MAAMBUKIZI YA SIKIO



Maambukizi ya masikio ni maambukizi  yanayotokea sana na mara nyingi husababishwa na bakteria au virusi ambao huathiri sikio la kati ambalo lipo nje au ndani ya sikio( eneo lililopo kwa ndani ya ngoma ya sikio). Watoto hupata sana maambukizi ya masikio ukilinganisha na watu watu wazima.
Maambukizi kwenye masikio yanaweza kusababisha maumivu ya masikio, maumivu haya husababishwa na michomo inayoletwa na maambukizi na kujikusanya kwa maji maji kwenye sikio la kati
Kwa sababu maambukizi ya masikio huisha yenyewe wakati  mwingi, matibabu huanza kwa kutibu maumivu na kuzuia Matatizo yanayotokana na maambukizi haya.
Dalili
Dalili na viashiria vya maambukizi ya masikio hutokea ghafla.
Dalili za watoto
Dalili za maambukizi ya masikio kwa watoto huwa pamoja na;
Maumivu ya masikio, san asana mtoto akilala
  • Kuweka vidole wkenye masikio au kuvuta masikio
  • Kushindwa kulala
  • Kulia kulika kawaida
  • Mtoto kusumbua kusiko kawaida
  • Kushindwa kusikia au kuitikia sauti
  • Kushindwa kuwa na balance anapotembea
  • Homa au joto la mwili Kupanda
  • Kutokwa maji au usaha masikioni
  • Maumivu ya kichwa
  • Kupoteza hamu ya kula

Mtu mzima
Dalili zinazotokea kwa watu wengi ni
  • Maumivu ya sikio
  • Kutokwa na maji au usahaha kwenye sikio
  • Kupunguza kusikia
Visababishi
Maambukizi ya sikio husababishwa na maambukizi ya bakteria au virusi kwenye sikio la nje au ndani
Maambukizi haya yanaweza kutokana na kupata mafua, mzio ambao husababisha maji maji kuziba kwenye njia za pua, koo na mrija wa sikio(bonyeza hapa kusoma kazi za mrija huu)
Vihatarishi
Umri wa mtu-watoto kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 huwa na kihatarishi cha kupata maambukizi haya kwa sababu ya umbo na ukubwa wa mrija(eustachian) wa sikio na kuwa na kinga za mwili kidogo
Mtoto kulelewa kwenye vituo vya watoto
Watoto wanaosoma shule za boording au kulelewa kwenye vituo vya watoto huwa na kihatarisi cha kupata mafua na maambukizi ya masikio kuliko watoto wanaokaa nyumbani, hii ni kwa sababu wanajiweka kwenye hatari ya maambukizi kama vile homa ya baridi(mafua)
Kunyonyesha mtoto kwa chupa
Mtoto kunyonyeshwa kwa njia ya chupa haswa akiwa amelala chali hupata maambukizi haya sababu ikiwa maziwa huwa yanaingia kwenye mrija wa sikio. Watoto wanaonyonya maziwa ya mama kwenye chuchu huwa hawapati maambukizi hay asana.
Hali ya msimu
Hali za kimsimu huwa sababu kuu ya  kupata maambukizi ya masikio hasa kipindi cha baridi na mvua ambapo watu hupata sana mafua na homa ya baridi. Watu wenye aleji na maua hupata sana maambukizi ya masikio wakati wa msimu wa maua
Hewa chafu-Hewa iliyochanganyika na moshi wa sigara au tumbaku au maeneo yenye uchafuzi wa hewa huwa kihatarishi kikubwa cha kupata maambukizi ya masikio
Madhara
Kupoteza uwezo wa kusikia

