Saturday, 22 February 2020

UGONJWA WA KISUKARI

Kisukari (Diabetes mellitus) ni kundi la magonjwa linalotokana na kuathirika kwa mfumo wa utumiaji sukari mwilini. Sukari ni chanzo cha nguvu mwilini mara inapoingia katika chembe hai, hivyo ina umuhimu kwa kuendeleza maisha ya chembe hizi. Ubongo hupata nguvu za kuweza kufanya kazi kwa asilimia kubwa kutoka kwenye sukari(glucose) na isipokuwepo inaweza kuleta madhara kama kuzimia n.k

Mtu akiwa na kisukari pasipo kutegemei aina gani, kinachotokea ni kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika mzunguko wa damu na  hivyo huleta matatizo makubwa kwenye ogani mbalimbali mwilini.

Matatizo sugu ya kisukari yanaweza kugawanyika katika sehemu mbili, kisukari cha kupanda aina ya kwanza na cha aina ya pili, mtu mwenye dalili za awali za kupanda kwa sukari ila bado hana sifa za kuitwa anakisukari, kisukari chake huweza kudhibitiwa, na mtu huyu anaweza asiugue ugonjwa wa kisukari endapo atazingatia masharti ya chakula na mazoezi.

Kipo kisukari kinachotokea wakati wa ujauzito ambacho huitwa kisukari cha ujauzito, kisukari hiki  huweza kuisha baada ya ujauzito au huweza kuendelea baada ya ujauzito

Aina za ugonjwa wa kisukari


kisukari aina ya kwanza

Kisukari aina ya kwanza ni ugonjwa unaotokana na kushindwa kuzalishwa kwa homoni ya insuline kwa sababu ya kuharibiwa kwa chembe hai ndani ya kongosho zinazotengeneza homoni hii, chembe chembe za mwili wa mtu huhusika kufanya uharibifu huu.

Ugonjwa huu huanza utotoni kwa asilimia kubwa lakini unaweza kuanza kwenye miaka ya 30 au 40.

Kisukari aina ya kwanza kimeonekana kuhusianishwa na maambukizi ya kirusi cha enterovirus kwa kuwa watoto wengi walioonekana kuwa na maambukizi haya huko taiwan walikuwa na kisukari aina hii kwa kiwango kikubwa ukilinganisha watoto ambao hawakuwa na virusi hao.

Kisukari hiki huwa na dalili  za kula sana , kunywa maji sana, kukojoa sana, kupungua uzito  dalili zingine ni kuchoka, kichefuchefu na kutoona vema.

Kisukari aina ya pili

Kisukari aina ya pili hutokea kutokana na udhaifu unaotokea mwilini  kama upinzani wa hormoni ya insuline kufanya kazi au kutozalishwa kwa wingi kwa homoni hii au homoni ya glucagoni ikizalishwa kwa kiwango kisichotakiwa madhara ya haya yote ni kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu na chembe hai za mwili.

Kisukari aina ya pili hutokea kwa watu wazima yaani watu wenye umri zaidi ya miaka 35 na vihatarishi vya kupata kisukari hiki ni

  • Uzito. kuwa na uzito mkubwa kunakuweka hatarini  kupata kisukari aina ya pili , jinsi unavyokuwa na mafuta mengi upingamizi katika kazi za homoni ya insulini huongezeka. Ingawa haina maaana unatakiwa uwe na uzito mkubwa ili upate kisukari ila hata mwembamba anaweza kupata kisukari hiki aina ya 2
  • maeneo mafuta yalipojihifadhi. Kama mwili wako umehifadhi mafuta sehemu ya tumboni huwa ni kihatarishi cha kupata kisukari zaidi ya mtu mwenye mafuta haya sehemu nyinginezo kama mapaja na nyonga.
  • Kutofanya kazi. kutojishughulisha na kazi za hapa na pale kunaongeza hatari ya kupata kisukari aina ya 2.kufanya kazi au mazoezi kunasaidia mwili kutumia sukari na kuongeza utumiaji wa chembe hai wa insulini na sukari(glucose)
  • Historia ya ugonjwa huu kwenye familia kama mzazi au watoto wana kisukari aina hii ya pili basi unahatari ya kupata pia.
  • Utaifa. watu weusi, wa hispania, muamerika na muhindi na waasia wapo hatarini zaidi kupata kisukari aina hii ya pili
  • Umri. Umri zaidi ya miaka 45 kisukari aina hii ya pili hutokea sana na hili ni kwasababu labda watu katika umri huu hufanya mazoezi kidogo na wanapoteza misuli na kuongezeka uzito sana. Kisukari aina hii kinaongezeka sana kwa vijana wadogo pia katika karne hii.
  • Kisukari wakati wa ujauzito. Kama ulipata kisukari wakati wa ujauzito basi kisukari hicho huweza kuendelea kwa baadhi ya wanawake na endapo umejifungua mtoto zaidi ya kilo 4 basi pia inakuweka hatalini.
  • Ugonjwa wa Polycystic ovary syndrome. ugonjwa unaoleta dalili za kuwa na vipindi vya hedhi katikati ya mzunguko, kuwa na nywele nyingi kama mwanaume, kitumbo-obesity huongeza hatari ya kupata kisukari aina hii ya pili.
Zipi ni dalili za kisukari hiki?

