Kinywa kutoa harufu mbaya huweza kuwa kero kwako binafsi au kwa watu wanaokuzunguka.
Yapo matibabu aina mbalimbali dhidi ya kinywa kutoa harufu mbaya, ikiwepo pamoja na pipi, bigijii na dawa za kusafisha meno
Dawa hizi huweza kuwa zinafanya kazi au kutomsaidia mtu. Jambo la msingi ni kufahamu nini kisababishi na kuanza matibau ya
Kisababishi
Dalili
Darufu ya kinywa hutofautiana kutokana na nini kilichosababisha, kuna baadhi ya watu huhofu saa kuhusu harufu ya kinywa ingawa wana harufi kidogo inayotoka, na kuna wengine wanavinywa vinavyotoa harufu mbaya bila wao kujitambua. Siku zote muulize jirani yako endapo kinywa chako kinatoa harufu au la.
Visababishi
Kuna visababishi mbalimbali vinavyoweza kupelekea kinywa kutoa harufu mbaya, mara niyngi huwa chakula, Tania na hali ya kiafya ya mtu
Chakula
Vyakula jamii ya vitunguu, tangawizi, na viungo vingi vya chakula endapo vitamengenywa na bakteria katika kinywa huleta harufu mbaya ya kinywa. Vyakula jamii ya nyama pia endapo vitaliwa na kubaki katika kinywa huoza nakusababisha harufu mbaya kutoka kinywani
Kutofanya usafi wa kinywa
Kama husafishi kinywa kwa dawa ya mswaki na kuchukutua mdomo mara baada ya kula haswa wakati wa jioni, utapata harufu mbaya mdomoni kutokana na vyakula hivyo vinavyobaki kinywani kuoza na kutoa harufu. Vyakula mara nyingi vikibaki kinywani hutengeneza ukuta kuzunguka meno na ulimi na kuta hizi ni chakula kizuri kwa bakteria waliopo mdodomoni. Bakteria wanapokula kuta hii husababisha kuzalisha kwa tindikali na harufu mbaya mdomoni
Midomo kukauka
Mate husaidia kuosha mdomo dhidi ya mabaki ya chakua na harufu, endapo mtu ana midomo iliyokauka kwa kukosa unyevu wake atapata harufu mbaya kinywani. Midomo kukauka hutokea sana wakati wa usiku kama asili ya maumbile ya binadamu na hivyo mtu kuamka na harufu mbaya kinywani wakati wa asubuhi. Tatizo la harufu mbaya kinywaji huzidi endapo mtu amelala kinywa kikiwa wazi.
Baadhi ya dawa
Dawa zinazokausha mate husababisha kinywa kutoa harufu kama yalivyo maelezo ya hapo juu. Baadhi ya dwa pia huwa na kemikali ambazo zikivunywa kinywani au tumboni husababisha mtu kuwa na harufu mbaya kinywani.
Maambukizi ya kinywa
Mtu akiwa na maambukizi kinywani huweza kutoa harufu mbaya. Maambukizi haya yanaweza kuwa kwenye vidonda vinavyotokana na upasuaji, kutolea jino, kuoza kwa meno au magonjwa mengine ya kinywa na meno.
Magonjwa mengine ya kinywa, koo na pua kama tonsil n,k
Saratani, magonjwa ya kimetabliki na tatizo la kiungulia huweza kusabaisha kinywa kutoa harufu kali, watoto wadogo wanaweza kutoa harufu kali kinywani kutokana na vipande vya chakula kubaki kinywani.
Mara nyingi mtu anaweza kuimarisha afya ya kinywa chake kwa kuzingatia usafi wa kinywa


No comments