Degedege ni mijongeo ya ghafla, mikali, isiyo ya hiari na mpangilio maalumu inayotokea kwenye mwili inayosababishwa na kujongea kwa misuli kama matokea ya kuharibika kwa mfumo wa fahamu wa ubongo kwa kutoa taarifa pasipo mpangilio.
Kwa kawaida Ubongo hutoa taarifa za kuamrisha viungo vingine kufanya kazi, taarifa hizi husafiri kama umeme kupitia mishipa ya fahamu na kufika sehemu ambayo imeamuriwa kufanya kazi. Umeme unapofika sehemu husika ya mwili, mwili huitikia kwa kufanya ile kazi iliyoamriwa. mfano wa baadhi ya kazi ni kama vile kutembe kushika kitu, moyo kufanya kazi, kutoa haja kubwa n.k.
Mfuo huu wa ubongo ukitoa umeme pasipo mpangilio, mtu hupata dalili za mijongeo isiyo ya hiari na kuonekana kama degedege
Kifafa ni hali inayotokea endapo mtu atapata degedege mara mbili ama zaidi ndani ya masaa 24 bila kuwa na kisababishi chochote.
Visababishi
Nini huweza kuamsha degedege?
- Homa
- Maambukizi kwenye ubongo au ukuta wa meninjo
- Kuzimia
- Kupigwa ama kuumia kichwani
- Kukosa hewa safi ya oksigeni
- kunywa Sumu inawezekana kuwa ni dawa au chakula
- Magonjwa ya moyo
Kifafa endelevu
Kifafa endelevu ni pale mtu anapopatwa na degedege la kudumu zaidi ya dakika 30 ama kutokea kwa degedege pasipo kurudiwa na fahamu kati ya degedege moja na lingine
Nini sababu za kupata degedege la kifafa?
- Asilimia 70-80 hakuna sababu inayofahamika
- Uvimbe ndani ya kichwa(uvimbe wa kawaida au saratani)
- Kuharibika kwa mishipa ya fahamu ya ubongo
- Sababu zingine kama kuharibiwa kwa ubongo kama kunakoweza kusababishwa na maambukizi ya kuzaliwa nayo, kukosa hewa safi ya oksigeni wakati wa kuzaliwa, kuvilia kwa damu ndani ya ubongo haswa kwa watoto njiti
- Maumbile mabaya ya kichwa ama kupata tatizo baada ya kuzaliwa kama kichwa maji
Nini husababisha degedege lisilo la kifafa
- Homa kali
- Kuharibika kwa mfumo wa damu mwilini kama kushuka sana kwa kiwangoo cha sukari ya glukosi, kuzidi ama kupungua kwa kiwango cha madini ya kalisium, potasiamu, na madini ya sodiamu
- Kupigwa kichwani ama kuumia kichwa kutokana na ajari
- Maambukizi ya uti wa mgongo
- Michomo katika ubongo
- Sumu/ madawa
Aina za degedege
Kuna aina mbalimbali za degedege
Degedege linalotoka katika sehemu ndogo ya ubongo
Mfumo wa umeme huharibika katika sehemu ndogo sana ya ubongo, hivyo halidhuru eneo kubwa sana la mwili. Mtu anaweza kupoteza ama kutotopeza fahamu degedege linapotokea na hutanguliwa na dalili za onyo.
Degedege linalotokana na sehemu kubwa ya ubongo kutoa umeme
Umeme mkubwa hutolewa kutoka sehemu mbalimbali za ubongo, pasipo kutanguliwa na dalili za onyo na mtu hupoteza fahamu siku zote
Dalili za degedege
Dalili na viashiria vya degedege zinaweza kuwa dalili za wastani au kali ikitegemea aina ya degedege. Baadhi ya dalili huwa kama zifuatazo;
- Kuchanganyikiwa kwa muda mfupi
- Kuwa na sura ya kuogopesha
- Kujongea kwa misuli ya mwili bila hiari haswa mikono na miguu
- Kupoteza fahamu au kutojitambua
- Dalili za kutojitambua kama kuogopa,
- Kutokwa na mkojo au kinyesi bila hiari kama dalili ambata
- Kutokwa na mate au undenda mdomoni kama dalili ambata


No comments