Si
mara chache tumewahi kushuhudia au kusikia mtu au kundi la watu
likiugua ghafla baada ya kula chakula katika mkusanyiko au sherehe. Bila
shaka nawe ni mmojawapo wa waliowahi kukumbwa na hali hii.
Aidha
tumewahi pia kusikia au kushuhudia hata baadhi ya watu wakiamini
kulishwa sumu baada ya kula chakula katika shughuli au sherehe fulani.
Hali hii imewahi kuzusha tafrani na sintofahamu miongoni mwa wanajamii
kwa vile si wengi wanaofahamu hasa chanzo cha hali hiyo.
Lakini usumu au maambukizi katika chakula (food poisoning) ni nini hasa?
Food
poisoning ni hali ya kuchafuka kwa chakula kunakotokana na uwepo wa
vimelea mbalimbali kama vile bacteria, virusi, au parasites au sumu zao
ndani yake. Hali hii hutokea wakati unapokula chakula au kunywa
vinywaji/maji yaliyochanganyika na vimelea hawa hususani vya bacteria wa
jamii ya Staphylococcus au Escherichia coli (E. coli).
Ieleweke
kuwa food poisoning haimaanishi sumu inayowekwa na mtu/watu kwenye
chakula bali hutokana na vijidudu vya magonjwa mbalimbali kama vile
bacteria.
Vihatarishi vyake
Kwa
kawaida food poisoning hutokea zaidi baada ya kula vyakula
vilivyoandaliwa kwenye mikusanyiko kama vile cafeteria za shule au
kazini, kwenye misiba, matanga, hitma, maulid, ngoma, harusi, mahoteli,
na mikusanyiko mingine yeyote ambayo inahusisha ulaji wa chakula cha
pamoja; ambapo mtu mmoja au kundi la watu hupatwa na usumu huo na kuwa
wagonjwa.
Watoto
wadogo chini ya mwaka mmoja pamoja na wazee ni miongoni mwa makundi ya
watu wanayoongoza kuwa katika hatari ya kuathirika zaidi na tatizo hili.
Wengine ni pamoja na watu wenye matatizo ya kiafya kama vile magonjwa
ya figo au kisukari, wenye upungufu wa kinga ya mwili, na wasafiri
wanaotembelea maeneo yanayojulikana kuwa na vimelea wanaosababisha hali
hii kwa wingi.
Visababishi
Kama
ilivyotangulia kuelezwa hapo awali, food poisoning husababishwa na sumu
inayotokana na vimelea vya bacteria, virusi, au parasites. Vimelea hawa
hujumuisha bacteria jamii ya
• Clostridium botulinum wanaosababisha usumu unaoitwa botulism
• Campylobacter wanaosababisha uambukizi kwenye utumbo mdogo kuharisha na kutapika
• Vibrio cholera wanaosababisha kipindupindu
• E. coli ambao pia husababisha uambukizi katika utumbo mdogo, kuharisha na kutapika
• Bakteria wengine ni pamoja na Staphylococcus aureus, Salmonella, Listeria na Shigella ambao husababisha kuharisha damu, na aina fulani ya bacteria wanaopendelea kuishi kwenye magamba ya samaki.
• Clostridium botulinum wanaosababisha usumu unaoitwa botulism
• Campylobacter wanaosababisha uambukizi kwenye utumbo mdogo kuharisha na kutapika
• Vibrio cholera wanaosababisha kipindupindu
• E. coli ambao pia husababisha uambukizi katika utumbo mdogo, kuharisha na kutapika
• Bakteria wengine ni pamoja na Staphylococcus aureus, Salmonella, Listeria na Shigella ambao husababisha kuharisha damu, na aina fulani ya bacteria wanaopendelea kuishi kwenye magamba ya samaki.
Vimelea vya sumu huingiaje kwenye chakula?
