Mara
nyingi alama hizi za michirizi humtokea mtu maeneo ambayo kwa asilimia
kubwa huwa na mafuta (fat), mfano katika mwili hutokea mara nyingi
kwenye mapaja, upande wa juu wa mikono (biceps), tumboni, kwenye
makalio, pia kwa baadhi ya watu hutokea maeneo ya kifuani au kwenye
matiti kwa wanawake.
kwa kawaida michirizi hii huwa haimletei mtu maumivu ya aina yoyote, bali jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu. Kwa baadhi ya watu michirizi hii huwa ni mikubwa sana, na kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na amani pindi anapokuwa mbele za watu kwa kutegemeana na michirizi hiyo imetokea sehemu gani ya mwili.
VISABABISHI
michirizi hii hutokana na kutanuka kwa
ngozi na ongezeko la hormone ya Cortisone
ambayo inazalishwa na tezi zilizopo kwenye figo kitaalamu zinajulikana
kama adrenal glands.Hormone hii huathiri uwezo wa ngozi kutanuka na kusinyaa.
Vitu gani vinaweza kupelekea tatizo hili.
1.wakati wa ujauzito kutikana na ngozi
ngozi ya tumbo kutanuka kwa kasi kuendana na ukubwa wa tumbo na mtoto.
2.Michirizi hii inaweza kutokea pale
unapoongezeka uzito au kupungua kwa kasi
3.Matumizi ya dawa za kupaka (cream) zilizo
katika group la CORTICOSTEROID Mfano Carolight kwani hizi huathiri uwezo wa
ngozi kutanuka na kusinyaa.
4.magonjwa mfano Cushing's syndrome,marfans
syndrome na ehlers danlos syndrome.
WATU GANI WAKO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI
1.wanawake wanene
2.wajawazito
3.watu wenye ngozi nyeupe
4.wajawazito
5.kubeba mimba ya mapacha
6.kupungua uzito kwa kasi
7.wanaotumia cream zenye Corticosteroids.
MATIBABU
Michirizi hii hupotea baada ya muda fulani,
ila inachukua muda mrefu sana.zipo dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutibu
tatizo hili ila inahitajika kutumika kwa muda mrefu ili kupata matokeo.
Dawa hizi ni kama ifatavyo
1.Tretnoin cream
Hii hufanya kazi kwa kuipatia ngozi protini
aina ya collagen ambayo ndo inahusika katika kuweka sawa uwezo wa ngozi
kusinyaa na kutanuka.
ANGALIZO; cream hii haipaswi kutumika kipindi cha ujauzito.
2.pulse dye laser therapy hii ni tiba ya
kutumia mionzi
3.microdermabrasion
Pia
matumizi ya mafuta ya kujipakaa yenye mchanganyiko wa vitamini E
husaidia kuijenga ngozi na kutoa makovu na michirizi. Ulaji wa vyakula
na kunywa vinywaji vyenye vitamini A, D na E huimarisha ngozi.
MATIBABU YA NYUMBANI
1.Kupaka mafuta ya nazi kwenye sehemu iliyoathirika husaidi kwenye tatizo hili
2.Aloevera,kwa kupaka maji maji ya mmea wa aloevera husaidia kutibu tatizo hili.Mafuta
ya Aloe vera, pakaa mafuta haya katika ngozi yenye michirizi, pia
unaweza kuyachanganya na vitamini A na ukapakaa ngozi yako.
3.sukari
Sukari inatumika kwa kufanya scrub katika shemu iliyoathiriwa na tatizo hili. Fanya kama ifatavyo.
1.Changanya sukari na mafuta ya nazi au almond oil
2.ongezea maji ya limao
3.scrub eneo lililoathirika kwa muda wa dakika 8 hadi 10.
4.Fanya hivi angalu mara tatu kwa wiki.
4.VIAZI MVIRINGO
Tumia
vipande vidogo vidogo vya viazi kufuta sehemu ya ngozi yenye michirizi,
ruhusu juisi au maji maji ya kwenye viazi yakae katika ngozi, na kisha
baadae unaweza kuosha ngozi yako kwa maji ya vuguvugu, kwani viazi vina
madini na vitamini ambazo zikinyonywa katika ngozi, husaidia kuondoa
michir

No comments
Post a Comment