Wednesday, 25 March 2020

Mabadiliko ya mwili wakati wa ujauzito

Utangulizi
Unapogundua kwamba una ujauzito, unaweza ukaanza kupanga kuhusu afya ya ujauzito wako wiki moja baada ya nyingine. Kila siku unaweza kuwa unajiuliza maswali jinsi ya kuwa na afya njema ya ujauzito uliobeba na kama nile chakula gani?  nini au vipimo gani nifanye?
Kama umebeba mapacha unaweza kuanza kupanga kuhusu ujauzito huo kila wiki kwamba uzito gani natakiwa kua nao? Nini nifanye nisipate uchungu kabla ya wakati wake? Au unahitaji kupumzika?
Kwa Kila jambo unaloweza kujiuliza, kifupi ni kwamba ni muhimu kujua kuhusu ujauzito wako wiki moja baada ya nyingine kwa sababu kutakupa kufanya uamuzi sahihi kipindi chote cha ujauzito. Jifunze kuhusu vyakula vinavyotakiwa na ambavyo havitakiwi na upate elimu ya msingi kuhusu mambo flani yanayotokea kipindi cha ujauzito kuanzia mazoezi maumivu ya mgongo na kuhusu kujamiiana, jinsi unavyofahamu kuhusu ujauzito wako kunakuweka tayari kujiandaa kwa wakti wote kukabili mambo yanayoweza kutokea mbeleni wakati wa ujauzito

Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito

 

Miezi mitatu ya kwanza (first trimester) huambatana na mabadiliko ya haraka ya mwili wako na mtoto aliyepo tumboni
Kwako wewe mama, mabadiliko ya kimwili yanaweza kuwa maumivu ya ziwa, kuchoka, na kichefuchefu. Hulka yako inaweza kuwa ya furaha au huzuni sana. Kwa mtoto wakati huu huwa anakuwa haraka na kubadilika. Ubongo wa mtoto, uti wa mgongo na viungo au organi mbalimbali huanza kutengenezwa na moyo wa mtoto huanza kufanya kazi pia na vidole vya mkono na miguu huanza kuwa na umbo halisi.
Kama upo katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya kwanza basi fanya mawasiliano na mtaalamu wa afya unaze kliniki kwa ajili ya wajawazito unaweza kujifunza kuhusu nini utarajie katika kipindi hiki na utakachojifunza kinaweza kukusaidia kuchukua hatua ili uwe na afya njema na mtoto wako

Miezi mitatu ya pili


Kipindi cha miezi mitatu ya pili au Second trimester, kuanzia miezi mitatu hadi sita unaweza kujisikia vyema kuliko ilivyokuwa miezi mitatu ya kwanza na wakati huu ni wa kufurahia ujauzito ulionao

Kipindi hiki mtoto anaanza kuonekana kuwa kama binadamu. Dalili kwa mama zinaweza kuwa maziwa kubwa makubwa, tumbo kuongezeka na mabadiliko ya ngozi yako. Mtoto hupata uwezo wa kucheza na kusikia pia. Unapofikisha wiki ishirini za ujauzito unakuwa katikati ya  kipindi cha ujauzito

Kutembelea kliniki kila mwezi au wiki kutokana na taratibu ulizowekewa na dakitari hutakiwa kufanyika kama kawaida, mwambie mhudumu wa afya kuhusu nini unataka kujua nini hata kama ni cha ujinga au hakina umuhimu eleza hisia zako

Miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito


Miezi mitatu ya mwisho au third trimester inaweza kuwa kuwa na mabadiliko ya kimwili na kihisia laini mama  anaweza kupata dalili za maumivu nyuma ya mgongo, kuvimba miguu na kupata huzuni inayoongezeka

Wakati huu, mtoto atafungua macho na kuongezeka uzito pia. Ukuaji au uongezekaji wa haraka wa uzito unaweza kuambatana na mtoto kuongeza kucheza tumboni na unapoanza wiki ya 39 za ujauzito , mtoto huwa ameshakuwa katika kiwango cha wisho

Kipindi cha miezi mitatu ya mwisho utatakiwa kukutana na wataalamu wa afya au kliniki kama ilivyo ratiba uliyopewa na tarehe za matarajio za kujifungua zinapokaribia jaribu kuuliza maswali mengi kwa mtaalamu wa afya. Mtaalamu wa afya utaweza kupimwa shingo ya kizazi na mlalo wa mtoto.
Kujua kuhusu kipindi hiki cha miezi mitatu ya mwisho kunaweza kukusaidia wakati wa mwisho wa kujifungua

No comments

Post a Comment