Wagonjwa wengi wenye kisukari hiki aina ya pili huwa hawana dalili na kama wanadalili huwa ni;
  • Dalili za kisukari ambazo ni
  • Kukojoa mara kwa mara 
  • Kupata kiu sana/Kunywa maji sana,
  • Kupata njaa mara kwa mara/kula sana
  • Kupungua uzito

Dalili zingine ni
  • Kuona ukungu
  • Ganzi miguuni
  • Maambukizi ya fungasi(kwa sababu ya kinga ya mwili kushuka)

Vipimo


Je vipimo gani hufanywa ukiwa hospitali?

  • kipimo cha sukari kabla hujala kitu chochote asubuhi toka ulipokula usiku wa kuamkia siku hiyo (fasting blood glucose)
    • kipimo hiki kwa kawaida kikizidi miligramu 126 kwa kila desilita moja(126gm/dl) au milimole 7 kwa kila lita moja ya ujazo 97mmol/L) basi mtu husemekana kuwa sukari yake ipo juu
  • sukari kuwa 200mg/dl(11.1mmol/L) au zaidi baada ya masaa mawili ya kupewa sukari yenye gramu 75- kipimo hiki huitwa oral glucose torelance test (OGTT)
  • sukari kuwa zaidi ya 200mg/dl(11.1) au zaidi unapopimwa kwa mara ya kwanza unapoonana na dakitari au kitaalamu huitwa rondum blood glucose-RBG
  • kipimo kingine ni cha kiwango cha sukari kwenye chembe za damu za hemoglobin A1c (HBA1c) ambapo ikiwa asilimia 6.5 au zaidi mtu anaitwa anakisukari

Mtu mwenye sifa zifuatazo anatakiwa kuwa anapima kisukari hata kama hana kisukari 

  • shinikizo la damu kuwa juu zaidi ya 135/80mmHg
  • uzito kupita kiasi au ana vihatarishi kama vya kupata kisukari kama(kuwa na ndugu wa baba/mama mmoja mwenye kisukari, shinikizo la damu zaidi ya 140/90 na kiwango cha lehamu nzuri kwenye damu chini ya 35mg/dl au kiwango cha triglceride kwenye damu  zaidi ya 250mg/dl)
  • Kuwa na miaka zaidi ya 45 hata kama huna sifa za hapo juu
Matibabu ya kisukari ni yapi?

Shirika la dawa na chakula duniani FDA limependekeza mara moja kwa siku mchanganyo wa dawa mbili kwa kisukari aina hii ya pili
dawa hizo ni sodium glucose cotransporter na mertformin.Vidonge vinatakiwa vitumiwe pamoja na mazoezi kwa mtu mwathirika wa kisukari na dawa zinatakiwa zitumiwe asubuhi na chakula. Lengo la matibabu ya kupambana na kupanda kwa sukari ni;
  • kupunguza hatari ya uharibifu wa  mishipa midogo ya damu(microvascular) inayoweza kuathiri utendaji kazi wa Macho na figo
  • Kupunguza hatari ya uhalibifu wa mishipa mikubwa ya damu (macrovascular) inayoweza kusababisha magonjwa ya mishipa ya moyo,ubongo, na maeneo ya miguuni
  • Kupunguza madhara ya kimfumo wa fahamu na utendaji kazi wa chembe hai

Kuzuia madhara ya kisukari


Dakitari au mgonjwa wa kisukari anaweza kuzuia madhara ya kisukari kwa kufanya yafuatayo
  • kupima HBA1c kila baada ya miezi 3 hadi 6
  • kupima macho kila mwaka
  • kupimwa kiwango cha protini kwenye damu
  • kujichunguza miguu kuona kama kuna vidonda na kuvitunza na kupata matibabu kama vitakuwepo
  • kupima shinikizo la damu linatakiwa liwe chini ya 135/80 au pungufu ya hapa kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo kutokana na kisukari
  • kuwa kwenye dozi ya dawa ya statin ili kuzuia hatari ya kupanda kwa lehamu mbaya mwilini Low density lipoprotein cholesterol (LDL-cholesterol)
Madhara sugu ya kisukari

Kuna baadhi ya mambo ya kijeni na uwezo wa kudhibiti sukari yanayoweza kutabiri mtu  gani atapata madhara ya kisukari hapo mbeleni.

Kutokea kwa madhara hutokana na kubadilishwa kwa glukosi kwenda sorbitol kwenye damu, kemikali hii ni sumu kwenye tishu mbalimbali mwilini.
Kuna ushahidi wa kisayansi kwamba kudhibiti vizuri sukari huweza kuzuia madhara mengi yanayoweza kutokea kutokana na kisukari

No comments

Post a Comment