumiza sana pale mtu anapoongelea maswala ya afya halafu anamislead watu. tena ili kujizidishia wateja anaacha kabisa kuongea habari za lishe bora, na usafi anakazania kuhubiri products zake zinavyotengeneza afya ya mgonjwa hata nje ya lishe bora hivi kweli huu si uuaji??
Vipimo vyao sasa,utakuta mtu anashikishwa kitu mkononi alafu anaoneshwa video aupicha ya tumbo lake lilivyo ndani kwenye computer ukifatilia hiyo video ni video ya kipimo cha endoscope ambacho mtu humeza,matokeo yake utaambiwa utumbo umeoza,Matokeo yake unaishi kwa stress.
Jamani wenzangu tiba bora unaweza kuipata Hospitali pekee kwa watu ambao wako trained na kila siku wanaongezewa maarifa. Afya yako mgonjwa utaiboresha kwa kula chakula bora, kumeza dawa sahihi, na kuwa msafi basi nje ya hapo ni uongo tu. Kumbukeni kwamba kwa kula mlo kamili unapata virutubisho muhimu kwa ajili ya kupambana na magonjwa, kukuza mwili, kutia nguvu na joto na hata kuimarisha mifupa na kungeza damu, na kwa kuwa msafi unajikinga na magonjwa hasa yaenezwayo kwa iyo lishe bora na usafi ni muhim.
Unapoamua kutumia dawa za mitishamba hakikisha inaonesha Active engridients na inafanyaje kazi mwilini,na je haina madhara yoyote mwilini.
Kwa wauzaji na watengenezaji wa dawa hizi ni vyema mkahakikisha kwenye vifungashio vyenu mmeonesha active engridients,pharmacodynamics na pharmacokinetics za dawa zenu.
NAOMBA IELEWEKE SINA NIA YA KUHARIBU BIASHARA YA MTU, BALI NINASEMA KWELI MANAKE WAMEZIDI KUTUIBIA.

No comments
Post a Comment