Thursday, 25 July 2019

KUHUSU MENO YA PLASTIKI KWA WATOTO,


Kwa kawaida binadamu anaanza kuota meno kuanzia umri wa miezi 6-10,lakini kuna baadhi ya watoto wanaweza kuzaliwa na meno au kuota meno ndani muda wa mwezi mmoja tu tangu kuzaliwa,hii inaibua maswali mengi kwa watu wa jamii yetu na wengine wanayaita meno ya plastiki na kuhusianisha meno haya na imani zingine,ila unachopaswa kujua ni kwamba huwa inatokea na haiwezekani kumkinga mtoto asizaliwe na meno.Sababu za kuota meno mapema au kuzaliwa na meno hazijadhihirishwa kisayansi lakini inahusianishwa na hitilafu za vinasaba.Mara nyingi watoto huzaliwa na meno ya mbele ya chini mara chache sana inaweza kuwa sehemu nyingine yeyote ya taya.

HALI HII INATOKEA KWA MTOTO MMOJA KATI TU YA WATOTO 2000-3000 WANAOZALIWA.


Meno haya yanaweza kuwa meupe au kahawia au rangi kama ya fizi.Mtoto anaweza kuwa na fizi zilizovimba na nyekundu, anaweza kupata kidonda hasa chini ya ulimi hii inaweza kumletea shida wakati wa kunyonya.
Meno haya yanaweza hata kuhatarisha afya ya mtoto iwapo yamelegea na hivo anaweza kuyameza/kupaliwa wakati wa kunyonya na kuleta hatari kwa maisha yake,meno haya yanaweza kumchubua au kumuumiza mama pale anaponyonyesha.
Ufanyaje kama mwanao amezaliwa na meno au meno yameota mapema?
Usiwe na wasiwasi uwepo wa meno haya hauthiri ukuaji wa mtoto wako.
Kwa ushauri fika kituo cha afya na uonane na daktari wa meno ili akague men ohayo na wakati mwingine huwa ni lazima kuyatoa
Wakati mwingine kama meno haya hayahatarishi afya ya mtoto wala mama yake n ayamekua vozuri ynaweza kubaki kinywani na baadae meno mengine yataota na mtoto anaweza kuyatumia kawaida t
Usijaribu kuyatoa meno haya mwenyewe kwani unaweza kumuumiza mtoto
Usikubali meno haya yatolewe na waganga wa kienyeji kwani wantumia vifaa ambavyo siyo salam mtoto wako anaweza kupata mammbukizi mbalimbali ikiwepo virusi vya ukimwi
angalizo....

No comments

Post a Comment