Heshimu hamu ya kula ya mwanao- Kama
mwanao hana njaa, usimlazimishe kula chakula au kitu chochote kile cha
kutafuna. Vivyo hivyo usimlazimishe mwanao kufasisha sahani yaani
kumaliza chakula chote ulichomuwekea. ukifanya hivyo jambo hili huweza
kusababisha mtoto kujilazimsha kula. Kwa kuongezea Mtoto anaweza kupata
wasiwasi na kukataa au kuwa na hisia kidogo ya njaa na hivo tumbo lake
huwa kama limejaa.
Mwekee au mpe chakula kiasi-Kufanya hivi unaweza kuzuia mtoto kuona balaa la chakula,pa utampa uwanja aombe zaidi kama bado hajashiba.
Fuata utaratibu wako-Kula
au mpe chakula mtoto muda na wakali ule ule kila siku. Unaweza kumpa
maziwa ama juisi ya matunda na chakula. Katikati ya mlo mmoja na
mwingine mpe mwanao maji na vitafunwa vingine. Ukiacha mwanao anywe maji
tu na juisi na vitafunwa siku nzima huweza kupunguza hamu ya kula
chakula.
Uwe mvumilifu na chakula kigeni-Watoto
wadogo mara kwa mara hushika na kunusa chakula kigeni, na huweza kuweka
kiwango kidogo mdomoni na kisha kutema. Mwanao anaweza kuhitaji
kuonyeshwa chakula hicho mara kwa mara kabla hajaanza kula chakula
hicho.
Mtie
moyo mwanao kwa kuzungumzia rangi ya chakula, umbo na harufu na kama
kina radha nzuri. Weka chakula kipya kila unapokuwa unampa chakula
anachokipenda ili akizoee na hicho pia.
Mshawishi-Weka
chakula kwenye sahani nzuri ama kisosi anachokipenda. Unaweza
kukata chakula chako kwenye maumbo mbalimbali kwa kutumia kisu ili
kumvutia. Mpe vyakula anavyokula asubuhi kama kifungua kinywa wakati wa
usiku. Mpe chakula chenye rangi nzuri ya kuvutia.
Mwache mwanao akusaidie kufanya manunuzi-Ukiwa
umeenda kununua vitu vya kula, mpe nafasi ya kuchagua matunda, mboga za
majani na vyakula vingine vyenye afya. Usinunue chochote tu ambacho
hutaki mwanao ale. Ukiwa nyumbani, mshawishi mwanao akusaidie kuosha
mboga, atwange karanga ama aandae meza.
Kuwa mfano-Kama ukila vyakula vyenye afya njema mwanao pia atafuata jambo hilo
Kuwa mbunifu-Weka
vipande vidogo vya matunda kwenye sahani ya chakula cha nafaka, au weka
karoti kwenye supu nk. Fanya ubunifu mbalimbali kiasi kwamba mtoto
akipende chakula.
Punguza uharibifu wa mawazo ya mtoto-Zima
TV yako na vifaa vingine vya umeme ili kumsaidia mtoto awaze kula tu.
Kumbuka pia matangazo ya TV kuhusu chakula huweza kumfanya mtoto apende
kula vitu vyenye sukari ama kutokula vyakula vyenye afya.
Usimpe kitindamlo kama zawadi-Kusimamisha
kumpa kitindamlo mwanao kuna mpa ujumbe kwamba kitindamlo ni chakula
kizuri, ambapo kinaweza kumfanya mwanao apende vitu vitamu tu. unaweza
kuchagua siku moja au mbili kwa wiki wakati wa usiku kama usiku wa
kutumia vitindamlo na usimpe siku zingine za wiki au mzoeshe mwanao
kwamba vitindamlo ni matunda, maziwa au vyakula vingine vyenye afya ili
awe anavipenda na kula kila siku au mara kwa mara.
Fahamu pia
Kuandaa
chakula kingine mara baada ya mtoto kukataa kile ulichoandaa huweza
kusababisha mtoto kuwa mchaguzi wa chakula Fulani tu. Mtie moyo mwanao
akae mezani kwa mda wote mnapokuwa manakula hata kama hali hicho
chakula. Endelea kumpatia chakula chenye afya mwanao mpaka pale
atakapotambua na kuvifahamu vyakula na pendeleo lake.
Kama
una wasiwasi kuhusu mwanao kuchagua chakula kwamba kunamdhuru afya na
maendeleo yake ya ukuaji, onana na daktari wa mwanao. Daktari atachora
chati ya uzito na maendeleo ya ukuaji wa mtoto. Kwa nyongeza weka rekodi
ya aina na kiasi cha chakula anachokula kwa siku tatu zilizopita.
Daktari atapata picha na atakusaidia kukutoa wasiwasi. Rekodi ya chakula
alichokula siku za nyuma huweza kumsaidia daktari kutambua tatizo
lolote lile.
Kwa
sasa kumbuka, tabia ya ulaji wa mtoto haiwezi kubadilika ghafla uamkapo
asubuhi- lakini hatua ndogo ndogo zinazochukuliwa kila siku huweza
kusaidia ulaji wa chakula bora kwa maisha yake yote.

No comments
Post a Comment