Kuna maana 4 za maji kidogo kwenye uzazi, kuna ugumu ipi ni maana nzuri ya kuelezea kiwango kidogo cha maji kenye uzazi. AFI chini ya sentimita 5 au vipimo viwili vya kina kirefu tumboni vikiwa chini ya sentimita 2 au vizio viwili chini ya sentimita za ujazo 15.
Nini huweza kuwa sababu za maji kidogo kwenye uzazi?
Matatizo ya chromosome /madhaifu ya uumbaji
Mtoto kukosa hewa ya oksjeni(huelekea kiwango kidogo cha maji ya plazma kwa mtoto na kupungua kwa kiwango cha mkojo.
Ujauzito umepitiliza wiki 40(mtoto hunywa maji mengi na uzalishaji hupungua/kusimama)
Mama kuishiwa maji
Kupasuka kwa chupa ya uzazi
Madhaifu gani ya uumbaji huweza kusabaisha maji kidogo kwenye chupa ya uzazi?
Madhaifu katika uumbaji wa figo na kuziba kwa njia za mkojo(kutokana na kutofanyika kwa mirija ya mikojo) husababisha maji kidogo kwenye chupa ya uzazi.
Nini madhara ya maji kidogo
Madhaifu gani ya uumbaji huweza kusabaisha maji kidogo kwenye chupa ya uzazi?
Madhaifu katika uumbaji wa figo na kuziba kwa njia za mkojo(kutokana na kutofanyika kwa mirija ya mikojo) husababisha maji kidogo kwenye chupa ya uzazi.
Nini madhara ya maji kidogo miezi mitatu ya 2 kipindi cha ujauzito?
Kipindi cha miezi mitatu ya 2 wakati wa ujauzito upungufu wa maji husababisha kutofanyika vema kwa mapafu ya mtoto. Mtoto anapozaliwa hupata matatizo ya upumuaji.
Matibabu
Kama maana ya maji kidogo kwenye uzazi imepatikana kwenye ujauzito uliotimia umri, hii huwa sababu ya kujifungua haraka. Kuna ushahidi unaosema kwamba maji kidogo kwa ujauzito uliopitiliza umri huweza kusababisha mapigo ya moyo ya mtoto kutoridhisha na kujifungua kwa upasuaji. Hata hivyo hakuna tofauti kwa mtoto aliyezaliwa kwa mama aliye na maji kidogo au mengi kwenye ujauzito uliopitiliza umri.

No comments
Post a Comment