Ugonjwa wa kirusi cha corona kitaalam
COVID-19 uliripotiwa kwanza tarehe 31 December 2019 jimbo la Wuhan China. Mpaka
kufikia juzi March 13 wagonjwa 136,895 wamethibitishwa kati ya hao watu 5,077
wamepoteza maisha katika nchi 123 duniani kote kulingana na takwimu za WHO.
Kufikia March 13 nchi 12 za Africa
ziliripoti uwepo wa wagonjwa mpaka jana March 14 ziliongezeka Sudan, ambapo mtu
mmoja alifariki, Ethiopia, Kenya na Gabon. Wengi wameanza kusema kuwa huu ni
mwisho wa dunia wengine wakisema ni ugonjwa wa kutengenezwa.
COVID-19 ni nini?
Hiki ni kirusi kutoka katika familia kubwa
ya virusi vya corona. Virusi vya corona vipo vya aina nyingi na vinaweza
kusababisha mafua ya kawaida na pia mafua hatari kama Severe Acute Respiratory
Syndrome (SARS) NA Middle East Respiratory Syndrome (MERS). COVID19 ni
vinasaba vipya ambavyo havijawahi kutokea hapo awali.
Chanzo cha virusi vya corona inaripotiwa
kuwa wanyama pori dalili ni pamoja na homa, kikohozi, kukosa pumzi na kupumua
kwa shida.
Kwanini mlipuko huu sio mwisho wa dunia
Ugonjwa huu umeripotiwa kwanza December 31
mwaka jana, hii haimaniishi ulianza tarehe hio. Kuna uwezekano mkubwa watu
walianza kusambaza virusi vya Corona mapema zaidi na kwa sababu wengi hupata
dalili zisizo kali, zenye kufanana na mafua, wasijue wameambukizwa corona.
Kutoka katika ripoti ya chuo kikuu cha
John’s Hopkin’s marekani takribani 3.7 % ya waliougua corona wamefariki. Maana
yake ni kwamba takribani 96% ya wagonjwa watapona.
Ukilinganisha na aina nyingine ya virusi
vya corona kama SARS kiasi cha wagonjwa wanaofariki ni 10% (jumla ya wagonjwa
waliofariki duniani ni 774) na MERS ni 34% (toka 2012 watu waliofariki
wamefikia 858). Mafua ya msimu (seasonal flu) huko marekani yanauwa 0.1% ya
wagonjwa.
Kihistoria kuna magonjwa hatari zaidi
yaliowahi kutokea
Mwaka 1347 dunia ilikumbwa na ugonjwa wa
tauni (The Black Death) ambayo inakadiriwa kuuwa watu kuanzia milioni 25 hadi
milioni 200 sawa sawa na idadi ya wa
wananchi wote wa Nigeria leo hii.
Mwaka 1918 janga la kidunia (pandemic) la
mafua ya hispania (spanish flu) lilitangazwa. Mafua ya hispania yaliathiri watu
milioni 500 na kuuwa takribani watu milioni 50 sawa na idadi ya watanzania.
Mwaka 1968 mafua ya Hong Kong yaliuwa
takribani watu milioni 1 hadi 4. Na janga la mwisho la kidunia kutangazwa na
WHO kabla ya corona ni mafua ya nguruwe mwaka 2009 yalioathiri watu milioni 60
na kuuwa watu 12,469.
Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba dunia
imepitia majanga mengi yaliokuwa na athari kubwa kwa uhai wa mwanadamu zaidi ya
corona na tukashinda bila dunia kufika mwisho. Cha msingi ni kuendelea
kusikiliza maelekzo kutoka katika mamlaka za afya, kufuata maelekezo ya kunawa
mikono kwa sabuni au hand sanitizers, kutosalimiana kwa kupeana mikono na
kuripoti mgonjwa mwenye dalili tajwa. Usidharau lakini pia usi panic

No comments