Kuna
njia kadhaa ambazo hutumiwa na bacteria kuvamia chakula na hatimaye
kuzalisha sumu zao na hivyo kukichafua. Njia hizo ni pamoja na
• Maandalizi pamoja na upikaji mbaya wa chakula
• Maji yasiyo safi na salama yanaweza kuwa na kinyesi cha binadamu au wanyama ambacho huwa kimebeba vimelea hawa
• Nyama inapogusana na utumbo/matumbo ya wanyama yenye vimelea hawa wakati wa kuchinja, kuchuna ngozi na kuandaa nyama
• Maandalizi pamoja na upikaji mbaya wa chakula
• Maji yasiyo safi na salama yanaweza kuwa na kinyesi cha binadamu au wanyama ambacho huwa kimebeba vimelea hawa
• Nyama inapogusana na utumbo/matumbo ya wanyama yenye vimelea hawa wakati wa kuchinja, kuchuna ngozi na kuandaa nyama
Aidha mtu anaweza kupata food poisoning baada ya kula au kunywa
• Chakula kilichoandaliwa na mtu mwingine au yeye mwenyewe bila kusafisha vema mikono yake
• Chakula kilichoandaliwa kwa kutumia vyombo vichafu kama vile masufuria machafu, majungu, vijiko, visu, vikombe, sahani au vyombo vingine vinavyotumika kuandaa au kulia chakula.
• Vyakula vya jamii ya maziwa, jibini, mtindi ambao umewekwa kwenye friji kwa muda mrefu bila uangalizi wa kutosha.
• Vyakula vilivyohifadhiwa kwenye jokofu katika joto lisilo sahihi bila kuvipasha tena moto
• viporo visivyohifadhiwa vema
• samaki wabichi/wasioiva au kamba kochi
• matunda au mboga mboga mbichi zisizooshwa vizuri
• saladi isiyoandaliwa vema
• nyama isiyoiva vema au mayai mabichi
• maji kutoka katika bomba bila kuchemsha hususani kama limepasuka
• Chakula kilichoandaliwa kwa kutumia vyombo vichafu kama vile masufuria machafu, majungu, vijiko, visu, vikombe, sahani au vyombo vingine vinavyotumika kuandaa au kulia chakula.
• Vyakula vya jamii ya maziwa, jibini, mtindi ambao umewekwa kwenye friji kwa muda mrefu bila uangalizi wa kutosha.
• Vyakula vilivyohifadhiwa kwenye jokofu katika joto lisilo sahihi bila kuvipasha tena moto
• viporo visivyohifadhiwa vema
• samaki wabichi/wasioiva au kamba kochi
• matunda au mboga mboga mbichi zisizooshwa vizuri
• saladi isiyoandaliwa vema
• nyama isiyoiva vema au mayai mabichi
• maji kutoka katika bomba bila kuchemsha hususani kama limepasuka
Zipi ni dalili za food poisoning?
Dalili
za mtu mwenye food poisoning hutegemea na aina ya vimelea
wanaosababisha hali hii. Kwa kawaida, vyanzo vingi vya food poisoning
huwa na dalili zinazojitokeza ndani ya saa 2 mpaka 6 tangu mtu anapokula
chakula chenye usumu. Baadhi ya dalili za ujumla ni pamoja na
• maumivu ya tumbo. Tumbo huwa kama linakata au kusokota.
• maumivu ya tumbo. Tumbo huwa kama linakata au kusokota.
• Homa na kujihisi baridi
• Kuumwa kichwa
• Kichefuchefu na kutapika
• Kuharisha, kulingana na chanzo mtu anaweza kuaharisha majimaji au kuharisha damu
• Mwili kuwa dhaifu na kulegea. Ulegevu wa mwili unaotokana na usumu wa botulism waweza kuwa mbaya sana kufikia kusababisha mtu kushindwa kupumua sawasawa na hatimaye kifo.
Vipimo na uchunguzi
Mara
unapofika kwa hospitali, daktari pamoja na kukuuliza maswali ili
afahamu vizuri historia na chanzo cha ugonjwa, pia atakupima ili
kutambua viashiria vingine kama vile upungufu wa maji mwilini au maumivu
ya tumbo. Daktari atakuuliza kuhusu vyakula au vinywaji ulivyokula na
kunywa saa kadhaa zilizopita, kama uliandaa mwenyewe au la, ulikuwa au
kunywa wapi, kama kuna wengine wenye dalili kama zako, dalili nyingine
kama kuharisha, kutapika, vichefuchefu, maumivu ya tumbo, homa au dalili
nyingine kama zilivyotajwa hapo juu.
