Kukohoa
ni njia inayotumiwa na mwili ili kuhakikisha kwamba njia au mfumo wa
upumuaji katika mwili wako unakuwa salama, na hii ni kwa kuhakikisha
kwamba vitu kama vumbi, bacteria au kitu chochote kile kisichokuwa
salama, basi hakipati nafasi ya kukudhuru wewe kupitia njia ya upumuaji.
Pamoja
na kikohozi kuwa njia ya mwili kujilinda, bado unapaswa kuchukua hatua
za kupata matibabu zaidi endapo tatizo hili litakuwa endelevu hata zaidi
ya wiki moja baada ya kutumia njia tofauti tofauti za kujitibu au
kutumia dawa rahisi zinazopatikana katika mazingira ya nyumbani (mfano
tangawizi au kitunguu saumu).
Mpenzi msomaji, wewe binafsi unafahamu tatizo la kikohozi unalipa uzito gani, ila ningependa kukufahamisha baadhi ya madhara ambayo huweza kumpata mtu endapo atapuuzia tatizo hili:
Kwanza
kabisa utakubaliana na mimi kwamba, endapo mtu anakohoa, basi inamuwia
vigumu kuyanyoosha maelezo yake au hawezi kuongea katika mtiririko wa
maneno ulio mzuri, hii ni kutokana na kujikuta kila baada ya neno moja
au hata kabla hajamaliza kusema neno moja tayari kikohozi kinamkatisha
usemi.
Kutokana
na kukohoa kusababisha presha kubwa kujengeka katika mdomo na koo, hii
hupelekea mtu kupata maumivu ya kichwa na hivyo kukupelekea kupata
usumbufu zaidi na kuongeza gharama za matibabu kwako.
Kukohoa kwa muda mrefu husababisha matatizo katika kibofu cha mkojo kwani presha kubwa inajengeka katika kibofu cha mkojo na hivyo kuathiri mfumo wa kawaida wa namna kibofu chako cha mkojo kinavyo stahimili kuhifadhi mkojo na kazi zake kwa ujumla.
Kuna mishipa midogo ya damu katika pua na pia katika njia ya kutolea haja kubwa (Anus), ambapo kwa namna mtu anapokohoa kwa muda mrefu, mishipa hii huweza kupasuka na kupelekea damu kutoka au kusababisha tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kama, haemorrhage.
Wakati
mwingine kikohozi ni dalili ya magonjwa kama vile, Kifua kikuu, magonjwa
ya mapafu kama vile kansa, magonjwa ya moyo ( congestive heart failure )
pamoja na magonjwa ya masikio.
Pia kikohozi kingine husababishwa na matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu presha (High blood pressure) mfano dawa ya Captopril ( ACE- Inhibitor ), na hivyo kuhitaji kubadilishiwa dawa na kupewa ushauri unaostahili.
Mpenzi
msomaji, ni vyema tukazidi kuwa makini na kuchukua tahadhari mapema pale
tunapoona hali isiyokuwa ya kawaida katika afya zetu.

No comments
Post a Comment