MOLAR PREGNANCY - TATIZO LA MIMBA KURUTUBISHWA LISITENGENEZE MTOTO




Hii ni hali ya yai baada ya kurutubishwa  kutengeneza vitufe vidogo vidogo mithiri ya zabibu kwenye mji wa mimba. Tatizo hili  linatokana na matatizo kwenye kondo la nyuma (placenta) yanayotokana na matatizo kwenye vinasaba.

Tatizo hili lipo kwa aina mbili.
1.partial molar pregnancy
2.complete molar pregnancy

1.partial molar pregnancy
Hii ni pale Mtoto anatengenezwa ila kondo la nyuma (placenta) linakuwa haliko kawaida.Tishu za placenta zinatengeneza Vitufe vidogo vidogo.Mtoto hawezi kuendelea kukua kutokana na matatizo ya placenta.
Tokeo la picha la Molar pregnancy

2.complete molar pregnancy
Hapa ni hali ambayo kunakuwa hakuna mtoto wala kondo la nyuma bali yai baada ya kurutubishwa linatengeneza tu vitufe hivyo tu.

Picha inayohusiana
DALILI ZA TATIZO HILI
1.kichefu chefu na kutapika sana. Endapo mama anapata tatizo la kutapika sana hadi.kuishiwa maji muhimu kucheki tatizo hili.
2.kutokwa damu ukeni.
3.Shinikizo la damu/presha kuwa juu
4.kiwango cha hormone ya HCG kuwa juu
5.dalili nyingine za mimba zinaweza,kuwepo pia.

UTAJUA VIPI UNA TATIZO HILI
tatizo hili linapimwa kwa kipimo cha ultrasound ambapo katika picha ya ultrasound inaonekan kama fungu la zabibu.


TATIZO HILI LINATIBIKA VIPI?
Mara nyingi mimba ya aina hii inatoka yenyewe, mama atatokwa na damu zimeambatana na vitu mithili ya zabibu.

Endapo haitatoka yenyewe basi anapata msaada wa mimba hii kutolewa kwa njia maalumu inayojulikana kama dilation and curratage.

No comments