Daktari
pia anaweza kushauri ufanyike uchunguzi kama wa damu, mkojo, choo,
matapishi, au masalia ya vyakula ili kutambua chanzo cha ugonjwa wako.
Hata hivyo ieleweke kuwa wakati mwingine vipimo hivi vinaweza kushindwa
kuthibitisha kwamba ugonjwa wako unatokana na kuwepo kwa usumu kwenye
chakula. Baadhi ya wagonjwa wanaoharisha damu wanaweza kuhitaji
kufanyiwa vipimo zaidi ili kutambua chanzo cha kuharisha damu ili
kujiridhisha kuwa hakuna uhusiano na food poisoning.
Matibabu
Wagonjwa
wengi wa food poisoning kwa kawaida hupona kabisa baada ya siku chache
tangu kujitokeza kwa dalili. Jambo la msingi ni kuhakikisha unaendelea
kula na kunywa vinywaji au maji ya kutosha ili kurejesha kiasi chochote
cha maji kitakachopotea kutokana na kuharisha au/na kutapika.
Haishauriwi
kula vyakula vigumu mpaka kuharisha kutakapokoma, na jiepushe kula
vyakula vya jamii ya maziwa (maziwa, mtindi) ili kupunguza uwezekano wa
kuharisha zaidi, wakati huo huo kunywa maji ya kutosha au vinywaji
vingine kwa wingi.
Watoto
wadogo ni vema wapewe maji yenye madini maalum ya ORS au kama
hayapatikani, maji yenye mchanganyiko wa chumvi na sukari hufaa sana.
Wagonjwa hususani watoto wanaoharisha na kutapika na ambao hawawezi
kunywa maji wala vinywaji kwa sababu ya kutapika hawana budi kutibiwa
kwa kutumia drip (i.v. fluids) ili kurejesha maji yaliyopotea.
Mara
nyingi, matibabu ya food poisoning hayahusishi utumiaji wa dawa za
jamii ya antibiotics isipokuwa mara chache sana daktari wako anaweza
kushauri utumie dawa hizo hususani kama kunaambatana na kuharisha damu.
Nini cha kutarajia kwa mtu aliyepatwa na food poisoning?
Kwa
kwaida watu wengi wenye kupatwa na hali hii hupata nafuu kamili ndani
ya saa 12 mpaka siku mbili; ingawa wapo baadhi ambao hali zao zinaweza
kuwa mbaya sana. Ni mara chache food poisoning husababisha kifo lakini
kama mgonjwa anaharisha sana na kutapika bila kutibiwa, kifo kinaweza
kutokea kwa sababu ya upungufu mkubwa wa maji mwilini.
Nini madhara ya hali hii?
Madhara
yaliyozoeleka zaidi ya hali hii ni upungufu wa maji mwilini unaotokana
na kutapika na kuharisha kupita kiasi bila kurejesha maji yanayopotea.
Madhara
mengine hutegemeana na aina ya bacteria anayesababisha ugonjwa huu.
Bacteria wengine husababisha madhara kama vile magonjwa ya figo,
matatizo ya kutokwa damu bila kukoma, magonjwa ya viungo vya mwili,
magonjwa ya mfumo wa fahamu, na madhara katika moyo.
Kinga ni bora kuliko tiba
Kujikinga
ni bora kuliko kusibiri mpaka tatizo litokee. Unashauriwa kuepuka kula
vyakula ambavyo ubora na usafi wake unatia shaka. Aidha epuka kunywa
vinywaji au maji ambayo si safi na salama pamoja na kuacha kula nyama au
samaki wasiopikwa vizuri.
Unashauriwa
kwenda hospitali haraka iwapo utaona damu au usaha katika kinyesi
chako, kinyesi kimekuwa cha rangi nyeusi, tumbo linazidi kusokota hata
baada ya kujisaidia, kujihisi dalili za kukaukiwa maji mwilini kama vile
kiu, kizunguzungu au kujihisi kichwa chepesi, kuharisha pamoja na homa
kali, moyo unakwenda kasi au una dalili nyingine za tatizo hili.



No comments