kuangalia picha za ngono inaweza kusababisha
tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwani Ubongo unapokua na mohemko kwa muda mrefu mikali huzoea mihemko
hiyo na baada kutopata mihemko hiyo kabisa.
NINI HUTOKEA.
Ubongo huzalisha kemikali inayoitwa dopamine ambayo kazi
yake hii inakufanya utamani au huwe na hamu na vitu vinavyouzawadia mwili mfano
vyakula na tendo la ndoa. Mfano unapoona chakula ubongo unazalisha hii dopamine
ili upate hamu ya kula. Vivyo hvyo unapoona mwanamke mzuri kwako inazalishwa na
kukupa matamanio na kupelekea process ya uume kusimama kuanza.
Sasa picha za ngono hiathiri mfumo huu kwa kufanya ubongo
kuzalisha kwa wingi sana kuliko kawaida kwa Dopamine hivo kupelekea ubongo
kuzoea kiwango kikubwa hiki cha dopamine na hivo kufanya uhitaji kiwango kikubwa zaidi cha mhemko zaidi ya awali ili uume usimame,hali inayopelekea mtu kutopata mhemko wa
kutosha kufanya uume kusimama vzuri akiwa na mwanamke.Hai hii humwathiri mtu kwa kumfanya kwamba ubongo uzoee tu kiwango kikubwa cha dopamine anachokipata kwa kuangalia video au picha za ngono na kufanya kiwango cha dopamine kinachosababishwa na akiwa na mwanamke kuwa kidogo kwake kusababisha mhemko au uume kusimama matokeo yake akiwa na mwanamke uume kutosimama vizuri au kutosimama kabisa.Pia anavyozidi kuangalia picha hizi na kujichua kiwango kinachosababishwa na kufanya vitu hivi nacho kinakuwa kimezoeleka na ubongo hivyo anaweza kupata tatizo la uume kutosimama kabisa hata akiwa anajichua au anaangalia picha hizi.

Pia dopamine hii inavyozidi kiasi cha kawaida kwa muda mrefu inaathiri uzalishwaji wa hormone ya testosterone ambayo ni muhimu katika nguvu za kiume na a ya tendo la ndoa hali inayokuacha na tatizo la kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa.
Kwa wanawake kuangalia picha hizi hupelekea pia ubongo kuzoea kiwango kikubwa cha dopamine na kusababisha mwanamke asiwe anapata raha akikutana na mwanamke au kumsababishia tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Unaweza kukuta mtu huyo huyo akirudia kuangalia picha au
video hiyo hiyo siku inayofata hapati mhemko sana kama jana yake kwa sababu
ubongo wake ushazoea kiwango kikubwa cha dopamine kilichozalishwa jana yake na
video au picha hiyo anavyoendela kuiangalia inafikia hatua anapoiangalia hapati kabisa mhemko.
Kwa hiyo unaweza kuona kitu hiki kinavyoweza kuathiri uume
kusimama unapokuwa na mwanamke.
Vivyo hvyo tatizo la kujichua wengi huamini kwamba
linadhoofisha uume,ila ni kwamba nalo linaathiri nguvu za kiume kwa njia hii.
Pia kiwango kikubwa cha dopamine kwa muda mrefu huathiri
sehemu ya ubongo inayohusika na kufanya maamuzi
mbali mbali ijulikanayo kama CINGULATE CORTEX
Kiufupi unapotaka kufanya tendo la ndoa au unapokuwa na
mwanamke ubongo unazalisha dopamine hii inafanya upate mhemko,na kufanya damu
nyingi kwenda kwenye mishipa ya uume na misuli ya uume kuzalisha kemikali ya
nitric oxide na kufanya mishipa mikubwa (chambers) za uume kujaa damu na
kufanya uume kusimama. Kwa hiyo kusimama kwa uume inategemea sana na jinsi gani
ubongo umeipokea kemikali ya dopamine.
HABARI NJEMA.
Ni kwamba suluhisho la hali hii ni
kuacha kuangalia picha za ngono ,au kujichua. Unapoacha kufanya hivyo mwili na
ubongo huanza kuzoea kiwango cha kawaida cha Dopamine na kurudia katika hali
yako ya mwanzo.


No comments