Kuchelewa kuongea na maendeleo ya mtoto
Mtoto akipata maambukizi ya masikio mapema katika maisha yake anakuwa na kihararishi cha kushindwa kuongea na kushirikiana na jamii yake ipasavyo
Kusambaa kwa maambukizi
Kama maambukizi ya masikio yasipotibiwa huweza kusambaa kwenye mifupa na sehemu zingine zilizo karibu na sikio, mtoto anaweza kupata uvimbe nyuma ya sikio endapo maambukizi yameenda kwenye mifupa au kupata homa ya uti wa mgogo.
Kupasuka kwa ngoma ya sikio
Maambukizi yasiyotibiwa au maambukizi sugu ya masikio huweza kushia kupasua ngoma ya sikio, ngoma ya sikio ikipasuka inaweza kupona ndani ya masaa 72 wakati mwingine huhitaji upasuaji ili kurejesha ngoma hiyo
Matibabu
Baadhi ya maambukizi huweza kupona yenyewe bila matibabu ya dawa, matibabu bora kwa mtoto wako hutegemeavitu vingi ikiwa pamoja na umri na ukubwa wa tatizo
Kutizamia hali kwanza bila tiba
  • Dalili za maambukizi ya sikio hupotea siku chache na nyingi ha maambukizi mengine hupona bila matibabu.
  • Watoto wanaoweza kusubiria ni wale wenye umri wa miezi 6 hadi 23 wenye maumivu ya wastani ya sikio kwa mda wa masaa 48 na joto la mwili kuwa nyuzi joto za cilisius 39 au mwenye miezi zaidi ya 24 na akiwa na dalili hizo kwenye sikio moja au yote kwa mda wa masaa 48 na joto likiwa chini ya nyuzi joto 48
Tafiti zinaonyesha kuwa matibabu mapema yanaweza kusaidia kuliko kusubiria
Kutibu maumivu
Maumivu yanaweza kutibiwa kwa njia mbalimbali
Tumia kitambaa kilichochovywa kwenye maji ya uvuguvugu  kwenye sikio lililoathiriwa na maambukizi
Tumia dawa za maumivu
Dawaza maumivu jamii mbalimbali zinaweza kutumia katika matibabu ya mtoto mwenye tatizo la masikio kuuma na kutoa usaha ikiwa pamoja na paracetamu, ibrupofen. Tumia dawa kama ulivyoshauriwa na daktari wako kuwa mwangalifu unapokuwa unampa dawa ya maumivu aina ya aspirini kwa sababau huweza kuleta madhara endapo mtoto anaumwa tete kuwanga
Dawa za antibiotic
Dawa mbalimbali za antibiotic zinaweza kutumika, uchaguzi wa aina ya dawa na kiasi hutegemea hali ya maambukizi na usugu wa tatizo. Siku zote wasiliana na daktari ili kupata dawa sahihi na kiasi kinachotakiwa usinunue dawa bila kuongea na daktari.
Kujikinga
  • Mfundishe mtoto anawe mikono mara kwa mara na sehemu zote na asishiriki vyombo vilivyotumiwa na watoto wenzake.
  • Mfundishe mtoto kupiga chafya kwa kuziba mdomo na mikono miwili
  • Mzuie asilelewe kwenye shule zenye watoto wengi au akiwa anaumwa mchukue kumtibu
Zuia mtoto kukaa na anayevuta sigara
Usikae karibu na mtu anayevuta sigara au kukaa karibu na mazingira yenye uchafuzi wa hali ya hewa kwa moshi ili kuzuia kupata maambukizi ya masikio.
Mnyonyeshe mtoto ziwa la mama
Kama ukiweza mnyonyeshe mtoto kwa ziwa la mama kwa mda wa miezi sita kwanza na endapo utakuwa unamnyonyesha mtoto kwa kutumia chupa basi hakikisha amekaa wakati wa kunyonya. Usimlaze mtoto wakati wa kumnyonyesha

Ongea na daktari wako
Ongea na daktari wako endapo kuna kinga dhidi ya maambukizi ya masikio ili upatiwe
Kabla ya kukutana na daktari jiandae kujibu maswali yafuatayo;
Kama mwanao ana umri mkubwa na anaweza kujibu maswali, mzazi unatakiwa kujiandaa na maswali yafuatayo
  • Dalili gani ulizoziona kwa mtoto
  • Dalili zilianza lini?
  • Kuna maumivu ya masikio, unawezaje kuelezea maumivu hayoaumaumivu hayo yakoje?(makali au ya kawaida)
  • Umewahi ona dalili ashiria zozote za maumivu kama ni mtoto mchanga kama vile kuvuta sikio, kushindwa kulala au kulia lia tum da wote
  • Mtoto anachemka? Mwili kupata homa
  • Je kuna uchafu wowote ule unatoka kwenye masikio?(maji maji, usaha au damu) na unatoka mara ngapi kwa siku na kwa siku ngapi sasa?
  • Je mtoto amekuwa hasikii?, mtoto anaweza kusikia sauti za mnong’onezo na kama ni mkubwa je anasema sema  umesema “nini”  au “unasemaje” mara kwa mara?
  • Mwanao amepata mafua au homa baridi hivi karibuni au magonjwa mengine ya kifua?
  • Mwanao ana mzio wa majira Fulani?
  • Mwanao alishawahi pata maambukizi ya sikio kipindi cha nyuma?
  • Mwanao anamzio wowote na dawa mfano dawa jamii ya penicillin?

Wakati gani uonanae na daktari
Dalili na viashiria vya magonjwa ya sikio huweza kumaanisha mambo mbalimbali, ili kupata kujua tatizo halisi ni vema kuonana na daktari wako endapo dalili zinakaa zaidi ya siku moja au zinaonekana kwa mtoto aliye chini ya mwaka 1 au kupata maumivu makali sana, au mtoto anashindwa kulala au kama umeona uchafu ukitoka

1 comment: