Wednesday, 5 February 2020

Maotea sehemu za siri-Genital warts


Maotea sehemu za siri ni aina mojawapo ya aina ya ugonjwa wa zinaa unaotokea si kwa nadra sana na huambukizwa kwa njia ya zinaa. Nusu ya wanao jihusisha na ngono mara kwa mara haswa isiyo salama hupata maambukizi ya virusi hawa kwenye kipindi fulani katika maisha yao. Wanawake wana patwa sana na maotea haya kuliko wanaume.

Kama jina lilivyo maotea haya hudhuru sehemu za siri zilizo na umande kwenye maeneo ya siri. Maotea haya huweza  kuonekana kama kitu mwinuko mdogo mrefu au kuwa na umbo la uwa lililosambaa. Kwa watu wengi huwa na umbo dogo sana na kuonekana kwa shida.

Kama maotea yanayoweza kutokea sehemu yoyote ya mwili, maotea sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya kirusi cha Human papilloma (HPV). Baadhi ya aina ya virusi hawa huweza kusababisha saratani za aina nyingi kama saratani ya shingo ya kizazi. Kuna chanjo pia ya kuzuia kupata baadhi ya virusi hawa wa HPV.

Dalili

Kwa wanawake maotea sehemu za sili huweza kukua kwenye kuta kati ya haja kubwa na uke, kwenye haja kubwa, kwenye uke na kwenye shingo ya kizazi. Kwa wanaume hukua kwenye kwenye kichwa au mpini wa uume, kwenye pumbu, au nje ya njia ya haja kubwa. Maotea sehemu za siri huweza kutokea kwenye mdomo au koo kwa mtu aliyekuwa akishiriki ngono kwa njia yam domo na mtu aliye na virusi hao.

Dalili huwa pamoja na;

  • Uvimbe mdogo, mbichi rangi ya kijivu kwenye sehemu za siri
  • Maotea mengi kwa pamoja yanayotengeneza umbo la ua
  • Kuwashwa na kujihisi vibaya kwenye maeneo ya siri
  • Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana

Mara nyingi, maotea sehemu za siri huweza kuwa madogo sana na haiwezekani kuonekana kwa macho. Wakati mwingine huweza  kuwa makubwa zaidi na kuwa kwenye mkusanyiko.


Kisababishi

Kirusi cha human papilloma (HP) husababisha maotea sehemu za siri. Kuna aina zaidi ya 40 ya kirusi huyu wanaodhuru sehemu za siri.

Kirusi huyu huambukizwa kwa njia ya zinaa, kwa kawaida mtu anakuwa na kinga ya mwili nzuri ya kuwaua virusi na mara wanapo mwili mgonjwa hutapata dalili na viashiria vyake. Baadhi ya watu walio na kinga ya mwili ya chini kwa sababu mbalimbali huweza kupata maaambukizi haya na kuota vinyama sehemu za siri.

Vihatarishi

Shirika linalojihusisha na mambo ya afya la CDC limelipoti kwamba nusu ya wanawake wanaoshiriki ngono hupata maambukizi wakati Fulani kwenye maisha yao. Baadhi ya vihatarishi ni kama

  • Kushiriki ngono na wapenzi wengi pasipo kutumia kondomu
  • Kuwa na historia ya kuumwa  magonjwa ya zinaa
  • Kuwa na mpenzi ambaye hujui historia yake ya mapenzi
  • Kuanza kushiriki mapenzi kwenye umri mdogo

Madhara

Madhara yanaweza kuwa;

Saratani- Saratani ya shingo ya kizazi imekuwa ikihusishwa na maambukizi ya baadhi ya virusi vya HP, aidha aina kadhaa ya saratani kama saratani ya uke, njia ya haja kubwa, uume na saratani ya kinywa na koo huchangiwa na kirusi huyo pia. Kirusi cha HPV sio mara zote husababisha saratani lakini ni muhimu kwa wanawake kuwa na utaratibu wa kupima kipimo cha pap smear, haswa ukiwa umeambukizwa na kirusi huyu.

Matatizo katika ujauzito- Maotea ya sehemu za siri huweza kusababisha matatizo wakati wa ujauzito kama ugumu kukojoa, kwenye mlango wa uke huweza kusababisha mtoto kushindwa kutoka wakati wa kujifungua kwa sababu hudhuru utanukaji wa tishu za mlango wa uzazi, kutokwa na damu sana endapo vimbe zitachanika wakati wa kujifungua

Mara chache, mtoto anayezaliwa na mama mwenye maotea sehemu za siri huweza kupata maambukizi hayo kwenye koo.

Vipimo na uchunguzi

Kwa sababu ni vigumu kutambuwa vinyama vidogo sana sehemu za siri, daktari anaweza kupaka dawa kwenye maeneo hayo ya siri ili kufanya vinyama view vyeupe ili kuchugulia kwa kutumia hadubini maalumu.
Vinyama vilivyo kuwa zaidi huonekana kwa macho na mara nyingi mtaalamu wa afya hata hitaji vipimo zaidi ili kutambua.

Kipimo cha pap
Kwa wanawake ni vema kuwa na kipimo hiki kila baada ya muda fulani kupita, kipimo hiki kinaweza kusaidia kutambua mabadiliko yanayo sababishwa na kirusi  huyu kwenye uke na shingo ya kizazi mapema zaidi yanayo ashiria dalili za awali za saratani ya shingo ya kizazi. Kujua kipimo hiki kinavyo fanyika soma makala ya saratani ya shingo ya kizazi katika mtandao wetu.

Kipimo cha kirusi cha HP

Sehemu tishu za shingo ya kizazi huchukuliwa na kupimwa wakati wa kipimo cha pap smear ili kutambua aina ya kirusi.

Kipimo hiki kwa sasa kimehifadhiwa kutumika kwa wanawake wenye umri wa miaka 30 na zaidi. Hakitumiki sana kwa umri mdogo kwa sababu kinga zao za mwili huua virusi hawa bila matibabu yoyote ya dawa.

Matibabu na dawa

Kama maotea haya sababishi kujihisi vibaya, matibabu hayatahitajika. Endapo dalili zako zinahusisha kuwashwa, kuungua na maumivu au kama maoteo yanaonekana makubwa huweza kusababisha mtu kujihisi vibaya. Daktari wako anaweza kukupa matibabu ya dawa au upasuaji, hata hivyo maoteo huweza kujirudia kwa baadhi ya wagonjwa wenye kinga za chini za mwili mara nyingi miezi sita. Watu wenye kisukari, UKIMWI au wanaotumia madwa Fulani yanayoshisha kinga ya mwili hupata hali hii ya kujirudia kwa vijivimbe sehemu za siri.

Madawa

Dawa  imiguimond- huongeza kinga za mwili ili kupambana na kirusi huyu anaye sabaisha maotea, hii ni dawa ya klimu inayo pakwa kwenye vinyama vya maotea. Dawa hii huweza kudhoofisha kondomu au vizuizi na huweza kusababisha miwasho kwa mpenzi wako.

Maudhi ya dawa hii ni kuleta wekundu wa ngozi, malenge lenge, maumivu, kikohozi na uchovu.

Podophyllin na podofilox- ni dawa inayotafuna vinyama vya maotea kwa kuunguza . Unatakiwa kuchukua tahadhari unapotumia hii dawa kwani huweza kula sehemu zingine za mwili. Podofilox huwezwa kutumiwa na mgonjwa akiwa nyumbani akiwa anapaka mwenyewe lakini podophyllin ni lazima ipakwe na daktari wako.

Trichloroacetic acid (TCA) Hii ni dawa  inayounguza maotea. Hupakwa na daktari, huweza ku sababisha maumivu na michomo kwenye sehemu iliyopakwa.
Interferon- dawa inayo sababisha kuamka kwa kinga za mwili na kupambana na ugonjwa, ipo kwenye mfumo tofauti, ya kuchoma  na kupaka, tafiti zinaonyesha hufanya kazi vema inapochomwa.

Sinecatechinis- dawa hii hai julikani inafanya kazi vipi, lakini huweza kutumiwa na mgonjwa nyumbani, huongeza kinga ya mwili na kuua chembe za kwenye maotea, hupakwa kwa mda wa wiki 16. Haitakiwi kutumika ndani ya uke au mlango wa haja kubwa, kwa watu wenye kinga ya chini ya mwili au kwa wanawake wenye tete kuwanga.

Upasuaji
Matibabu ya upasujai hufuata endapo matibabu dawa hayajafanikiwa, upasuaji huweza kuwa wa aina mbalimbali kama
  • Kugandisha chembe na kukata
  • Kukata maotea kwa kutumia kisu cha umeme
  • Kukaka kwa kutumia kisu cha upasuaji
  • Matibabu ya mionzi ya laser

Matibabu haya hutofautiana nchi na nchi pia hutegemea upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitalimbalimbali.

Kujikinga
Tumia kondomu, kondomu inaweza kuzuia kupata maambukizi haya, ingawa inaweza kuzuia kwa asilimia kadhaa unaweza kupata pia kwa sababu haitendi kazi asilimia 100

No comments

Post a Comment